PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

Ni wakati muafaka wa kuhamishia huduma za serikali na wafanyakazi kwenye makao makuu ya nchi DODOMA.
 
Hizi picha za huyo binti na huyo kijana ni za zamani kama sikosei ni mwaka uliopita, mleta mada kafanya kuxipandishia tu hapa..


Watanzania wa DSM poleni sana na Mvua hizi zinazoendelea. ni maafa hasa sehemu ambazo si za kilimo, huku kwetu zinanyesha pia tunajishauri tukapande nini maana msinu umepita

nngu007Jamaa yangu vipi huyu Dada uliyemchukua picha akibebwa ilikuweje abebwe ba kundi zima na mkoba bila kulowana.
du siku nyimgine ma Photographer muwe mnasaidia hata kuokoa baada ya kupiga picha

majanga+3.jpg

majanga+1.jpg

majanga+2.jpg
 
APR132014




Screen-Shot-2014-04-13-at-4.01.50-PM.png


Asubuhi April 13 2014 makamu wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecky Sadick na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dsm Suleiman Kova walipata ajali ya Helikopta iliyoanguka uwanja wa ndege Dar wakitaka kutembelea sehemu zilizo athirika na mafuriko.

Mwandishi mmoja aliekuepo kwenye ndege hiyo aliongea kwa ufupi anasema wakati wanaanza kupaa, ni kama upepo mkali ulikua unaivuta Helikopta kurudi nyuma ikiwa imepaa urefu wa kama futi tano ambapo ilizidiwa nguvu na kugonga paa kisha ikaanguka.

Baada ya ajali walijitazama wakaona ni wazima isipokua michubuko midogomidogo kisha wakarudi kwenye magari yao na kuyatumia kuelekea moja kwa moja kwenye maeneo waliyokua wamepanga kwenda kwa Helikopta.


Makamu wa Rais akionyeshwa na katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Injinia Mussa Iombe, sehemu ya daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam lililokatika kutokana na mvua kubwa.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Injinia Mussa Ibrahim Iombe wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick.

Malori yakiendelea kumwaga vifusi vya mawe kwenye daraja hilo



Nguzo za umeme baada ya kuzidiwa nguvu na maji yaliyobomoa daraja.






Picha zote zimepigwa na OMR


 
Hizi picha za huyo binti na huyo kijana ni za zamani kama sikosei ni mwaka uliopita, mleta mada kafanya kuxipandishia tu hapa..
Hata hii si ya mwaka huu maana naikumbuka tunayo humuhumu JF
Kweli kalamu (picha) inaweza kuua (kuleta vita) au kujenga Nchi
Hofu ilishanipamda hawa watu kila siku mafuriko kwao tu na wanapanda kila siku hicho kibaraza cha nyumba yao?
tena ni walewale

bongo5.jpg
 
Mvua na inyeshe tu, kuna watu wanameamua kuwa samaki na Hawataki kuondoka mabondeni
Yaani"

hivi serikali inashindwa kuwabana kina NSSF na PPF wajenge maghorofa yenyenyumba za vyumba hata viwili wapangishwe Watu wa mabondeni, wakusanye kodi na wawape muda hata wa miaka mitatu au nne kuishi humo. Kisha wajipange kutafuta maeneo ya kujenga nyumba zao za kudumu Baada ya hiyo miaka minne. Badala ya kujenga mijumba ya mamilioni inayoweza kununuliwa na mafisadi.
 
kinachosikitisha makosa haya yaliyofanyika jangwani yanaendelea kufanyika mbezi, kimara na ubungo wananchi kujenga kwenye mikondo ya mito like there is no city planner

hii mbaya sana


ni madhara ya kuendelea kuweka CCM madarakani
Acha ujinga wako mwehu wewe kwani ccm ndiyo iliwaambia wajenge bondeni watu wanaumia unaleta siasa mpuuzi kweli wewe.
 


10245459_731499710204062_3795484696833819556_n.jpg




Mkazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa ameokoa baadhi ya mali zake huku asijue kwa kwenda





Mbali ya nyumba hizi kufunikwa na maji ila bado nyumba hii kushoto umeme unawaka jambo ambalo ni hatari zaidi na Tanesco wanatazama (picha na Mroki Mroki)



Hivi ndivyo mvua inavyowatesa wananchi wanaoishi mabondeni jiji Dar es Salaam ila bado hawataki kuhama
















1903013_228076957390205_7736600670026576248_n.jpg


Source: Kandili Letu
 
Wow Uzuri ni Dar hakuna NYOKA au MAMBA wala Watu...
 
Aiseee hatari sana

hiyo picha kubwa kama maeneo ya sokoni imezungukwa na maji mengi ni wapi hapo!!!!
 
Duh! Hayo magari mpaka yanatumbukia madereva hawakuona vionyeshi hatarishi? Au ndio mambo ya ngoja niwahi kabla hapajameguka?
 
Dereva aliepanda juu ya mti akaacha Land Cruiser ni wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
 
kiukweli miundombinu yetu inatukwamisha ktk kipindi hiki najaribu kujiuliza huu ugonjwa utakuja kuisha na je ni nani atakumbuka kuboresha hali hii? baada ya kuona mafuriko haya nimemkumbuka yule dereva wa roli aliyezolewa na maji akijaribu kuvuka daraja(pumzika ktk aman) ningewaasa madereva wengine kuwa makini maji ni kitu hatari sana...
 
Kweli lakin haya majanga yanatisha,usiombe yakukute polen sana wahanga wa mafuriko!
 
Back
Top Bottom