Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Picha za Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo imewekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita leo tarehe 11 Januari 2021.

Ni muhimu sasa tukaambiwa kuwa makao makuu ya mkoa wa Geita yapo Chato, habari za kusema GEITA-CHATO badala ya CHATO -GEITA hatutaki
 
Kama kawaida CCM Mpya kufanya propaganda kwa kutumia takwimu zisizo sahihi kuwa wapo wagonjwa milioni 18 ukanda huo wenye kuhitaji huduma kutoka hospitali hiyo.

Ingekuwa takwimu hizo ni kweli basi Tanzania ingekuwa hoi taabani kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ktk eneo moja kupita nchi zote duniani. Na tungeona madhara yake kwa hospitali kufurika idadi ya wagonjwa hao huku wengine wakikimbilia Dodoma, Mbeya , Iringa , Kilimanjaro n.k kutafuta huduma za matibabu.



Johnthebaptist ilitakiwa habari hii isomeke Hospitali ya Rufani ya Chato kuhudumia ukanda huo wenye idadi ya wakaazi 18 milioni.

Eeenh, mkuu 'Bagamoyo', kwani kuna mtu anayehoji takwimu kweli siku hizi, mbali ya wachache kama wewe.
Hawa watu wanapenda sana kuyatumia haya manamba kila mara, kwa sababu wanajua hakuna anayeyadadisi kwa undani. Wengi wetu ni watu wa kuyasoma tu hayo manamba na kuimba nyimbo za kusifu.

Lakini hapo hapo, tunaambiwa kuna sheria inayohusu takwimu. Kwani maana ya sheria hii ni kuwabana wengine wote kama akina Zitto Kabwe; lakini haiwahusu hao wanaoisimamia sheria hiyo. Wao wana kila haki ya kuivunja sheria wanayotakiwa kuisimamia?
Hii ndio maana ya 'good governance'?
 
Nimecheka kwa nguvu, eti itatibu wagonjwa 18m kwa mwaka. Watanzania tuko karibia 60m, hivyo 18m ni 1/3 ya watanzania wote, kwahiyo 1/3 ya watanzania ni wagonjwa na wako kanda ya ziwa! Sifa na uongo mwingine hata ni aibu kuusema mbele ya watu.
 
Nani wa kuifufua Mtwara? Sijui nimewaza nini tu! Enwei kuchele.

Gesi inalazimisha kufufuka kwa Mtwara, huyu Msukuma akitoka mradi utaendelea tu. Gesi haiozi, Chato kufa ni rahisi sana maana hakuna sababu ya kudumu zaidi ya Rais aliyopo madarakani.
 
Chato viwanja bei gani?
Nataka kiwanja huko
Acha tu ndugu, nakumbuka nilijazwa wakati wa gas ya Mtwara nikaenda kununua kiwanja Mtwara. Hadi leo sijarudi huko. Nimegundua haya mambo yanaenda na upepo wa kiongozi, siku akitoka madarakani inakula kwako. Kuna wengine walinunua viwanja hapo Bagamoyo kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, leo hii hata kuuza huko 100,000 kwa heka ni ngumu.
 
Mimi ninachopinga ni ule uwanja wa ndege. Nadhani haukuwa wa lazima kabisa. Zile pesa zingeenda Mwanza kujenga temino ya kisasa au zikaenda Dodoma kuuboresha uwanja wa ndege pale.

Hapa kwenye hospitali nakubaliana na Rais kabisa. Wasukuma ndio kabila kubwa zaidi Hapa nchini. Kanda ya ziwa ndio eneo lenye watu wangu kuliko yote nchini. Ikiwa na hospitali ya rufaa moja tu pale Mwanza ilikua haikidhi mahitaji kabisa.

Kuwa na hospitali za rufaa tatu. Karibu Karibu kama hivi, yani Chato, Mwanza na Musoma. Kutasaidia sana kuipunguzia Bugando pressure. Yaani ilikua imezidiwa kabisa.
Chato hawapo wasukuma huko. Wangekuwepo angalau pangekuwa pamelimwa vizuri.
 
Picha za Hospitali ya Rufaa ya Kanda -Chato mkoani Geita ambayo imewekwa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita leo tarehe 11 Januari 2021.


Nimekuja kugundua Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa ni RAIS NA NUSU. Alitumia muda wake madarakani kuijenga Tanzania, sio Butiama au Musoma.

