Picha: Siku ambayo Rais Magufuli alipata PHD yake akiwa waziri

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Magufuli.JPG
Mama Magufuli.JPG
Magufuli.JPG
Mama Magufuli.JPG
Mh. John Pombe Magufuli akitunukiwa shahada yake ya uzamivu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Balozi Fulgence Kazaura baada ya kukamilisha nondo zake katika fani ya sayansi ya kemia . Du hapo nakubali.

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye fani ya kemia katika mahafali ya 39 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kufanya utafiti kuandika na kufanikiwa kuitetea tasnifu (thesis) inayohusu matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu. Tasnifu hiyo inahusu uwezo wa tabaka jembamba linalojipanga lenyewe la aside ya anakadi itokanayo na kioevu cha maganda ya kokwa za korosho kama njia ya mpako wa kuzuia kutu.

Mh. Magufuli alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Fulgence Kazaura akiwa mmoja wa wanafunzi 19 wa shahada hiyo. Mbali na hao katika mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo wanafunzi wengine 4,331 walitunukiwa vyeti, stashahada na shahada mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza akitambuliwa kama Dr. Magufuli alisema kuwa baada ya kufanya utafiti huo, maganda ya korosho badala ya kutupwa kama zamani kwa kuonekana kama takataka sasa yatatumika katika kuzuia kutu. Alisema kuwa kutu ni tatizo linalokumba dunia na kuongeza kuwa nchi ya Marekani huingia gharama za dola milioni 100 kwa ajili ya kuzuia kutu. Eeh kweli penye nia pana njia , hongera Dr.PJM.(habari/picha -Daily News)

Chanzo
MIRINDIMO: November 2009
 
Mtaalamu wa kudhibiti Kutu!

Nguli wa kudhibiti Kutu Duniani! Hahahahahahahah!

Kutu za Ufisadi lazima zing'olewe

Tumshauri aanzishe Kiwanda cha Kutengeneza Vidhibiti Kutu tuajiri Wanyonge na Walalahoi!

Mhhh! First Lady wetu Maashallah
 
View attachment 454464 View attachment 454465 View attachment 454464 View attachment 454465 Mh. John Pombe Magufuli akitunukiwa shahada yake ya uzamivu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Balozi Fulgence Kazaura baada ya kukamilisha nondo zake katika fani ya sayansi ya kemia . Du hapo nakubali.

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye fani ya kemia katika mahafali ya 39 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kufanya utafiti kuandika na kufanikiwa kuitetea tasnifu (thesis) inayohusu matumizi ya maganda ya korosho katika kuzuia kutu. Tasnifu hiyo inahusu uwezo wa tabaka jembamba linalojipanga lenyewe la aside ya anakadi itokanayo na kioevu cha maganda ya kokwa za korosho kama njia ya mpako wa kuzuia kutu.

Mh. Magufuli alitunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Fulgence Kazaura akiwa mmoja wa wanafunzi 19 wa shahada hiyo. Mbali na hao katika mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo wanafunzi wengine 4,331 walitunukiwa vyeti, stashahada na shahada mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza akitambuliwa kama Dr. Magufuli alisema kuwa baada ya kufanya utafiti huo, maganda ya korosho badala ya kutupwa kama zamani kwa kuonekana kama takataka sasa yatatumika katika kuzuia kutu. Alisema kuwa kutu ni tatizo linalokumba dunia na kuongeza kuwa nchi ya Marekani huingia gharama za dola milioni 100 kwa ajili ya kuzuia kutu. Eeh kweli penye nia pana njia , hongera Dr.PJM.(habari/picha -Daily News)

Chanzo
MIRINDIMO: November 2009
Tunataka na vyeti vya Mbowe hapa.
 
Back
Top Bottom