Mvua zaendelea kuwa kilio kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,779
1685974990954.png

Dar is big Slum ni Jiji la hovyo sana,mvua kidogo mnaanza kutafutana,Barabara shida,foleni,vinyesi na upuuzi kama huo.

Bado mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam zimeendelea kuwa kilio kwa wakazi wake kutokana na adha ya usafiri wanayoipata kufuatia baadhi ya barabara kujaa maji.

Hayo yanathibishwa na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu wanaodai maeneo mengi yaliyokuwa sugu kwa kujaa maji kipindi cha mvua kama Jangwani na Kamata yameendelea na hali hiyo jambo linaloleta kero kwao.

Mvua hizo zilizoanza kunyesha kuanzia alfajiri ya kuamkia leo Juni 5, 2023 zimeleta madhara mbalimbali kwa wakazi wa jiji hili ikiwemo kushindwa kufika kazini kwa wakati.

Wakizungumzia changamoto hizo watumiaji wa barabara jijini hapa wamedai licha ya kujengwa kwa lami zimekuwa zikijaa maji kiasi kwamba hata watumiaji wa vyombo vya usafiri wanaogopa kupita.

“Eneo la Kamata limekuwa sugu limekuwa likitusababishia vyombo vyetu kama hizi pikipiki kuharibika,’’ amesema Joseph Stanley ambaye ni dereva wa bodaboda eneo la Kamata.
 
Back
Top Bottom