Daraja la Somanga limekatika

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,092
2,605
Wakuu wale wanaosafiri toka Dar kwenda mikoa ya kusini yaani Mtwara na Lindi tunawaombeni mchukue tahadhari kwani daraja maeneo ya Somangafungu limekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
1711350990011.png

======
Daraja la Somanga linalounganisha barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara limekatika na kusababisha magari kukwama njiani.

Kwa mujibu wa waliopo eneo hilo, daraja hilo limekatika leo Jumapili Machi 24, 2024 saa 2 usiku na jitihada za kurejesha mawasiliano zinaendelea.
 
Back
Top Bottom