Picha: Viongozi wa CUF watinga Ikulu leo!

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Viongozi wa CUF wakiwasili Ikulu leo

inwy03.jpg

x5qr00.jpg

a1o1ua.jpg

t0nckm.jpg

1446yqt.jpg

23k6ihx.jpg

35iyrr8.jpg

rwtn3q.jpg


UJUMBE watu saba wa Chama cha Wananchi CUF ukiongozwa na Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Machano Khamis Ali, leo unakutana na Rais Jakaya Kikwete, ili kujadili Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011.

Wengine wanaoshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF- Bara, Julius Mtatiro, Ismail Jussa (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Abdul Kambaya (Mjumbe Baraza Kuu la Uongozi Taifa), Habib Mnyaa (Kiongozi wa Wabunge wa CUF), Mkiwa Kimwanga (Mbunge Viti Maalum CUF), Twaha Taslima (Mwanasheria na Wakili wa CUF).

Taarifa ya CUF kwa vyombo vya habari jana ilisema kikao cha ujumbe wa CUF na Rais kitaanza saa 4:00 na kwamba ajenda zitatolewa baada ya kikao hicho. Juzi taarifa iliyokuwa imetolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari ilisema baada ya kupata ombi la CUF Rais alikubali kukutana nao.

Mwananchi.
 
Hawa kidogo wanaonesha wana nia ya dhati kuliko Magwanda walioingia Ikulu kwenda kupiga picha na kuchekacheka.
 
Hawa watu wa ajabu sana,siwalishapitisha kile wanachoendea kwa Jk? Da kweli leo wanaenda kuimarisha mtoto aliepo tumboni ingawa karibu kujifungua kufike
 
Kama kawaida JK anawapa Juice ya machenza na kahawa ya Yemen, watatepeta kma wenzao Chadema JK bana toto ya mujini

na samaki wa kuchemsha..kumbuka ferry haiko mbali!......

hawa wapinzani wetu mpaka rrrraha!
 
Hawa kidogo wanaonesha wana nia ya dhati kuliko Magwanda walioingia Ikulu kwenda kupiga picha na kuchekacheka.

Mkuu Mwita25 wakati mwingine cjui unavutaga ile kitu ya Mpwapwa hata sielewi,kwani ww haujiulizi hawa waendao Ikulu si ndio hawa walopitisha ule Mswada kwa mbwembwe zote na wale CCM A?
 
Kama kawaida JK anawapa Juice ya machenza na kahawa ya Yemen, watatepeta kma wenzao Chadema JK bana toto ya mujini
CDM wametepeta?wewe kweli chizi,hujui CCM na JK sasa ndio hawalali maana wanajua mziki utakao fata kuucheza ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom