PICHA: Kwanini Tundu Lissu amelia baada ya kushinda kesi??

Heeeh! Yaani wewe unalijua koromeo la huyo wakili ama umetambua kola ya shati lake? Mabigi!
Wanajamvi huyo jamaa hapo nyuma ya lisu mwenye kola nyeupe ni kaka yake wa kuzaliwa lisu anaitwa alute mughwai ndiye aliyekua wakili upande wa magamba kwenye kesi ya lema arusha mjini....
 
mara nyingi strong people hide their emotions during the battle,but that does not mean they are not emotional! he is a human being just like you and I! let him be! Hongera Tundu,Alicia (good to see you by your man's side), and your twins! Mungu awatangulie daima.
 
Wakuu ni kweli Tundu Lissi atakuwa kilio chake kililiza wengi. Hata nilipokuwa naangalia ITV niliona camera man akipisha camera pembeni baada ya kumuonyesha kidogo akijifufa machozi.

Kwa tasfiri ya haraka ni uchungu aliokuwa nao baada ya yeye kujua hana kesi lakini alitaka kupotezewa muda tu. Inasikitisha sana. Katika mazingira haya kutoa chozi kwa uchungu inaweza kutokea.
 
HONGERA IDARA YA MAHAKAMA KUJIREJESHEA JAPO KA-THELUTHI YA HESHIMA KWA UMMA WA TANZANIA KUPITIA KWA JAJI MUSA MZUNA KULE SINGIDA:

Chozi la Mhe Tundu Lissu pale Mahakamani Singida hapo majuzi ni ushahidi tosha kwamba kwa uhakika kuna kitu kizito ajabu kimetokea katika taifa hili katika medani za sheria kuhusiana na UTAMADUNI ULIOZOELEKA KATIKA UTARATIBU MZIMA WA UTOAJI HAKI MAHAKAMANI.

Naam, si siri tena kwamba Jaji Musa Mzuna si tu kwamba atakua amejizolea heshima kwetu sisi akina kabwela ambao ni miaka mingi HATUFAHAMU KITU HAKI BILA FEDHA AU UHUSIANO NA WATAWALA bali zaidi ni kwamba huyu ndugu kafanikiwa, hata bila ya yeye kutambua, kuandika upya historia ndani ya nchi yetu juu ya utoaji haki kwa HAKI bila kutazama USAHIHI WA MTU MSIMAMO WAKE DHIDI YA WATAWALA kinyume kabisa na matarajio kwamba miaka yote hukumu huwafuata watawala wanavyotaka au dau kubwa la wenye fedha watakavyowiwa kumkirimu hakimu au Jaji husika. Ewe Jaji Musa Mzuna, hakika hata mimi sijaamini hiki kilichotokea!!!

Hakika nchi hii laiti tungekua na wanasheria mahiri na wenye FIKRA HURU, walau 10 tu, ambao ni fanania yake huyu Jaji Musa Mzuna wa Singida na wengine kama yule Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, ki-ukweli Tanzania hii hata sisi MASIKINI japo kidogo tu tungebahatika kuelewa NINI MAANA YA HAKI inayoelekezwa na Katiba yetu kuwa itolewe Mahakamani.

Kwa mtaji wa kile kilichotokea Singida na kuiletea Heshima Kuu Idara ya Mahakama machoni mwetu Umma wa Tanzania, kinyume kabisa na hukumu ya Arusha iliocha uchachu hata katika midomo yaa wataalaam wenyewe wa sheria ndani ya nchi hii, napenda nitoe rai yangu kwenu wakubwa zetu kwamba ENYI WAJUMBE MLIOTUKUKA 'KAMATI KAMATI YA KATIBA', KATIBA MPYA IJAYO ITAFUTE KUREJESHA (1) HAKI, HESHMA NA UTU WA MTANZANIA WA KAWAIDA, (2) ULINZI IMARA WA RASILMALI ZA TAIFA, NA (3) KUWEKA NJIA KIBAO ZA UWAJIBIKAJI KATIKA KILA NGAZI YA UTAWALA .

