Philosophy is a disease for both theists and atheists

Philosophy is a disease for both theists and atheists

Brother!

Hata waliyoikubali Quran na Mtume hawakuikubali kibubusa! Bali waliikubali Quran na mtume baada ya kufikiri kwa kina; aidha kwa hoja au kusikia kilichosemwa na Quran.

Tangu mababu zangu walisema haya masanamu ndiyo miungu. Muhammad anakuja na hoja zake anasema hawa si miungu bali kuna Mungu! Haya mambo yapoje!

Walitumia akili kwa usahihi si kwa mtindo wa logic. Logic ni fani pweke, ambayo msingi wake ni akili pekee, Sasa kwa uhalisia akili haiwezi kudiriki kila kitu. Hili jambo la kwanza. Sasa nitakuuliza hao maswahaba walitumia logic ? Kumbuka hapa tunaongelea logic kama fani na si kama matamko.

Sababu kila mtume alikuja baada ya kutanguliwa mitume wengine, ukirejea historia mitume utaona mitume wamekuja kujibu maswali ambayo akili imekoma. Walikuwa na nyenzo za kuwafanya watu waamini ikiwemo miujiza. Kingine kila mwanadamu ameumbwa na hali ya kumjua Allah yaani Fitrah.
 
Everybody is a day dreamer life in the world is a dream,wewe ukiwa unaota usiku ukiwa kwenye ndoto muda ule unaota unajua kuwa hapa naota?
Mi samtaimu najuaga, wapo wengi tu wanaowezaga kujua wanaota af wakaendelea kuota au kuamka.

Tena mara nyingi hawa ndio wanaoweza kukuelewa unachozungumza maana wana uwezo wa kujitambua from time to time. Sema tu mda mwingi tunaamaua (na wewe included) ili maisha yaendelee na tusionekane machizi. It is normal bro.
 
Hapo mtu anafanya correct reasoning ambayo kiujumla inaitwa logic (mantiki). Na Logic inamfanya mtu anafanya uwiano anachanjua fikra ili aweze kuwa na wazo sahihi. Kumbuka hapo kote mtu anatafuta kuelewa ili ajiridhishe: Sasa ile hali ya kuwaza na kuwazua yaani unafanya ni kama jaribio ili mradi uweze kuelewa unachokifikiri wakati unafanya reasoning na hitimisho kwa kuelezea hicho ulichokichanjua kwa njia ya kufuata logic(mantiki) na logic ni correct reasoning; hii ndiyo inaitwa falsafa.
Nilikuuliza hivi maneno na logic kipi kilianza ?!

Kufikiri kwa usahihi hakuhitaji logic kama fani. Sababu tunaweza kufikiri na kupatia pasi na logic.

Nilikupa kazi utumie akili kupatia katika chanzo Cha ulimwengu. Kama Falsafa ingekuwa ipo katika kuupata ukweli au kupatia katika kufikiri wangepatia katika kutambua sifa za Mola na chanzo Cha Ulimwengu.
 
Vipi kama ungelikuwa kipindi cha Mtume Muhammad na angelikuambia yeye ndiye Mtume aliyetumwa na Mungu marejeo yako ungeliyafanyia wapi? Kipi ambacho kingelikufanya uamini na usadiki kuwa Muhammad kweli ni Mtume na ni kweli ametumwa na Mungu?!

Hakuna rejea nusus hapo Muhammad ndiyo kakufuata kakwambia hivyo utasemaje?
Falsafa zinawafanya muwe wajinga sana, ulimsoma Waraqah Bin Nawfal bin Abdul Uzza ? Yule mtu ilikuwaje akamuamini Mtume zama zile ? Jibu rahisi sana Sababu alikuwa na Elimu ya mambo yale na Mtume si wa kwanza katika kufikisha ujumbe juu ya Mola ?

Kijana Sasa hapa ndipo utakapo ona matumizi sahihi ya akili si kama unavyotumia wewe kujenga tatizo na kulitafutia ufumbuzi kwa akili yako wakati majibu ya tatizo Hilo yapo tayari. Huu ni uvivu wa kufikiri.
 
Can you prove nothingness exists?

Other than an abstract idea?

Even the abstract idea of nothingness is not nothingness, it is an abstract idea, with properties.
Hapa upo sawa, nobody can prove that nothingness exists. One can only know that nothing exists.

To prove one needs something already, but if you think about it everybody just know that nothing is
 
Bado unakumbuka!

Nina majukumu Mungu. Msimamo wangu bado upo vilevile Mungu hayupo Mbinguni.

Na usifikiri huwa nashindwa bali napuuzia ninapomuona mtu si muelewa. Ushahidi ninao ila hapa si mahala pake.

Niwekee link ya huo Uzi hapa kwenye hii koti nitaenda kukujibu hukoo!
Nimecheka sana. Hili Kama wakubwa zako walishindwa kuthibitisha wewe huwezi mpaka unakufa.