Hebu fikiria ule uwanja wa Ndege wa KIA ulioko Kilimanjaro. Frankly speaking, ule uwanja Nyerere angeweza kuujenga Mugumu Serengeti, ambako ni mkoa wa Mara anakotoka. Kwakeli katika kutembea kwangu Tanzania, nimegundua kuwa mji wa Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara ulipaswa kujengwa kimkakati, ili pamoja na jiji la Arusha, iwe ni major gateway za kuingiza watalii katika ukanda wa utalii wa kaskazini mashariki mwa Tanzania, ambao ndio strongest zone ya utalii Tanzania na Africa Mashariki. Hata wilaya ya Loliondo ina the same features kama Mugumu za kuwa strong gateway za kuingiza watalii wengi.

Lakini, Mwalimu Nyerere hakutazama kwao kwanza, bali alitazama nchi. Nilifanikiwa kumuuliza mzee mmoja ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchi ( kwa sasa ni marehemu), kwanini Mwalimu Nyerere aliamua kuijenga kaskazini mashariki mwa TZ kiutalii, badala ya Mugumu? Yule mzee akanijibu kuwa, Nyerere alikuwa haongozwi na ubinafsi katika kuijenga Tanzania, bali uzalendo na uhalisia wa hali halisi ya mambo. Akasema, pamoja na mapungufu mengi ya Nyerere, lakini weledi wake kiutawala ulimfanya aheshimike sana. Yule mzee akaendelea kusema kwamba, ukanda wa Arusha-Moshi ilikuwa ni sahihi kuliko Mugumu Serengeti kujenga uwanja wa ndege, sababu tourism ecosystem ya Africa Mashariki ilishikiliwa na jiji la Nairobi Kenya kwa kiasi kikubwa, ikifuatiwa na Arusha Tanzania, na miji hii inategemeana sana kiutalii. Vilevile Mlima Kilimanjaro una umuhimu wa pekee katika ecosystem ya utalii ya Kaskazini Mashariki mwa TZ. Kwasabu hizi, ilibidi KIA ijengwe ilipo sasa. Huyo ni Nyerere.

So far, sijashawishika kabisa na justification zinazotiwa na JPM kuijenga Chattle kwa speed na magnitude hii. Kama hospitali za kanda, serikali ilipaswa kutuambia kwanza, why Chattle na not elsewhere huko kanda ya ziwa. Likewise, JPM alipaswa kutuambia, hospitali za kanda zingine, zinajengwa wapi na lini? Ikumbukwe kuwa, tayari Chattle ina uwanja wa ndege wa kimataifa, of which, hakuna so far hakina vivid economic rationale ya kuujenga huo uwanja pale. Ni bora huo uwanja ungejengwa katika mji wa Katoro-Geita sababu wafanyabiashara wengi wangeutumia kuliko kwenda Mwanza. Frankly, mji wa Chattle hauna any economic rationale ya kujengwa uwanja wa ndege kwa sasa. Alafu hatujazungumzia proposed ujenzi wa uwanja wa mpira Chattle, na ujenzi unaoendelea wa maofisi makubwa ya umma, ambayo hadhi yake inazidi hadhi ya majengo ya aina hiyo katika wilaya zingine.
 
Kwa nini unaamini ni ushauri mbovu na sio maamuzi yake mwenyewe?

Waafrika pamoja na Wakomunisti wa China na Russia tunaamini Rais ni Mungu Mtu, akichemka tunasema likikuwa ni wazo la washauri kwa sababu Rais hawezi kutunga wazo la kiduwanzi kiasi hicho. Tunakwama hapo pia kwa sababu tunashindwa kuwalaumu na kuwawajibisha wao binafsi.
Ata kama ni maamuzi yake kabla ya kujenga ana wataalamu wakumuelewesha criteria za kufanya such an investment.

Hospitali yenye uwezo wa kuhudumia watu 700 kwa siku rural district sio mahala pake kutokana na factor abc za everyday operation requirements.

Kwa ivyo ni swala la education pia kwa upande wake sio kila wish yake apewe; if it’s not practical inabidi aelezwe pia.
 
Naona Chato kumeCHATUKA! Ni jambo jema, haya ngoja sasa nirudi kwetu SMZ kama wana mpango japo wa kupiga rangi Hospitali ya Mnazi Mmmoja au ndio kina Balozi Sefu hawakuacha ata chenji :D
 
Hakika mkuu...

Itafika siku MAGUFULI atakumbukwa kwa wema mno...

Si Katika kipindi chake Cha UONGOZI....ila akiondoka....atakumbukwa zaidi ya WENGI WALIOPITA....

Mungu Mwenyezi atupe uhai mrefu aaamin pale tutakapoyahitaji sana maendeleo ya VITU NA WATU huku YAKISIMAMISHWA TU MAENDELEO YA WATU PEKEE.....

Muda utaongea.....
Atakumbukwa kama anavyokumbukwa Mobutu DRC.
 
Back
Top Bottom