Hakika kwa walalahoi tuliowengi, wala si jambo la huzuni tena kwetu sisi kutokufahamu nini maana halisi ya HAKI KWA WOTE MAHAKAMANI; ukweli ni kwamba wengi tumefika mahali tunajionea tu jambo la kawaida kwa bidhaa hii ya 'HAKI MAHAKAMANI' kuwani miliki yao tu (1) WaTanzania wachache wenye VIJISENTI pamoja na (2) tabaka dogo la watawala, ndugu na marafiki zao.

Kwangu mie, ushindi wa Mhe Tundu Lissu kule Singida ni sawa tu na kusema ni USHINDI KWA IDARA YA MAHAKAMA kujichagulia, kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi saana, KUJIRUDISHIA JAAPO KA-CHEMBE CHA HESHIMA tuliobaki nayo akina kabwela wa nchi hii.

Naam, ni matumaaini yangu kwamba safari hii hawajafanya kazi zao kwa maelekezo ya simu kutoka Magogoni ya kujitafutia umwamba na kukomoana na mwisho wa siku kujikuta tuliokomolewa zaidi ni wapiga kura na wala si Mbunge mlengwa wa hila zote hizo.

Kwa kuhitimisha tu, kutokana na somo tunayoipata kutoka katika Mahakama zetu za Arusha, Singida na ukweli juu ya jinsi gani 'HAKI MAHAKAMANI' ilivyogeuka kuwa ni msamiati mgumu ajabu kwa WaTanzania masikini ambao ni zaidi ya asilimia 80% ya watu wote hapa nchini, ni wazi kwamba huyu Jaji Musa Mzuna kaatushangaza mno kwa ujasiri wake wa aina yake, baada ya miaka mingi sisi kutofahamu kitu haki nje ya vile waonavyo waatawala, kwa kutoa hukumu unaoegemea weledi wake tu na wala si vinginevyo!!

Kutokna na mshangao huo aliotupiga nayo huyu Mtanzania mwenzetu, nje kabisa ya mazoea tulivyokua tukiyasubiria, napenda nichukue fursa hii nikatume SALAMU ZENYE UPEKEE kwa magwiji wa sheria mnaoheshimika sana nchini na tena kubahatika kuingia katika Tume ya Katiba ya nchi yetu (Mzee Jaji Sinde Warioba, Mzee Jaji Augustino Ramadhani, Prof Mwesiga Baregu, Dr Sengondo Mvungi,na Mhe Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar) kwamba fanyeni yote juu ya yote kuunda katiba mpya ya nchi yetu kwa KUTUFANYA SISI WANANCHI WA KAWAIDA MITAANI NDIO TUWE KWELI ndio wenye nchi Kiutawala na maamuzi yote muhimu na wala si tu wana wa nchi tunaosukumwa kiholelaholela na watawala wachache na wenye hela.

Ndio, nasema mnalo jukumu lisilokwepeka Mzee Warioba wa kutufanya katika hiyo KATIBA MPYA, sisi tujihisi, kuonekana na kusomeka 'WAFALME NA WENYE USEMI WA MWISHO JUU YA MAMBO KIBAO yenye mustakabali mzima wa nchi yetu BILA KUWEKA REHANI MATUMAINI YETU YA BAADAYE KAMA NCHI mikononi mwao watawala wachache' kwa kutegemea eti siku gani watakua wameamka vipi au wake zao watakua wamefurahi au wamenuna.

Ndio, kwa hao vingunge wa sheria tunaowaheshimu sana nchini
(bila kusahau Prof Shivji, Jaji Bomani, Tundu Lissu na Prof Peter Maina), nasema KATIBA MPYA haitokua na maana yoyote kwangu mpaka pale ambapo FARAJA YANGU ITAKAMILIKA TU PALE AMBAPO LENGO KUU YA KUWEKA CHECKS AND BALANCES KIBAO YENYE LENGO LA KUFANYA bidhaa hii adimu ya 'HAKI MAHAKAMANI' kuwa ni bidhaa inayoweza ikapatikana hata kwa Mzee Matonya tu Barabarani dhidi ya Mzee Makamba katika ofisi ya Ukuu wa Mkoa - Bila kuingiliwa hata kidogo na 'Tawi la Pili la Kutoa HAKI MAHAKAMANI kupitia simu na vi-memo kutoka Magogoni.

Kwa lugha rahisi tu, ukitaka kuelewa ninachosema hapa ni kwamba jiulize kama haitokua
KICHEKESHO CHA KARNE kusikia eti Mzee Matonya kampeleka mahakamani yule Mzee Makamba kwa madai ya kuingilia uhuru wake wa kikatiba kutembelea popote, kukaa popote na kufanya shughuli zake popote BILA KUBUGHUDHIWA na mtu wala chombo chochote ILMRADI HAVUNJI SHERIA?

Kesi kama hii, kwa misingi ya Katiba ya sasa na mfumo uliopo, wala sio siri kwamba WaTanzania tunaweza hata tukakuambia kwamba hukumu itatoka vipi hata kabla kesi haijaanza. Ni kero, unafiki, na uzabizabina (Rweyemamu et al, 2011 - Kurugenzi za Mawasiliano Magogoni) endapo safari hii mtaendelea tena kuifanya Sheria na Katiba zote ziwe ni vyombo vinavyompendelea MHESHIMIWA MTAWALA pamoja na yule mwingine mwenye 'enzi' yote MHESHIMIWA MWENYE PESA.

Napenda nikuhakikishieni kwamba endapo kutazaliwa tena KATIBA isiompa UKUU MWANANCHI WA KAWAIDA ambaye ndiye uhalali wote wa kutawala inakamiswa kutoka kwetu, basi ninaweza kuwahakikishieni kwamba mnaweza kunihesabu mapema kuwa mstari wa mbele sana tu katika kutumia ushawishi wangu wote (UWEZO TUNAO) kuhakikisha kwamba marudio ya UDHALIMU NDANI YA KATIBA tunauangusha kwenye kura ya maoni bila ajizi.

Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia bila kutoa vielelezo dhahiri vunavyoonyesha tukio husika.

Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.

Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.

Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.


Source:Mwananchi Jumamosi

LISSU1.jpg

Mbunge wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge.

LISSU.jpg

Tundu Lissu akifutwa machozi wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo, ni halali.(PICHA NA Dewjiblog)

Ndugu,wakati wa kesi Tundu Lissu alikuwa thabiti na mwenye kujiamini, sasa baada ya kushinda kesi ndiyo anaonekana kulia.

Nini maana ya kulia huku kwa Tundu Lissu?

Kwa hisani ya Mjengwablog.
 
Nadhani kisaikolojia , mguso( reaction) ya matukio na hisia hujidhihiri kwa vicheko,hasira na hata machozi... Nadhani alitoka machozi ya furaha baada ya mapambano na hasa pale hisia zake zinapokutana na utashii au maamuzi. Kwa maneno rahisi Lissu aliamini kwamba ile kesi ilipikwa..akapambana nayo kwa nguvu zake na ujuzi wake wote kwa jinsi alivyoamini.... Ukifuatilia kesi yake utaona kwamba hoja za walalamikaji zilikuwa vichekesho mno. Pengine wanahabari wanaweza kumhuji akatuipa maaelezo yake ya hali hii ingawa saikolojia ya tabia ya binadamu nimeigusia hapo juu!
 
Topic nyingine ni za kijinga kwelikweli, haya na huyu Mchezaji wa Zambia hapa anafanya nini baada ya kuchukuwa Ubingwa wa Africa!!??....

chansa tears.jpg
 
Nini maana ya kulia huku kwa Tundu Lissu? Kwa hisani ya Mjengwablog.[/QUOTE said:
Simple! Over joyed!! Hujui hisisa ya furaha kubwa inapelekea hisia kali ya kucheka au kulia?
 