Shida yenu hamsomi haya mambo, wakubwa zako kama hujui wali nakili fikra za ambqo siyo Waislamu wakaziingiza katika Uislamu. Ndiyo maana mwisho wa siku walikuja kujuta na kurejea katika hali.

Huo uzi siukumbuki kwa jina nachokumbuka ni kuwa uliomba udhuru na hukurudi tena.

Ushahidi wa kusema Mola hayupo Mbinguni huu huna, na hautakuwa nao mpaka unakufa. Sababu nawajua vizuri sana nyinyi tena kwa kuwasoma vitabuni.
 
Hakuna Nothingness hapa ulimwenguni au nje ya ulimwengu.
Maana Kuna possibility ya Multiverse labda uwe hujui.

Atathibishaje kitu ambacho hakipo.
Kumbe ulikuwa umeshakazia.

Kisichokuwepo hakithibitishiki. Labda kama tutatumia kigezo ambacho kipo nje ya hicho kitu. Na hapo tutarudi kwa bwana Godell nadhani na ile incompleteness theorem yake.
 
Mi samtaimu najuaga, wapo wengi tu wanaowezaga kujua wanaota af wakaendelea kuota au kuamka.

Tena mara nyingi hawa ndio wanaoweza kukuelewa unachozungumza maana wana uwezo wa kujitambua from time to time. Sema tu mda mwingi tunaamaua (na wewe included) ili maisha yaendelee na tusionekane machizi. It is normal bro.
Nakuelewa
 
Kwanini Wanafalsafa wote katika harakati zao walishibdwa kupatia katika chanzk Cha Ulimwengu. Rejea historian ya Wabafalsafa wa kale wa Magharibi, kina Socrates, Aristoto, Plato na wengine ?
Chanzo cha ulimwengu kujulikana kilihitaji ufunuo.

Brother, hata mimi ninakubali kwamba UKWELI ndio upo na ndio mkubwa kuliko chochote huku chini.
Niandike kizungu ndio kina maneno mengi; kuna,,, there is TRUTH which is above everything below. And that is all and the vice versa so it is nothing. Only an eternal God can understand that very well. But here we are time bound humans and can find and comprehend facts. Facts are bits of truth but not complete truth. In order to find truth we need to draw relationship between facts. This act is called philosophy. Philosophy helps us understand the facts and build(I mean discover) the truth. This is the hard way.
Sometimes we get revelations which shortcuts this process and it reveals the truth. This is the easy way.
Both ways have their place, we live with both. They complement each other.

Wewe Kisai umekuwa fiti zaidi kuuelewa ukweli ni kwa sababu ya kutumia hizo njia zote. Filosofia ni kitu kizuri katika kuimarisha imani. Hata mimi nisingekuwa imara kama nilivyo katika imani (Ukweli) bila kuzijua falsafa na mantiki.
Ina kazi yake. Kubwa tu hasa katika dunia ya leo ambayo tayari inazo elimu nyingi. Hatuwezi kutegemea kujua kwa 'inocence' ya ujinga, lazma na inabidi akili itumike ili kurudi mwanzo na kupafaidi zaidi.
 
Chanzo cha ulimwengu kujulikana kilihitaji ufunuo.
Safi kabisa maana yake hakuna haja ya Falsafa kujua uhakika wa mambo wala uhalisia, hili mpaka kwenye mengine.

Mfano kwetu sisi Kuna "Elimu ya uhakiki wa habari" ukitaka kujua Elimu Ina miujiza yake basi ni kwenye elimu hii, mpaka huwa najiuliza hivi mfano Elimu hii ingekuwa imejengeka kwenye misingi ya logic au Falsafa hivi tungeujua ukweli wa mambo kweli kama ulivyo ? Weka nukta hapa.
 
This act is called philosophy.
Hapa unarudia kosa lile lile. Huwezi kuupata ukweli kupitia Falsafa labda kama Falsafa huijui. Tuachane na suala la Chanzo Cha ulimwengu ambalo umekiri ya kuwa lilihitaji ufunuo, na walio jaribu kuufunua ukweli walikosea.

Naomba utumie Falsafa au Logic kujua kesho yako au kujua mambo kabla ya Uhuru.

Kinyume chake Falsafa itakuwa haina maana tena.
 
Wewe Kisai umekuwa fiti zaidi kuuelewa ukweli ni kwa sababu ya kutumia hizo njia zote. Filosofia ni kitu kizuri katika kuimarisha imani. Hata mimi nisingekuwa imara kama nilivyo katika imani (Ukweli) bila kuzijua falsafa na mantiki.
Ina kazi yake. Kubwa tu hasa katika dunia ya leo ambayo tayari inazo elimu nyingi. Hatuwezi kutegemea kujua kwa 'inocence' ya ujinga, lazma na inabidi akili itumike ili kurudi mwanzo na kupafaidi zaidi.
Hapa twende kwa mifano zaidi usiwe kama Hawa Wakana Mungu wasio gusa hoja ya msingi.

