Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye fani ya kemia katika mahafali ya 39 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kufanya utafiti kuandika na kufanikiwa kuitetea tasnifu (thesis) inayohusu matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu. Tasnifu hiyo inahusu uwezo wa tabaka jembamba linalojipanga lenyewe la aside ya anakadi itokanayo na kioevu cha maganda ya kokwa za korosho kama njia ya mpako wa kuzuia kutu.
Mh. Magufuli alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Fulgence Kazaura akiwa mmoja wa wanafunzi 19 wa shahada hiyo. Mbali na hao katika mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo wanafunzi wengine 4,331 walitunukiwa vyeti, stashahada na shahada mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza akitambuliwa kama Dr. Magufuli alisema kuwa baada ya kufanya utafiti huo, maganda ya korosho badala ya kutupwa kama zamani kwa kuonekana kama takataka sasa yatatumika katika kuzuia kutu. Alisema kuwa kutu ni tatizo linalokumba dunia na kuongeza kuwa nchi ya Marekani huingia gharama za dola milioni 100 kwa ajili ya kuzuia kutu. Eeh kweli penye nia pana njia , hongera Dr.PJM.(habari/picha -Daily News)
Chanzo
MIRINDIMO: November 2009