Tundu ana kila sababu ya kulia kwani hali ilivyokua pale mahakamani ilidhihirisha kwamba angepigwa chini kwa sababu yoyote ile.Labda kipengele kimoja tu ambacho Judge alikiona na yeye mwanasheria Tundu hakukiona.
Arusha mapolisi walikua wengi wakati wa hukumu ya kesi ya Lema kama ilivyodhihirika Singida siku ya hukumu ya kesi ya Tundu.Hali ilivyoonekana kimazingira,kwa mlinganisho na Ar hata wewe ungelia kwa matokeo yale.
 

Question 1: Was Jesse Jackson tears genuine?
500 × 333 - 103k - jpg
mrsgrapevine.com

Jesse Jackson reacts after projections show that Sen.
294 × 394 - 19k - jpg
belfasttelegraph.co.uk

Jesse Jackson sheds tears shortly after the news that Barack Obama captured ...
300 × 463 - 11k - jpg
latimesblogs.latimes.com

Jesse Jackson's tears of joy
308 × 480 - 36k - jpg
wp.theoblogical.org
 
Anajua kuwa ameshinda kwa dhuruma na ametumia ujuzi wake wa kisheria katika kupindisha sheria,
kwa hiyo yale machozi ni majuto ya nafsi kwamba anaonekana mshindi kwa njia zisizo halali.[/QU
nimekutana na vilaza ila wewe ni kilaza plus
 
Jaji Mzuna siyo mtu wa hovyo hovyo ni mtu mpole, muungwana, mpenda haki namjua vizuri nk Kesi ya Lema ingeangukia mikononi mwake Lema angeshinda!
 
Wanajamvi huyo jamaa hapo nyuma ya lisu mwenye kola nyeupe ni kaka yake wa kuzaliwa lisu anaitwa alute mughwai ndiye aliyekua wakili upande wa magamba kwenye kesi ya lema arusha mjini....

hahahaa! we njemba unashangaza sana, kama ni kaka yake wa kuzaliwa kwanini asingeitwa alute lisu badala ya alute mughwai?
 
Wasiwasi wangu huyo Jaji ataundiwa zengwe na kustaafishwa kwa kuwa tu katenda haki, hawa majamaa wa ththm noma kichizi..
 
Wakati mwingine macho huwa nilaana!Kama kweli waliofungua kesi hawakutumwa basi,kama walitumwa hawana muda watarudisha kadi CDM nakukiri hadharani!Nawawe makini wanapotaka kurudi CDM!
 
Tafsiri ya kilio chochote kiwe cha furaha ama huzuni ni kuwa huamini kama lililotokea limetokea ama limekuwa. Lissu hakuamini angeshinda na aliposhinda hakuamini.
 
lissu1.jpg

mbunge wa jimbo la singida mashariki chadema),tundu lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na shaban selema na pascal halu wa ccm,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge.

lissu.jpg

tundu lissu akifutwa machozi wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo, ni halali.(picha na dewjiblog)

ndugu,wakati wa kesi tundu lissu alikuwa thabiti na mwenye kujiamini, sasa baada ya kushinda kesi ndiyo anaonekana kulia.

Nini maana ya kulia huku kwa tundu lissu?

Kwa hisani ya mjengwablog.

lissu is only human and life can sometimes be overwhelming especially when you are tried for something you should not be!
 
kulia kwa lissu ni mawazo yaliomjia nghafla juu ya mustakabali mzima wa jinsi nchi inavyo endeshwa kibabe na viongozi wa juu,halafu akafikiria na kuamini jinsi haki haitendeke kwa walio wengi alizani na kwenye kesi yake hivyo hivyo badala yake hakuamini kilichotokea ikabidi alie kwa kusononeka kile asichokiamini maana ameshashuhudia kesi nyingi za wenye haki wakifungwa kwa manufaa ya watu.
 
Back
Top Bottom