Rais Samia ampokea Klaus Werner lohannis, Rais wa Romania Ikulu - Dar es Salaam, leo Novemba 17, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpokea Klaus Werner lohannis, Rais wa Romania Ikulu - Dar es Salaam leo tarehe 17 Novemba, 2023


View: https://www.youtube.com/live/n0CG2IQgQtM?si=DEDi79Uv7U9lOxLL
f89c4492-02f9-43db-9609-4e33088e4cdc.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mgeni wake Rais wa Romania, Klaus Iohannis wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika mapokezi Rasmi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.

RAIS WA ROMANIA APOKELEWA IKULU YA DAR, AKAGUA GWARIDE KWENYE MVUA
Rais wa Romania, Klaus Werner Iohannis akishuka kwenye jukwaa kwa ajili ya kukagua kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo anaonekana akikataa kufunikwa na mwamvuli licha ya mvua kunyesha eneo hilo la Ikulu - Dar es Salaam, leo tarehe 17 Novemba, 2023

Amekaribishwa na kupokelewa na mwenyeki wake, Rais Samia Suluhu Hassan.
f2c77061-1c45-4837-a852-8c045e924636.jpeg

Rais wa Romania, Klaus Iohannis akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.
39b734d6-08de-481b-83c4-b654e6b09d20.jpeg

Rais wa Romania, Klaus Iohannis akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023 .
4131201d-b64f-4ef9-8107-c0180dce3349.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Romania, Klaus Iohannis mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023 .

355bc04e-3393-4d8e-8189-05e316ba382f.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Romania ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo, Klaus Iohannis Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.
29f52156-d58f-42db-8bb5-28fc816ea94f.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo iliyotiwa saini na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama na Waziri wa nchi wa masuala ya Dunia na Mikakati ya Kidiplomasia wa Romania, Traian- Laurentiu Hristea kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.
 
Hii nchi ina watu milioni 19 tu sisi tupo 61 lakini utashangaa sisi ndiyo tunaomba misaada kwao na wakati tuna madini kila kona, maziwa, bahari, mito, ardhi safi, mifugo, mbuga za wanyama, mmazao ya biashara, gas n.k lakini tumekosa uongozi bora. Shame on us
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpokea Mhe. Klaus Werner lohannis, Rais wa Romania Ikulu - Dar es Salaam leo tarehe 17 Novemba, 2023


RAIS WA ROMANIA APOKELEWA IKULU YA DAR, AKAGUA GWARIDE KWENYE MVUA
Rais wa Romania, Klaus Werner Iohannis akishuka kwenye jukwaa kwa ajili ya kukagua kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo anaonekana akikataa kufunikwa na mwamvuli licha ya mvua kunyesha eneo hilo la Ikulu - Dar es Salaam, leo tarehe 17 Novemba, 2023

Amekaribishwa na kupokelewa na mwenyeki wake, Rais Samia Suluhu Hassan

Mbona ka inchi masikini sana haka inakuwaje tunakuwa nako karibu jamani, yaani hapa sijapenda kabisa Mama kumkaribisha huyu kiongozi wa gypsies. Yaani hawa walivyo masikini ndiyo watataka watokee kwa rasilimali zetu, tena waweza kuta wakatumia magenge yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom