ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,114
- 49,840
Pamoja na ufuatiliaji wangu wote wa mambo ya Serikali, ziara ya Rais Samia Mikoa ya Kusini ndio imefanya nimejua kwamba kumbe Mama amejenga bonge la hospital Mpya ya Mkoa wa Lindi.
Nafahamu Kuna Mikoa zinajengwa hospital kama hii mfano Shinyanga,Songea, Kigoma, Ukerewe na Rukwa(Mpango) ila sikuwahi jua Kwa upande wa Lindi.
Mama anafanya miradi Mingi sana kwenye sekta zote ila inaonekana Kitengo cha habari kwa Umma cha Serikali kinapwaya kwenye kuhatarisha Umma au kuna kusudi inafanywa ili ionekane hakuna kitu Rais anafanya.
Kukitokea Changamoto hiyo ndio inashikiwa bango kana kwamba bila hiyo Changamoto hakuna maisha eg Bandari vs DP World, mafuta na Sasa umeme. Ukiwakuta wanavyo comments huko mitandaoni unaweza dhani Kila kitu kimesimama na maisha ni very worse.
Kuna Ile awamu iliyopita yaani Kila kamradi kalishikiwa bango kuanzia Stand Hadi vyoo vya shule bila kusahau viwanda vya vyerehani nk. Je, Mama hana Kitengo Cha Propaganda? Maana kwa jinsi awamu hii ilivyo na utitiri wa miradi nilitegemea mambo ingekuwa smooth sana au tatizo ni nyota?
My Take
Ingekuwa ni Ile awamu ya Wazalendo wa Chato tusingeekunywa maji maana hata hospital ya Kanda ya Kusini Mtwara tukiambiwa ni wao wamejenga kumbe mradi ulinza na Nyerere 1978 ukasima ndio kaja uendeleza na Samia kaukamilisha.
Hongera Rais Samia ila Sasa jitahidi kuwa na wasemaji wako vinginevyo hata hii miradi utaambiwa ni miradi ya Mwendazake.
HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA LINDI KUZINDULIWA NA RAIS SAMIA LEO
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo mchana anatarajia kuweka jiwe la Msingi Hospitali ya Rufaa Lindi (MITWERO), ambayo kwa hadhi yake inafanana kabisa na Hospitali zingine kubwa Kama Muhimbili ya Dar es Salaam.
Aidha wananchi wa Mkoani humo wamefurahishwa sana na jitihada hizo za Mhe. Rais kuwajengea Hospitali hiyo kubwa na kupunguza kero waliyokuwa wanaipata hapo Mwanzo kusafiri nje ya mkoa kupata huduma ya matibabu kwa yale Magonjwa Sugu.