Picha: Viongozi wa CUF watinga Ikulu leo!

There's something about ikulu watu wakienda wanakenua tu kama "mazuzu" Hizo si smile mkuu Lol!

Halafu tatizo wakitoka huko wanakuwa kama walisahau kilichowapeleka na inawachukuwa muda kukaa sawa na kusema walichoongea na mkulu!

Wakivusha mguu tu ndani ya ikulu wanakuwa kama "misukule" wanacheka cheka tu hovyo!

Sijui ni tactic ya JK kuwachekesha na kuwalamba mipicha?

Ama sijui huwa ana wa hypnotize?

Maana si ndiyo wao walikuwa wakidai ooh sijui anacheka cheka na kwamba hayuko serious?

Sasa hii yao mbona kali sana tu?

Teh teh teh...JF kuna machungu na raha zake!
You know what!!seems kweli kuna some kind of internal influence inayowafanya wakiwa ikulu hawa majamaa wacheke unconditionally.....unajua this can be natural.

....na inaonekana kuingilia hata fikra zao kimaamuzi au kimkakati mara wanapokuwa mbele ya rais wao tena ikulu......imagine this.....wewe umejararibu kupanda mlima kili na lengo lako ufike kileleni...........umejaribu kwa shida na taabu huku kila mara ukitaka kuishia njiani maana kileleni bado mbaaali alafu njiani msitu mkali, baridi kali, wanyama, mawe, uchovu balaa........umeendelea pamoja na vikwazo vyote huku umekunja uso kwa machovu alafu mara du!umejikuta umefika kileleni. ...hakika hata kama ulikuwa unalia,ukifika kileleni lazima ucheke,tena saana yaani....maana umeweza kufika(kwa mara ya kwanza maishani) killeleni......

Sasa hii parable inamaanisha.......hawa jamaa wanapokuwa pale ikulu.......naturally wanakuwa na some kind of hype.......yaani...some pseudo relief kwamba oh!tupo ikulu!.........na kwa hivyo twawaona wakicheka.....maana kwenye agenda za vyama vyao........wooote dream zao ni siku kumoja kuwepo ikulu for real.......yaani kushika dola........lol
 
Mtatilo nae ana "sigida " sikuhizi, vp jamani huyu mtu nae anaswali siku hizi? au kanuni yakuwa CUF ni lazima u-Silim!
 
CDM wakisema wanamuomba Dr Slaa atoe ushauri kuhusu muswada, CUF nao wataomba wamuone Slaa
 
Huyo mwenye tisheti na jinzi sijui ni nani tena huko, ndio wamerudisha POSA? mmh haya
 
Kuna hako kajamaa kafupi kamevaa suti ya bluu bahari naona kaenda kwa fundi aikate kidogo chini fundi akapitiliza, sasa kamening'inia tu
 
Watu wakishindwa kufikiri watajitukana hata wao wenyewe. Bila shaka walitamani kukalia masofa ya ikulu baada ya chadema kukalia. Duh
 
Wameenda kuonesha (hasa kwa Wananchi) kuwa hata wao ni wapinzani, ingawa wengi tunajua SIO WAPINZANI WA KWELI.
Sijui hata wanapeleka mapendekezo gani wakati walisema ndioooooooooooooooo kama wenzao CCM A, basi tutarajie kuona pia CCM A
wakiwasilisha nao mapendekezo yao.
 
Chadema imeonekana kuongoza Taifa maana kila inachoamua ndo kinatekelezwa.Sas na ccm wataomba kumuona Rais nape na Mukama nao wataomba
 
kuna jamaa kaninog'oneza hapa ati CUF kirefu chake kipya ni : ni Chama cha Usaliti na Fitina kwa watanzania. kwa kweli watanzania hawakosi ....
 
Asante chadema maana bila kulianzisha na sisi kaf tungeendalini kupigalini picha na Rais.Chek huyo mzee haamini kama nikweli au anaota
 
Uchaguzi nchi hauna maana yote usanii tu wanatuchukulia hela zetu CCM chagueni rais na wabunge katika vikao vya NEC na CC hela nyingine pelekeni kwenye huduma za jamii nchi hii haina upinzani.
 
Kuna hako kajamaa kafupi kamevaa suti ya bluu bahari naona kaenda kwa fundi aikate kidogo chini fundi akapitiliza, sasa kamening'inia tu

haa haaa haaaaa

weekend imeanza
 
ijumaa ijayo NCCR nao waende kuonja maji ya ikulu kisha wanaharakati nao waelekeee huko wakanywe juice ya ikulu halafu wananchi tuamue wenyewe hatutaki mtu wa kukaa bele yetu
 
Hawa kidogo wanaonesha wana nia ya dhati kuliko Magwanda walioingia Ikulu kwenda kupiga picha na kuchekacheka.

nia ipi tena wakati nia yao walishaonesha bungeni waziwazi, hao CUF ni kama mtoto anaedeka kwa mama yake baada ya kuona mwenzake kabebwa na yeye analilia abebwe kwa kusema "mama mbona unambeba 'kaka chadema' mimi hunibebi wakati huwa nakusaidiaga kufagia jikoni"
 
Hawa CUF kweli ichefu chefu. Hii yote ni kuhakikisha waliyofanya CHADEMA yakose maana. Sasa wao walikuwepo bungeni, wakaunga mkono mswada wa mume wao, ni nini tena wanataka kama sio mambo ya kitoto?
 
Mtatilo nae ana "sigida " sikuhizi, vp jamani huyu mtu nae anaswali siku hizi? au kanuni yakuwa CUF ni lazima u-Silim!

daah! hata mimi nimeiona hiyo sigida au jamaa wameshamslimisha nini? maana naskia anataka achukue uenyekiti, inawezekana hayo ndo masharti ya chama!
 
Viongozi wa CUF wakiwasili Ikulu leo

inwy03.jpg

x5qr00.jpg

a1o1ua.jpg

t0nckm.jpg

1446yqt.jpg

23k6ihx.jpg

35iyrr8.jpg

rwtn3q.jpg


UJUMBE watu saba wa Chama cha Wananchi CUF ukiongozwa na Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Machano Khamis Ali, leo unakutana na Rais Jakaya Kikwete, ili kujadili Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011.

Wengine wanaoshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF- Bara, Julius Mtatiro, Ismail Jussa (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Abdul Kambaya (Mjumbe Baraza Kuu la Uongozi Taifa), Habib Mnyaa (Kiongozi wa Wabunge wa CUF), Mkiwa Kimwanga (Mbunge Viti Maalum CUF), Twaha Taslima (Mwanasheria na Wakili wa CUF).

Taarifa ya CUF kwa vyombo vya habari jana ilisema kikao cha ujumbe wa CUF na Rais kitaanza saa 4:00 na kwamba ajenda zitatolewa baada ya kikao hicho. Juzi taarifa iliyokuwa imetolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari ilisema baada ya kupata ombi la CUF Rais alikubali kukutana nao.

Mwananchi.

Hao CUF walienda kupiga picha na JK tu hakuna lolote bana...
 
Back
Top Bottom