Picha: Viongozi wa CUF watinga Ikulu leo!

Dubu ni mtaalamu wa kulala hata akiwa kasimama.

a1o1ua.jpg
 
Kila jambo alifanyalo CDM lazima wengine COPY - CUT, nasikia hadi bajeti, hoja wanaziiba toka kwenye vichwa vya CDM. hongera CDM kuwa proactive.
 
Hawa CUF kweli ichefu chefu. Hii yote ni kuhakikisha waliyofanya CHADEMA yakose maana. Sasa wao walikuwepo bungeni, wakaunga mkono mswada wa mume wao, ni nini tena wanataka kama sio mambo ya kitoto?

Wanadeka tu hao,hawana jipya wana kitu gani kipya ambacho hawakusema bungeni walipokuwa bega kwa bega kumsapoti mume wao ccm? nia yao na wao wafike ikulu baada ya kuona wapinzani wa kweli CHADEMA walienda huko, wakaona iwaje na wao wasiende wakati ndo masapota wakubwa wa ccm! eti walikuwa wanasawazisha goli,duu jamaa hawa!!!
 
ukiangalia timu hiyo hapo hasa ya upande wa serikali utaona utofauti na ile iliyokuwa imeandaliwa wakati jk anakutana na CDM hapo ndo utagundua kuwa CUF ni CCM B. maana hakuna jipya walilokwenda kulipeleka sana sana ni mambo ya kuiga tu.
rwtn3q.jpg
 
rwtn3q.jpg


JK kajua CUF hawana chochote cha kuibana serikali ndiyo maana hana ujumbe mkubwa wa serikali yake kama siku ile alipokutana na majembe ya CHADEMA. Si anajua wanakwenda kumfariji kutokana na maumivu aliyoyapata kutokana na kupelekwa puta na CHADEMA kwa siku mbili mfululizo?
 
ijumaa ijayo NCCR nao waende kuonja maji ya ikulu kisha wanaharakati nao waelekeee huko wakanywe juice ya ikulu halafu wananchi tuamue wenyewe hatutaki mtu wa kukaa bele yetu

Tutaenda 2015 na Rais kutoka chama chetu
 
Ni CUF waliotangulia kumuona Rais Ikulu ya Zanzibar enzi la Amani Karume. Hii itakuwa safari yao ya pili kwenda Ikulu kwa ziara za chama. Chadema ni mara yao ya kwanza. Ni chama kipi cha upinzania kimeweka kumbukumbu ya kufanya ziara kwa mara ya kwanza tangia mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995

Ina maana 'masaburi weye' mpaka leo hii hujui tofauti ya ikulu ya zanzibar na ikulu ya magogoni? pole sana, katiba inayohusu ni ya jamhuri ya muungano wa tanzania, sasa waende ikulu ya zanzibar wakamuone nani? na kwa lipi?
 
Kuna tatizo na siasa zetu. Tunatakiwa kujiangalia upya. Huu sasa ni kama mchezo wa kuigiza leo huyu kesho yula. Wao wanasema walishawasilisha mapendekezo ya katuiba before mswaaada mpaka wakapigwa virungu buguruni, sasa waone jamma wanakwenda nao hao. Kesho Mrema nae ataenda na yake. Nahisi hata huyu jamaa wa magogoni anaona hatuko serious thats why ameamua kusaini siku moja baada ya kukutana na wale jamaa wa gwanda. Hebu tujiulize tunapokutana nao huwa wanania ya dhati ama ni kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili kuwafurahisha wafadhili kuwa wanasettle mambo na wapinzani bajeti iweze kuongezewa fungu. Tafakarini ndugu zangu waenda magogoni!!
:embarassed2::embarassed2::shock::A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed:
 
hawa jamaa sijui kama leo wamekwenda kuswali swala ya ijumaa.

Viongozi wa CUF wameenda Ikulu kufanya nini cha mno zaidi ya kuuza sura na kutaka kupata air time kwenye media? Wao waliunga mkono hoja bungeni, pili walipokuwa bungeni CHADEMA walipotoka wao walibaki na kuongea upupu tu na kumjadili Tund Lissu, tatu hawana relevancy tena (watu hawawachukulii kama wapinzani).
 
CCM mabingwa wa propaganda?? aargh..

Chadema wamekutana nao - Jumapili-Wakristo

CUF wamekatuna nao - Ijumaa -Waislamu

You know what divide and rule..

tunasafari ndefu sana kuwatoa ccm ikulu
 
Wacha wanywe juice yao nao si walipa kodi na ikulu sio mali ya mkuu wa kaya na luhanjo ni ya wananchi wote. Ila nao wana ajenda gani tofauti na zile za bungeni!
 
Chadema walipoenda ikulu pamoja na mambo mengine walitaka kumshawishi JK asisani muswada, sasa JK ashasaini sasa hawa CUF wanaenda kufanya nini kama si kupiga picha na kunywa chai ya ikulu?
 
Ni ushaidi kuwa CHADEMA was and is always right. Hata CCM ukiwahoji mmoja mmoja kwa sharti la kutotaja jina au kutoa picha, watakukuambia mambo tofauti. The problem in our bunge sesssions is SIMBA VS YANGA. Goli safi wanasema ni offside.W

Then hii tabia ya Marais kuongea mambo serious na eti "Wazee wa DSM" inaniboa kweli. Why JK asikutane na jopo la wanaharakati, wataalamu na watu mbalimbali aeleze hayo na kujibu maswali yao, anaogopa nini?
 
Hawa angalau wanaonyesha wanaenda kuzungumza kitu cha maana sio magwanda attention seekers!!!! Tunaomba mtuonyeshe na ajenda zenu tuzisome pia.

Ningekushangaa usingesema hayo kwani hao wote pamoja na wewe ni wazee wa itikadi kali
 
Back
Top Bottom