PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

Duh! Hayo magari mpaka yanatumbukia madereva hawakuona vionyeshi hatarishi? Au ndio mambo ya ngoja niwahi kabla hapajameguka?

Naona namba za magari ya serikali, ukute ulitoka nalo kwa shughuli binafsi.
 
Kuanzia asubuh hadi mda huu sijajisoma bado kesho ntaenda vipi kwa ofisi
 

Attachments

  • 1397418565175.jpg
    1397418565175.jpg
    13.1 KB · Views: 307
Huwa hatuna tabia ya kujifunza kutokana na majanga kama haya.
Mvua iliyopiga Dar ni kubwa lakini maafa yaliyotokea ni makubwa zaidi ukilinganisha na mvua yenyewe.
Sio mara ya kwanza maafa ya mafuriko kutokea Dar na kila yanapotokea huwa tunalalamika miundo mbinu mibovu, mvua zikikata tunasahau kila kitu. hakuna hatua tunazochukua.
 
Thanks for the updates!!! Hali ni hatari!!!!
Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira.

Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika na mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi hasa wanaoishi bondeni au kwenye mkondo wa maji mfano mito.




attachment.php


attachment.php


Aprili 12, 2014
 
Tatizo ni kuwa tuliokulia hapa mjini tunajua maeneo mengi Dar ambayo yamejengwa nyumba hayakustahili kujengwa lakini watu wamevamia na kujenga. A big portion of Dar ni mabonde! Mvua nyingi zikija lazima maji yafurike. Inasikitisha ila for once tusiilaumu serikali!! Wengi waliokumbwa na mafuriko ni wale waliojenga mabondeni. Sasa hata wale wa jangwani wanailaumu serikali wakati walipewa viwanja, mabati na tofali!! Wao wakataka serikali iwajengee!!!!!
 
Naona Blogu njaa ziko kazini.Picha za kitambo zinatumika.

Nikweli mkuu

Lakini hiivi ni kwanini kila mwaka ni mafuriko tu?

Mungu kama ananisikia ningeomba inyeshe mvua ambayo itasababisha mikoa muhimu yote nchini kuzama kabisa na asipatikane hata mtu mmoja ili angalau tujulikane vile ambavyo hatuna maana kwenye vichwa vyetu

Utadhani hatuna serikali!
 
Kuhu usafi umakuta mitaa hata 10 hakuna hata sehemu 1 yakutupa taka hata kama ipo takataka haziondolew kwend dampo. Mipango miji na upimaji wa viwanja una matatizo mengi kupata kiwanja mpaka utoe rushwa wanagawa viwanja bila miundo mbimu barabara nk
 
\

unapojenga nyumba na kufanya specification ya sitting room , dinning room and bedding room this is your plan kama baba mwenye nyumba

hii inapaswa kutumika kwa viongozi wetu pia (city planner)
  1. shule wapi
  2. makazi ya watu wapi(high and low density)
  3. industrial area wapi
  4. market wapi
  5. play grounds wapi
  6. kanisa wapi na misikiti wapi

yote hapo juu yanatakiwa kuwa specified by the government through their city planners, Rafiki yangu mwenye uelewa wa mashaka kama kiwanja kinauzwa na mabalozi wa nyumba kumi kwanini kusiwe na shida

Ni kweli kabisa
 
Majanga!

Picha tumeona nini kifanyike sasa???????

mkipewa habari hivihivi mnataka picha, mkipewa picha, mnauliza kipi kifanyike, kweli ubinadamu kazi. ila ni vyema swali lako ukalielekeza kwa kitengo kinachosubiria maafa yatokee ndio kifanye kazi.
 
Nikweli mkuu

Lakini hiivi ni kwanini kila mwaka ni mafuriko tu?

Mungu kama ananisikia ningeomba inyeshe mvua ambayo itasababisha mikoa muhimu yote nchini kuzama kabisa na asipatikane hata mtu mmoja ili angalau tujulikane vile ambavyo hatuna maana kwenye vichwa vyetu

Utadhani hatuna serikali!

Kwa maombi Haya Bora tu Mungu asikusikie!
Hah!!
 
aisee, nilidhani mbagala tu ndo kuna miuondombinu mibovu, kumbe hata mwenge????????????? na kwa style hii mbagala safiiiiiiiii!!!ila Mungu atusaidie tusisikie vifo kabisa hata kama kuna uharibifu kiasi hiki.
 
sasa babangu, ndo hapo nauliza town planners wanafanza nini nji hii? kama woote town planners na wataalamu wenzao wanaenda kupima kiwanja (ambacho ni ghali, tunamuongelea anaeishi jangwani mostly kwa sababu ndio kuna nyumba affordable na pengine anakwepa nauli ya kwenda kazini pia kupunguza gharama za maisha. huyu mostly ni mfanyakazi kibarua asie na ajira ya kudumu, na waziri wake kaidhinisha mshahara wa tzs 80,000/= kwa mwezi na halazimiki kumlipia bima ya afya). unaendaje kupima kiwanja mahali penye mkondo wa maji? :A S 13:

na bado tusiilaumu serikali? seriously, wanaoishi mabondeni unadhani hawangependa kuishi mbezi beach ama masaki? watu hawana choice kama unavyodhani kakangu.

vitu vingine bana huitaji serikali ukuamlie, pesa si yako ya kununulia kiwanja, iweje uchague kwenye bonge, wakati kuna milima huko umeicha, ina maana wenye maisha duni ndo wanaishi mabondeni tu, hujaona nyumba kali hapo zimezungukwa na maji, mabonde ni kwa ajili ya kilimo baaaaaaas, basi hii serikali ina kazi sana karibia itaanza kupanga ratiba za milo kwenye majumba ya watu.
 
Back
Top Bottom