PICHA: Mererani mwanajeshi ajitoa mhanga

PICHA: Mererani mwanajeshi ajitoa mhanga

Magwanda ya kijeshi yanauzwa kila uchochoro wa mitumba! sasa gwanda hilo halinishangazi maana tangu turuhusu mitumba sio shida tena kujipatia gwanda la jeshi!
Jamii bwana kila lenye ukweli kisiasa lazima lipate propaganda, kiukweli haya ni majibu ya maisha bora kwa kila mtanzania.Kwamba hakuna maisha bora kwa kila mtanzania, na serikali ya ccm haina nafasi ya kuisikiliza jamii, bali ghiriba , na uongo wa takwimu ambazo haziendani na maisha halisi ya mtanzania;Kwa miaka mingi chumvi ilikuwa inanunuliwa t.shs 50/= leo mia mbili, piga hesa ya ongezeko la kia asilimia, na je na maisha nayo yemekuwa safi kiasi hicho?acha ubabe wa kupindisha ukweli si gwanda la kununua bali ni maisha magumu, JWTZ ana rushwa gani zaidi ya mshahara?na je huo mshahara unamtosha?akalalamike wapi?kumwona hovyo ndo kuondoa msongo wa maisha
 
aaaahaaah na bado magamba mtakomaaa mwaka mnataman uish leo welcome 2013!
 
Na kama ikatambulika kama si askari shahidi namba moja atakuwa lema na wenzake. Pia kuvaa sale za jeshi iwe la tz au nje ya nchi pia ni kosa. Na kwa akili ya kawaida hakuna askari mwenye akili kama hizo akatokeza mbele hivyo na magwanda ya jeshi ...

Mkuu KIBE,
Hivi ujiulizi kama wameshindwa kumkamata mtekaji wa Ulimboka wataweza kukamata huyo Askari? Na kama ikitambulika kama si askari (kama unavyosema) ishu ya lema kuwa shahidi inakuja vipi? Kwani huyo ni mwanae anaishi nae kwake? Au hujui kwamba tunapomaliza kufanya mkutano wa hadhara wahutubiaji huwa wanapiga picha na Wananchi mbali mbali uwe unawajua au huwajui?

TUMBIRI (Upanga, Dar es Salaam - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Last edited by a moderator:
Msimshabikie mwenzenu akifanyiwa court martial na kuondolewa jeshini muwe tayari kumpa ajira! Wanajeshi wakitaka siasa watoke jeshini kwanza ndio kanuni ilivyo.

kwani mtumishi wa serikali haruhusiwi kupiga picha na mwanasiasa au haruhusiwi kuhudhuria mikutano ya siasa mbana ccm inawalazimisha kuhudhuria..
 
kwanza nasikitika kwa tukio hili, mimi nilikuwa kwenye huu mkutano jana huyu mwanajeshi huwa anafundisha mgambo mjini mererani, jana wakati chadema wakifanya mkutano wa hadhara mwanajeshi huyo aliwaamuru mgambo wote waende kwenye mkutano kuwasikiliza wabunge wa chadema, kabla mwanajeshi huyu haja fikia uwamuzi huo, kuna haice moja ilikuja na makamanda kadhaa wa chadema, akiwepo mpambe mmoja wa millya, oleleshwa alikwenda kuongea na huyu mwanajeshi huyo na ndo migambo wakapewa amri ya kwenda kwenye mkutano, bado niko hapa mererani nafanya uchunguzi wa kina na nimesha gundua kuwa, lema, nassari, heche wakishirikiana na millya wanatengeneza jeshi na watatumia msitu wa komolo wilayani simanjiro, mtu anayeratibu mafunzo ya wa wanajeshi hao wanafundishwa kwa mwamvuli wa mgambo ni mzee mmoja anaitwa peter peshut akishirikiana na oleleshwa, kwa ufadhili wa kamanda ndesamburo na mbowe, naendelea na ufafiti na kuna taarifa kuwa gideon sanago naye yuko hapa mererani akiendelea kuwashawishi apolo wajiunge na jeshi la kina lema.

inawezekana nikweli mana lema si alishasema anaanzisha 23tz
 
Jamani kwani kupiga picha na mwanasiasa ni kujihusisha na siasa? Watanzania acheni woga uliopitliza

hahahah, mkuu sio woga ndio ilivyo... political neutrality in the military offices, lakini hili anweza kushinda kama ana kadi na kuna ushahidi kuwa alijishughulisha na shughluli za siasa moto utamwakia!!
 
Hairuhusiwi kujihusisha na siasa maeneo ya kazi, wakati wa kazi na ukiwa na sare za kazi.
Jamaa amekosea, na ni hatari kwa kibarua chake. kweli kaamua kujitoa muhanga.
 
hii ishu musiichangie kishabiki, naona watu wanachangia kishabiki zaidi..,

means justfy the end?? Imagine chadema imeshika madaraka 2015,, then kwny mkutano wa ccm anaonekana mwanajeshi na combat, ni kosa au si kosa?? Tusiongelee sjui kuchoka maisha au kukerwa na chama tawala,, swali la kujiuliza ni kosa au si kosa,,

JESHI HALINA DINI WALA CHAMA na hii miongozi ipo kwa nia nzuri sana pamoja na kua na mapungufu madogo madogo ila mwisho wa siku ni bora kuwa na taratibu za namna hii!!
 
kisheria mtu wa chombo cha ulinzi na usalama hapaswi KUJIHUSISHA NA MASUALA YA VYMA,HAPASWI KUSHABIKIA CHAMA AU KUWA MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE

sasa kama ndivyo mbona hao wasisem ndo wakuu wa wilaya, mikoa, na tibaigwana mwenyewe aligombea ubunge? Au kwa vile katokelezea upande wa chadema? Sooner very soon we are going to see great thngs!
 
