Mtoa mada inaonyesha haufahamu haya mambo kwa ustadi wake, yaani wewe bado una mtazamo wa software au app development ki uanafunzi sio ki professional.
Hili ni tatizo la watanzanaia wengi kwenye industry ya IT, ukishangaa hili la JF, na ukajenga hoja zako za kwa nini hawakuandika code from scratch, nitakuuliza je wewe hizo software unazotumia uliziandika from scatch?
Kuna mwalimu mmoja nae niliwahi kutana nae eti aliniwakia kisa alikuta nimeandika code za html kwa kutumia div tags, akokomaa umetumia Dream Weaver (kama unaijua lakini, maana kipindi cha nyuma ndio ilikua ni kama IDE ya maajabu kwa web devs) akiamini haiwezekani kuandika code kama hizo kwa notepad ambayo ni plaintext, yaani ni kukariri tu na kutojiongeza kuelewa na kufahamu mambo yalivyo.
Makampuni yote unayoyajua most of there products wananunua, hiyo google tu ni mfano mzuri, tena ukiwa mtaalamu wa app development ndio huwezi kuwa na upeo finyu wa kuanza kuandika from scratch, hakuna kitu kama hicho.
Niseme tu kajifunze zaidi... Maana hata hizo tools unazotumia kuandika codes pia ziliandikwa na watu ila wewe unatumia kufanyia majaribio yako pia na zinakurahisishia mpaka unaona wenzako (JF) ni wazemembe.