PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira.

Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika na mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi hasa wanaoishi bondeni au kwenye mkondo wa maji mfano mito.




attachment.php


attachment.php


Aprili 12, 2014

LEo ni majanga kila kona. Nilikuwa na kikao na DC bagamoyo. Nimefika mapinga daraja ukingo umekatika. Nimerudi nipite Tamco kibaha nakuta foleni kali Kibamba, naambiwa daraja la Kabila ya Mizani Kibaha nalo limekatika.eeeeheh.hayo yote ukandarasi wa KI CCM.

Mburahati na Mayfair leo asubuhi

attachment.php

Saturday, April 12, 2014




bongo5.jpg

MVUA.jpg




Kariakoo Jijini Dar hali ya mvua ipo hivi... ni hatari tupu

Foleni nayo usiombeeeeeeeeeeee....

12.jpg

Sehemu ya maduka yaliyopo eneo la Kituo cha daladala cha ITV yakiwa yamezingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Kutokana na mvua hizo na maji kujaa kumesababisha msongamano mkubwa wa mago kuanzia jana jioni na leo.


Barabara ya kuelekea Goba....


Barabara ya Goba ikiwa imeharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.


Maji yakitiririka kwa kasi katika Mto Mbezi eneo la Bondeni...


Vijana wakitumia fursa vizuri kwa kujipatia mchanga unaotiririshwa na maji ambapo huwauzia madereva wa maroli.


Eneo la Mwenge karibu na kituo cha daladala.....



Moja ya daladala lililokuwa gereji likiwa limezingirwa na maji eneo la Mwenge....


Maduka ya Mwenge yakiwa yamezingrwa na maji.....


Mdada huyu alikuwa akipiga hesabu na kujiuliza jinsi ya kuvuka maji yaliyojaa na kukatiza barabara eneo la ITV.


Mwenge karibu na Zahanati...... hakuna njia ya kuingilia Zahanati


Maduka eneo la Mwenge yamejaa maji....


Kazi haifanyiki leo katika maduka haya...


Mwenge eneo la Nakiete......



Maji yakikatiza barabara eneo la ITV.

source; MasaiNyotambofu
 

Attachments

  • IMG-20140408-WA0012.jpg
    IMG-20140408-WA0012.jpg
    88.9 KB · Views: 57,035
  • new.jpg
    new.jpg
    247.4 KB · Views: 3,879
  • IMG-20140408-WA0011.jpg
    IMG-20140408-WA0011.jpg
    77.2 KB · Views: 52,189
  • 20140408_120335.jpg
    20140408_120335.jpg
    258.5 KB · Views: 5,817
  • 20140408_120254.jpg
    20140408_120254.jpg
    344.4 KB · Views: 5,720
kinachosikitisha makosa haya yaliyofanyika jangwani yanaendelea kufanyika mbezi, kimara na ubungo wananchi kujenga kwenye mikondo ya mito like there is no city planner

hii mbaya sana


ni madhara ya kuendelea kuweka CCM madarakani
 
kinachosikitisha makosa haya yaliyofanyika jangwani yanaendelea kufanyika mbezi, kimara na ubungo wananchi kujenga kwenye mikondo ya mito like there is no city planner

hii mbaya sana


ni madhara ya kuendelea kuweka CCM madarakani
Mwulize Mbowe ruzuku kapeleka wapi, watu wanavua magwanda!
 
Mungu awanusuru wakazi wa huko(Ameen)

Subirini tumalize Operation safisha jiji,ondoa machinga,bodaboda na Bajaji kisha ndio tutafirikira kuja kuzibua mitaro ya maji.
Dar ni miongoni mwa Majiji machafu sana Duniani,na pia ndio mji wakiishi viongozi wakuu karibu woote.
Nitaitisha kikao leo jioni ili tupige posho kisha saa mbili kwenye taarifa ya habari nitawajibu
By Mkuu wa mkoa Meck Sadiq
 
Hivi kila siku itakuwa ni hivi hivi alafu badae watatuonyesha wanazunguka na helkopta kujionea badala ya kutatua tatizo ikiwezeka hata maamuzi magumu kufanyika kuepusha maafa katika jamii.
 
how magwanda related to this sir how uropokaji ndio asili yako
Nilikuwa najibu swali lako la awali kwa city planners, wewe unahamia bondeni halafu unategemea nini?
Wakati huo huo hata hao magwanda wanawafikia wapiga kura wao kwa helikopta, ndio maana wamefilisika sasa, na watu wanavua magwanda kwa kuona hayana msaada.
 
kinachosikitisha makosa haya yaliyofanyika jangwani yanaendelea kufanyika mbezi, kimara na ubungo wananchi kujenga kwenye mikondo ya mito like there is no city planner

hii mbaya sana


ni madhara ya kuendelea kuweka CCM madarakani

Kuna wakati aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mzee Makamba aliwakemea watu wanojenga kwenye mabonde,namnukuu "hivi nyie watu mnaopenda kujenga kwenye mabonde ya mito mmekuwa vyura?" Tatizo hapa sio CCM, tatizo ni watanzania tumekuwa wabishi, hatuwasikilizi viongozi wetu mpaka maafa yatokee ndo tunaanza kuliaumu serekali! Walishaambiwa siku nyingi hawa lakini wamekuwa viziwi na sasa wanavuna walichokipanda. Ukweli ndo huo na unauma.
 
Nilikuwa najibu swali lako la awali kwa city planners, wewe unahamia bondeni halafu unategemea nini?
Wakati huo huo hata hao magwanda wanawafikia wapiga kura wao kwa helikopta, ndio maana wamefilisika sasa, na watu wanavua magwanda kwa kuona hayana msaada.
\

unapojenga nyumba na kufanya specification ya sitting room , dinning room and bedding room this is your plan kama baba mwenye nyumba

hii inapaswa kutumika kwa viongozi wetu pia (city planner)
  1. shule wapi
  2. makazi ya watu wapi(high and low density)
  3. industrial area wapi
  4. market wapi
  5. play grounds wapi
  6. kanisa wapi na misikiti wapi

yote hapo juu yanatakiwa kuwa specified by the government through their city planners, Rafiki yangu mwenye uelewa wa mashaka kama kiwanja kinauzwa na mabalozi wa nyumba kumi kwanini kusiwe na shida
 
Wabongo hatujaelimika kuhusu usafi. Utaona vifurushi kibao vya taaktaka vinaelea. Hata kam wataweka mifereji bado itaziba tu.. Vitu vingine yutailaumu serukali wakati wenyewe hatujisaidii
 
Halafu kuna watu wanasifia kuwa Dar kuna skyline nzuri. Wakiambiwa mambo ya muhimu ni kuboresha sehemu wananchi wanapoishi, wanang'aka!!

Asilimia 70 mpaka 75ya DSM ni nyumba mbazo hazikujengwa kwa mpangilio na mbaya (slums/shanties) na wengi ndipo wanaishi.
 
Back
Top Bottom