Magwanda ya kijeshi yanauzwa kila uchochoro wa mitumba! sasa gwanda hilo halinishangazi maana tangu turuhusu mitumba sio shida tena kujipatia gwanda la jeshi!

Hilo nalo neno , Dada Zubeda , inawezekana kabisa huyu sio mjeshi wa ukweli bali kavaa gwanda hizo za mitumba kama kujifurahisha tu, mbona huwa tunasikia kwamba majambazi yamevamia sehemu fulani ya kiwa ktk sare za jeshi(magwanda), kwani siku hizi ziko nyingi tu kwenye mitumba, kwani kwa kanununi za majeshi yote ya usalama na ulinzi hawaruhusiwa kujihusisha na ushabiki wa chama chochote au kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ukitaka siasa vua gwanda ,acha kazi tumbukia kwenye siasa . Bila shaka ktk hiyo picha kuna hided agenda ambayo inataka kuonyeshwa kwamba hata wanajeshi wanakiunga mkono CDM. Hata mimi nakubali kuwa kuna a askari wa jeshi,polisi na magereza ambo ni wapenzi wakubwa wa CDm(ndabni ya nafasi zao, na sio kujionyesha hadharani) lkn hawawezi fanya kama huyo askari feki.
 
kwanza nasikitika kwa tukio hili, mimi nilikuwa kwenye huu mkutano jana huyu mwanajeshi huwa anafundisha mgambo mjini mererani, jana wakati chadema wakifanya mkutano wa hadhara mwanajeshi huyo aliwaamuru mgambo wote waende kwenye mkutano kuwasikiliza wabunge wa chadema, kabla mwanajeshi huyu haja fikia uwamuzi huo, kuna haice moja ilikuja na makamanda kadhaa wa Chadema, akiwepo mpambe mmoja wa Millya, Oleleshwa alikwenda kuongea na huyu mwanajeshi huyo na ndo migambo wakapewa amri ya kwenda kwenye mkutano, bado niko hapa Mererani nafanya uchunguzi wa kina na nimesha gundua kuwa, Lema, Nassari, Heche wakishirikiana na Millya wanatengeneza Jeshi na watatumia msitu wa Komolo wilayani simanjiro, mtu anayeratibu mafunzo ya wa wanajeshi hao wanafundishwa kwa mwamvuli wa mgambo ni mzee mmoja anaitwa Peter Peshut akishirikiana na Oleleshwa, kwa ufadhili wa kamanda Ndesamburo na Mbowe, naendelea na ufafiti na kuna taarifa kuwa gideon Sanago naye yuko hapa Mererani akiendelea kuwashawishi Apolo wajiunge na jeshi la kina Lema.
Ukirusha jiwe kwenye giza alafu ukaskia aiii! ujue limempiga mlengwa,
Olesendeka ameanza kuumizwa na moto wa M4C.
Nimefurahi sana umedhibitisha kuwa huyu ni mwanajeshi halali wa jeshi letu na sio raiya aliyevalia nguo za jeshi kama magamba wengi wanavyodai.
Big up sana Lema, Milya pamoja na Nasary.

Nakala kwa KIBE
 
Last edited by a moderator:
Hao ndiyo majambazi yanayochafua jeshi letu la wananchi...anajiandaa kuingia mstuni kama Lema alivyosema.
 
Nadhani kakosea, askari wetu wote hawana chama, wao ni AGIP members i.e. Any Govt In Position
 
Kosa lake litakuwa lipi?
Kosa lake ni kushabikia chama cha siasa. Maana mwanajeshi hapaswi kushabikia chama chochote. Kwa kujitokeza kwake kwenye mkutano wa CHADEMA na kuonyesha alama ya V, kuna influence ya moja kwa moja kwa raia, na pia kunamuondolea yeye sifa ya kuweza kutenda haki iwapo yatatokea machafuko au mgogoro kati ya CHADEMA na CCM au chama kingine chochote.
 
kisheria baada ya kuanzishwa mfumo Wa vyama vingi wanajeshi hawaruhusiwi kujiunga Na chama chochote cha siasa.

Taarifa nikizonazo wanajeshi wengi wana kadi za ccm kwa sababu kuna muda klikuwa lazima kuwa Na kadi ya ccm Au umoja Wa vijana ili kupata ajira jeshini. Sijui Kama baada ya kuwa Na vyama vingi walinuang'anywa hizo kadi Au waliendelea kuzilipia Na kuwa wanachama kisiri siri Au walibaki Na kadi za ccm Kama souvenir.

Hata hivyo wanajeshi wanaruhisiwa kupiga kura hivyo lazima wawe Na mapenzi Na vyama
 
Back
Top Bottom