Brother!
Huo ni msimamo wa Ibn Taymiyyah na walioshika njia yake.
Siyo kweli wasome kina Imamu Shafii utakutana na kauli zao kuhusu Falsafa, watu Hawa walichukua mawazo hayo mgando Toka kwa Wakristo na kuyaingiza katika itikadi ya Uislamu, yakazaliak mapote kama Qaadariyyah, Muutazila, Jahmiyyah, Ashaira na wengine.
Lakini wapo wengine waliosema falsafa ipo na maneno ya namna hii yapo hata kwenye Quran. Mfano wa huyu ni Imam Ghazal na wengineo.
Naomba unipe aya inayosema hivyo au ulivyo DAI Toka kwenye Qur'aan.
Inaonekana humjui Imam Al-Ghazal, kwanza kipindi chake alibishana nao sana watu Hawa na mpaka akaandika kitabu kiitwacho "Tahafut Al Falaasifa" itakuwa humjui Imam Al-Ghazal, japo aliathariwa na watu hao mpaka akawa Ashaira, ila inasemwa kabla ya mauti yake alitubu.
Wengine walio tubia kutokana na fikra hizo za kifalsa ni Imam Abu Musa Al Ashaariy, Imam Abul Maali Al Juweiny. Soma haya mambo upambaukiwe kijana inaonekana uko mbali na hivi vitu.
Wanazuoni wengine walio isema vibaya Falsafa,Ilmu Al Kalam, Ilm Al Mantiq ni Imam Al Harawi katika kitabu chake "Dhamu Al Qalam wa Ahlihi" kadhalika Imam Suyuti, Sasa unaposema ni msimamo wa Imam Ibn Taymiyyah unaonyesha wazi kwamba huna ulijualo juu ya haya mambo.
Wewe kwako ukiona ni haramu ni mtazamo wako na unaheshimiwa. Kwa wengine si haramu heshimu pia mtazamo wao.
Nitajie wanazuoni wakubwa katika Uislamu wenye kuruhusu kusoma Falsafa, Mantiq kuanzia kina Imam Abuu Hanifa, na wengine.
Na hapa aikhtalifiwi Mtume. Bali inaikhtalifiwa fahamu/uelewa wako na waliyo na ufahamu kama wako.
Unaijua Falsafa ? Mimi nimewahi kuisoma na kisadiki. Unajua athari iliyo letwa katika Itikadi ya Uislamu baada ya Waislamu kujifunza Falsafa ? Unawajua Ahlul Qalam ?
Kijana huijui Falsafa, ndiyo maana unasema maneno haya, ukiwasoma Ashaira wao kutokana na hizo fikra wakakanusha sifa za Allah na kuthibitisha sifa sita tu, lakini chanzo ni wao kuathirika na falsafa wakatumia akili zao kumeuelezea Allah, wakaacha nususi (Qur'aan na Sunnah).
falsafa ni jaribio la kuelewa na kueleza kwa kutumia akili inayofuata njia ya mantiki. Na mantiki ni aina ya msingi wa kufikiri kwa ujumla jinsi ya kutoa hoja sahihi!
Kufasiri Falsafa kama Jaribio hii siyo sahihi, na sijaona maana hii hapo kabla. Falsafa ni fani pweke kwayo Ina misingi yake ukitaka kuelewa maana ya Falsafa msome Aristoto na zile Ten Categories (Maaqulat Ashara) zake msome alipokuwa anaelezea chanzo.
Tumia Misingi ya Mantiki kuelezea chanzo Cha Ulimwengu na kumuongelea Muumba. Ukipatia Mimi naacha kutumia hii jf. Sasa Mantiki kama mnavyo fasiri ni njia ya kumfanya asikosee katika kujenga hoja kwa kutumia akili.
Kingine, unakubali ya kuwa akili ina ukomo ?