- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na watu wanapost huko X kuwa Mchezaji Aziz Ki amevuta jiko lingine
- Tunachokijua
- Februari 16, 2025 mchezaji Aziz Ki akiwa katika klabu ya Dar Young Africans alifunga ndoa na msanii na mwanamitindo kutoka nchini Tanzania, Hamisa Mobeto.
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na picha inayosambaa ikimuonesha mchezaji huyo akiwa na mwanamke mwingine wakiwa na ishara ya kufunga ndoa na kuelezwa kuwa mchezaji huyo amemuoa mwanamke mwingine.
Uhalisia wa madai hayo
Kupitia ufuatiliaji kwa njia ya mtandao jamiiCheck imebaini kuwa hakuna chanzo chcohote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ukilinganisha na ndoa yake ya awali.
Ufuatiliaji kuumia reverse search imeonesha kuwa picha hiyo imachapishwa mtandaoni hivi karibuni lakini haijachapichwa na vyanzo vya kuaminika. JamiiCheck imefuatilia pia mitandao ya Aziz Ki na kubaini kuwa haijachapishwa katika ukurasa wake rasmi wa mitando ya kijamii.
Aidha ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo ya kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde imebainisha kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa teknolojia hiyo kwa takribani 99%.