PICHA Ya Muonekano wa Soko jipya la Kariakoo Huu Hapa

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,750
21,204
Screenshot_2021_1108_172824.jpg

Picha za jengo jipya la Kariakoo zimeachiwa mapema leo, jengo hilo jipya linakusudiwa kugarimu shs za kitanzania 26.2 bilioni.
 
Soko la Uhindini Mbeya litajengwa lini? Hadi leo hata Michoro yake haijatoka
Haya ni matumizi mabaya ya pesa na mipango moji, wangerekebisha la zamani na wakajenga jipya Mbweni au Bunju au Pugu...nje ya mji ili kuepusha foleni mjini...wengine waalwkee kariakoo na wengine waelekee nje ya mji.
Kuelekeza huduma muhimu sehemu moka ni kuvutia msongamano wa magari.
Pili kariakoo hakuna maegesho ya magari ya kutosha
 
Katika kitu cha kusikitisha mara baada ya wanene kukaa na kushauriana kulijenga soko jipya lenye kuvutia, ni njia iliotumika kuwaondoa wauzaji katika hili soko ili kupisha ujenzi wa soko jipya.

● Waliona kuwaondoa kwa mdomo haitowezekana ili ujenzi ufanyike.

● Waliona kulibomoa na kujenga soko jipya ni kutafuta kupingwa kwa matumizi ya hela za wananchi.

Ikawa sasa tufanyaje?
 
Haya ni matumizi mabaya ya pesa na mipango moji, wangerekebisha la zamani na wakajenga jipya Mbweni au Bunju au Pugu...nje ya mji ili kuepusha foleni mjini...wengine waalwkee kariakoo na wengine waelekee nje ya mji.
Kuelekeza huduma muhimu sehemu moka ni kuvutia msongamano wa magari.
Pili kariakoo hakuna maegesho ya magari ya kutosha
Likijengwa Bunju kama lile la Ndungai au kama lile la Temeke.mtakuja hapa kuponda tena kwamba soko limejengwa nje ya mji hakuna wateja..kuishi na Wabongo ni kazi sana.
 
Likijengwa Bunju kama lile la Ndungai au kama lile la Temeke.mtakuja hapa kuponda tena kwamba soko limejengwa nje ya mji hakuna wateja..kuishi na Wabongo ni kazi sana.
Mji unakua soko likijengwa pembezoni itafanya kuwe na msomgamano mdogo wa magari
 
Likijengwa Bunju kama lile la Ndungai au kama lile la Temeke.mtakuja hapa kuponda tena kwamba soko limejengwa nje ya mji hakuna wateja..kuishi na Wabongo ni kazi sana.
Ukiwa kiongozi, jifunze kufanya kitu sahihi na sio vitu vizuri.
1. Kitu kizuri huvutia kwa mda mfupi
2. Kitu sahihi huwa kinaweza kisivutie kwa wakati huu lakini ni sahihi, kina faida ya muda mrefu.
Acha watu walalamike lakini huko mbeleni vuzazi vijavyo vitafaidi matunda na kukuona wewe ni shijaa wao.

Kujenga soko kubwa la kariakoo kwasasa ni jambo zuri lakini sio sahihi kwani hata lililopo halikidhi mahitaji hasa maegesho
 
Kwenye mid-level pamoja na single basement level, wajenge Self-Storage Units. Hizo storage units zitakuwa chanzo kikubwa sana cha mapato.
 
Wabongo hawana utamaduni wa kushop maduka ya ghorofani its either ni wavivu kupanda ngazi au wanaumwa magoti
 
Ukiwa kiongozi, jifunze kufanya kitu sahihi na sio vitu vizuri.
1. Kitu kizuri huvutia kwa mda mfupi
2. Kitu sahihi huwa kinaweza kisivutie kwa wakati huu lakini ni sahihi, kina faida ya muda mrefu.
Acha watu walalamike lakini huko mbeleni vuzazi vijavyo vitafaidi matunda na kukuona wewe ni shijaa wao.

Kujenga soko kubwa la kariakoo kwasasa ni jambo zuri lakini sio sahihi kwani hata lililopo halikidhi mahitaji hasa maegesho
Am sure wataweza parking kama ilivyo soko la kisutu
 
Miongoni mwa vitu vya kijinga zaidi na vya kifisadi katika utawala huu wa mama Samia na serikali ya CCM, basi mpango wa ujenzi wa soko la Kariakoo ni sehemu mojawapo. Ni ujinga mtupu.
Sababu ni hizi.

1. Zaidi ya 90% ya biashara zinazofanyika kwa sasa maeneo ya kariakoo hazitumii kabisa lile jengo la soko na hazihitaji uwepo wake, kariakoo haina shida ya maghorofa au majengo ya kufanyia biashara.

2. Ukiondoa sababu za kihistoria na alama ya kitovu cha shughuli za kibiashara maeneo ya kariakoo, jengo la soko kwa sasa ni kama halihitaji kabisa.

3. Eneo la kuweka miundo mbinu ya kuzunguka jengo jipya la kisasa kwa hapo kariakoo haipo kabisa, kuanzia car parking, barabara pana za kuingia na kutokea sokoni, njia za watembea kwa miguu nk. Ni hatari kiafya na kiusalama kutaka kujenga jengo kubwa zaidi.

4. Ujenzi wa masoko ya maghorofa huujawahi kuwa na matokeo yoyote mema kwa wanunuzi au wauzaji kibiashara popote. Ni kuchezea mtaji na kuwekeza kihasara.
 
Samia nae anaweka legacy zake kama Magu alivokuwa anaamua chochote atakacho,,,,Pesa za mazuzu (wtz) hazina kelele
 
Likijengwa Bunju kama lile la Ndungai au kama lile la Temeke.mtakuja hapa kuponda tena kwamba soko limejengwa nje ya mji hakuna wateja..kuishi na Wabongo ni kazi sana.
Yaan ni kazi kubwaa sanaa mkuu !!
Alafu hao hao wakiona picha za majiji ya watu nje ya Tz wana anza ku complain oh serikali yetu imejaa ufisadi oh vile .. tazama tazama ile soko ya magomeni pale inavyo pendeza ukilinganisha n zaman ..eti mtu unaingia CBD una anza kukutana na soko la makuti (kisutu market zaman) ..juzi raisi wa Znz aliongea kitu. Ambacho nafikir hata bara tuige ..HAM alisema wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi lzm ifanye kazi ya kuendeleza makazi bora ktk Znz ili kupanga nchi yao ..iyo ni point sanaa
 
Wawatie watu hasara halafu wanakuja kutamba na picha za jengo jipya.
 
Back
Top Bottom