ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 61,957
- 72,354
Chuo Kikuu Mzumbe kinatarajia Kumtunuku Rais Samia Shahada ya Udakatri wa Heshima katika Uongozi wa Chuo kama ishara ya kutambua jitihada zake katika kuboresha Elimu ya Juu Nchini hasa miundombinu,Utafiti na kuongeza idadi ya udahili.
Hiyo itakuwa ni Shahada ya 5 Kwa Rais Samia na Shahada ya 1 kutolewa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Ikumbukwe Rais Samia ni alumni wa Mzumbe Hongera Rais Samia, jitihada zako zitambuliwe Sasa Ukiwa hai na Kila mtu anaona.👇👇
Leo Jumapili, Novemba 24, 2024 ni mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkoa wa Morogoro.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atatunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Mwegoha amesema hiyo itakuwa shahada ya kwanza ya heshima kutolewa na chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.
Shahada hiyo ya udaktari wa heshima itakuwa ya tano Rais Samia kuoewa tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 akichukua kijiti cha mtangulizi wake, hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.
Shahada nyingine nne ametunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania), Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (India) na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Uongozi ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Morogoroyaliyofanyika katika eneo la Maekani, Kampasi Kuu Morogoro tarehe 24 Novemba, 2024. Shahada hiyo ni ya kwanza katika ngazi hiyo ya Uongozi kutolewa na Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake
Shahada nyingine za Udaktari wa Heshima soma viunganishi hapa chini
Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi ya Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), leo Desemba 28, 2023
Rais Samia Atunukiwa Udaktari wa Uchumi (Doctorate of Economics Degree) Uturuki
Rais Samia atunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, leo Aprili 18, 2024
Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa, Korea, Juni 3, 2024
My Take
Hata hili Chadema watapinga ila Sasa data za takwimu zinawakataa.
Mfano mzuri ni mradi huu wa kupanua Elimu ya Juu Nchini ambapo taasisi 23 za Elimu ya Juu zinaendelea na kazi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Kujifunzia.
Aidha Mikoa 15 ambayo hakikuwahi kuwa na Vyuo Vikuu au Matawi ujenzi unaendelea.Hii ni kazi ya Kutukuka ya Rais Samia. Haya yote yanatokea Chini ya Samia 👇👇
View: https://www.instagram.com/reel/DCr7oyLOtS4/?igsh=MWF5NWIzNHVhcm1mOQ==