PICHA: Mererani mwanajeshi ajitoa mhanga

PICHA: Mererani mwanajeshi ajitoa mhanga

Wako wengi hawa jeshini,lakini huyu kaamua kuthubutu.ukombozi wa kweli unakuja Tanzania,

Hongera kamanda wa ukweli
Ukombozi wa kweli hauwezi kuja kwa watu kuasi viapo vyao na kukiuka maadili ya kazi na sheria za kazi,ni hatari sana kushabikia hii hali,coz anaeshughulika na mapungufu yoyote ya serikali ni bunge na sio Jeshi,msitupeleke huko.Lema to me wewe ni hatari sana na angalia sana,sio kila mtu umtumie kufanikisha malengo yako kisiasa,makundi mengine yakitumika ni hatari sana.
 
kisheria mtu wa chombo cha ulinzi na usalama hapaswi KUJIHUSISHA NA MASUALA YA VYMA,HAPASWI KUSHABIKIA CHAMA AU KUWA MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE

Na je ni kosa kupiga picha na mwanasiasa yeyote?hata kama ni jamaa au ndugu yako?
 
Sheria ya majeshi dunia nzima hawafungamani na siasa ..... Na kama ikatambulika kama si askari shahidi namba moja atakuwa lema na wenzake .... Pia kuvaa sale za jeshi iwe la tz au nje ya nchi pia ni kosa... Na kwa akili ya kawaida hakuna askari mwenye akili kama hizo akatokeza mbele hivyo na magwanda ya jeshi ...
 
Hakuna lolote huyo ni mlinzi wa migodi ya mererani mbona haja taja jina lake cdm kwa kutaka sifa duh....noma kweli
 
muda sii mrefu mkuu wa majeshi,igp,mkuu wa magereza,dir tiss watanyoosha Viva!
 
jeshi lina sheria, kanuni na taratibu zake! lets wait...........
Hiyo ilikuwa zamani sana, siku hizi jeshini ni Gongo, Bangi, Ngono na Hongo.
Jeshi litakuwa na nidhamu siku vita ikitokea tu.
 
kosa lake litakuwa ni kujihusisha na mambo ya siasa wazi wazi! hili haliruhusiwi hata kidogo! ingawa ccm ni ruksa kabsa! lol

Jamani kwani kupiga picha na mwanasiasa ni kujihusisha na siasa? Watanzania acheni woga uliopitliza
 
ukombozi wa kweli hauwezi kuja kwa watu kuasi viapo vyao na kukiuka maadili ya kazi na sheria za kazi,ni hatari sana kushabikia hii hali,coz anaeshughulika na mapungufu yoyote ya serikali ni bunge na sio jeshi,msitupeleke huko.lema to me wewe ni hatari sana na angalia sana,sio kila mtu umtumie kufanikisha malengo yako kisiasa,makundi mengine yakitumika ni hatari sana.
binafsi katika hili siungi mkono ...hizi sio siasa na hukana na hakuna duniani kuwahi kutokea kituko cha wanasiasa kutafuta watu kuwavalisha kombati za jeshi kwa lengo la kufanikisha mambo yao ya kiasia..ndo naona hapa tz... Na ukweli uko wazi hasa hawa viongozi hawa vijana wa cdm ukweli ni hatari wanavuruga nchi wazi wazi... Tushabikie lakini tuangalie na ukweli wa swala hili ni hatari sana . Mbowe,slaa ,mzee mtei vyema mkaangalia upya njia ya kupata mafanikio katika siasa zenu kama ni sahihi au la...
 
Kosa Lake Kuchanganya Siasa na Kazi...Si kuna kitu kinaitwa 'POLITICAL NEUTRALITY MKUU"?

Vipongozi wa kijeshi wanapiga picha sana na viongozi wa ccm na wakiwa kwenye uniform
je wanafanya siasa hapo?!!!!
 
Ukombozi wa kweli hauwezi kuja kwa watu kuasi viapo vyao na kukiuka maadili ya kazi na sheria za kazi,ni hatari sana kushabikia hii hali,coz anaeshughulika na mapungufu yoyote ya serikali ni bunge na sio Jeshi,msitupeleke huko.Lema to me wewe ni hatari sana na angalia sana,sio kila mtu umtumie kufanikisha malengo yako kisiasa,makundi mengine yakitumika ni hatari sana.

Wakitumia ccm siyo hatari,ila Lema hatari.! Uko vizuri kweli?
AkIli.
 
Mtajipambambanua kwa njia nyingi lakini sawa na mwanaume asiye na kizazi ... Bado mtanunua hadi nguo za mgambo wa jiji,za manesi na madr alafu mpige nao picha.... Hata kwa macho tu mtoto mdogo anajua huyo kibaka tu kaokotwa mtaani kavalishwa nguo .


Ray C kambaka mkuu, hadi nchi inaenda kombo. Ndio maana wanajeshi wanajitokeza hadharani, na huu ni mwanzo tu.
 
Mtajipambambanua kwa njia nyingi lakini sawa na mwanaume asiye na kizazi ... Bado mtanunua hadi nguo za mgambo wa jiji,za manesi na madr alafu mpige nao picha.... Hata kwa macho tu mtoto mdogo anajua huyo kibaka tu kaokotwa mtaani kavalishwa nguo .

kwa hiyo wwe unafikiri kuwa wanajeshi wanafurahia hali ya nchi na maisha magumu wanayo face, wewe jidanganye tu usifikiri kwa kuwa wewe una uhakika wa kula na kwenda chooni na kusomesha kwa kuwakumbatia magamba ukazani ndio wote wapo kama wewe, me mwenyewe mwanajeshi na najua hali ilivyo ndani ya jeshi, poleni sana magamba kwa kujiweka pabaya na kuchukiwa na wananchi, ukombozi wakaribia....
 
KATIKA GAZETI LA MWANANCHI LA LEO TAREHE 24 DEC, KUNA MTU ANAYEONEKENA KUPIGA PICHA NA KUHUDHURIA MKUTANO WA CHADEMA .. INADAIWA KUWA NI ASKARI WA JWTZ TOKA KAMBI YA MONDULI ... KUTOKANA NA MIONGOZO YA JESHI NI VYEMA JESHI LIKATOA KAULI KAMA HUYO MTU NI ASKARI KWELI AU LA.. AU KAVALIWASHWA MAGWANDA NA UKIANGALIA PIA MAGWANDA YAKE NI TOFAUTI NA YA JWTZ, NI YA JESHI LA MAREKEANI.

lema_mjeshi.jpg
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara jana.
Hoya unauliza majibu ya nanii ino ya wakati umeshika mkia wake!! Mwanajeshi kesha tamka wazi kuwa yuko tyari kufukuzwa hana cha kupoteza!!!Mtu akishakuwa kwenye pointi hiyo unategemea.

Halafu kama uwezi kusoma maandishi kibe hata picha uoni,yani unayaona hayo magwanda ni ya jeshi la kimarekani!!Hivi kwanini uwa mnawapotosha watu wa Serikali ya JMT kwa kuwavisha na story za kipuuzi eti "AU KAVALIWASHWA MAGWANDA NA UKIANGALIA PIA MAGWANDA YAKE NI TOFAUTI NA YA JWTZ, NI YA JESHI LA MAREKEANI.".Kwanini usione katika picha na kujenga dot kuwa ni mmoja wa wana usalama wetu lakini aliyefika mwisho katika maamuzi yake ukizingatia kuwa ni kijana kwa sasa hana cha kupoteza.

Wapo walio acha Jeshi wakaenda kuwa wasanii wa muziki kama wakina ......wa Wanaume family,ni uamuzi wa ujana kwa mujibu wa jinsi anavyo ona yeye.Ila kwa kuwa huyu ni wa kisiasa basi kidogo yeye unamuangalia kwa jicho,kuwa nini kimemfikisha kwenye uamuzi huo je ni mwajili wake Serikali ya JMT imeshindwa kumtimizia ujira wake na doto zake azioni kuwa zitatimia hivyo ameamua kujiunga na CDM ili kutafuta ndoto yake hiyo,ambayo ni haki yake ya msingi pia,ila kwa kuwa akichagua kukaa huko basi inabidi kuvua gwanda hilo la JMT,na kuonyesha kuwa yuko tayari kwa hilo kasema yeye hana shaka yuko tayari kwa hilo,muda wowote mwajili wake akisema imetosha aludishe combat hiyo.

Kijana kasema kazi iko kwa JWTZ kujipima je ni wangapi watamfuata kijana mwenzao huko kama anayoyatafuta anayaona ni genuine kwanini na wenzie wasiyaone kuwa ni genuine vile vile.
 
Huyu bila ya kukosea ni kati ya wale waliojiita kikosi cha 2258 na hakika nami nasema wapo wengi sana na ngoja wajitokeze na hapo mbivu na mbichi itakapojulikana! Na hapo sasa ndiyo kazi inaanza!


Wapo wengine wengi, hawajaja hadharani!:target:
 
Ukombozi wa kweli hauwezi kuja kwa watu kuasi viapo vyao na kukiuka maadili ya kazi na sheria za kazi,ni hatari sana kushabikia hii hali,coz anaeshughulika na mapungufu yoyote ya serikali ni bunge na sio Jeshi,msitupeleke huko.Lema to me wewe ni hatari sana na angalia sana,sio kila mtu umtumie kufanikisha malengo yako kisiasa,makundi mengine yakitumika ni hatari sana.

daaa mkuki kwa nguluwe jamani, ila ndoo hvo sio huyo mwanajeshi kapenda ila ni mapenzi ya Mungu aliejuu
 
Back
Top Bottom