Unaweza kunipa au kuonyesha ukweli ambao umefukiwa na Falsafa au Falsafa imekusaidia nini katika kuujia ukweli ?
 
Safi kabisa maana yake hakuna haja ya Falsafa kujua uhakika wa mambo wala uhalisia, hili mpaka kwenye mengine.

Mfano kwetu sisi Kuna "Elimu ya uhakiki wa habari" ukitaka kujua Elimu Ina miujiza yake basi ni kwenye elimu hii, mpaka huwa najiuliza hivi mfano Elimu hii ingekuwa imejengeka kwenye misingi ya logic au Falsafa hivi tungeujua ukweli wa mambo kweli kama ulivyo ? Weka nukta hapa.
Kungekuwa hakuna haja ya falsafa na mantiki kama tungekuwa tunapokea mafunuo kila siku na katika kila kitu.

Lakini wewe ni shahidi, hakuna mtume yeyote aliyeleta ujumbe na tukapokea kama ulivyo. Na pia jumbe nyingi tu zilihitaji watu waelekezwe kwamba hii ni hii na inahusiana hivi na hiki na kile, kwa hiyo ishi hivi na ndugu na ndiyo njia sahihi. Hiyo ni sehemu ya falsafa uhusuano baina ya kweli.

Mfano ufunuo ukisema 'una roho' baada ya hapo falsafa itakusaidia kujua roho na mbingu sio physical. Kwa hiyo mambo mengine yafanyike kiroho hata kama physically utaikosa mantiki yake. Lakini yafanyike hivi bila kuathiri vibaya physical world. Mi nnaona zote hizo ni sehemu ya falsafa. Inatusaidia kuufikia na kuuishi ukweli.
 
Siyo kweli sema hivi hukijui Kiswahili vizuri. Kila lugha inajitosheleza kulingana na haja.
Nilishindwa kutofautisha fact na truth kwa kiswahili. Maybe ni mm tu sijui, au harakaharaka sikukumbuka. Whatever sio cha maana sana
 
Kungekuwa hakuna haja ya falsafa na mantiki kama tungekuwa tunapokea mafunuo kila siku na katika kila kitu.
Safi kabisa, bila shaka Mimi na wewe tutaelewena. Hakuna haja ya Falsafa na Mantiki sababu jambo limeshakamlika. Mfano katika imani yetu sisi Waislamu tunaambiwa dini imekamilika. Maana ya kitu kitu kilichokamilika ni kuwa ukiongeza kitu juu yake una kiharibu na ukipinguza kadhalika unaharibu. Kwahiyo kilicho bakia kwetu sisi ni kutumia akili yetu katika kufata mafunuo na kutafakari basi.
 
Lakini wewe ni shahidi, hakuna mtume yeyote aliyeleta ujumbe na tukapokea kama ulivyo. Na pia jumbe nyingi tu zilihitaji watu waelekezwe kwamba hii ni hii na inahusiana hivi na hiki na kile, kwa hiyo ishi hivi na ndugu na ndiyo njia sahihi. Hiyo ni sehemu ya falsafa uhusuano baina ya kweli.
Sahihi kabisa. Lakini wale walikuwa wanapatia katika kufikiri, na watu hao hawakumjua Plato wala Homeri wala Thales wala Anaksimenesi wala Anaksimanda wala Zeno wala Demokritus wala wala ...

Labda hatuelewani sehemu hii, unakubali Falsafa ni fani yaani elimu pweke ? Kama unakubali maana yake Inauanzilishi wake, Ina misingi kwayo ikafanya Falsafa isiwei Fizikia wala isiwe Kemia wala isiwe Hesabu. Sasa tumia hiyo Falsafa kama fani kuonyesha umuhimu wake. Kama unashindwa kufanya hivyo maana yake Falsafa ni Sanaa tu ya kucheza na maneno na haina faida yoyote zaidi ya kuwafanya watu wawe wajinga na wavivu wa kufikiri katikw uhalisia.
 
Safi kabisa, bila shaka Mimi na wewe tutaelewena. Hakuna haja ya Falsafa na Mantiki sababu jambo limeshakamlika. Mfano katika imani yetu sisi Waislamu tunaambiwa dini imekamilika. Maana ya kitu kitu kilichokamilika ni kuwa ukiongeza kitu juu yake una kiharibu na ukipinguza kadhalika unaharibu. Kwahiyo kilicho bakia kwetu sisi ni kutumia akili yetu katika kufata mafunuo na kutafakari basi.
Walishasemaga 'Truth (just like beauty too) is best adorned when unadorned'

Mimi suala lolote linalotumia akili kutafakari kuhusu vipande vya ukweli ili kuviunganisha na kuifaidi ile maana ya hivyo viukweli ili kujenga ukweli mzima nnaona ni falsafa na mantiki tayari.

Sasa utaniambiaje havina kazi?
 
Mfano ufunuo ukisema 'una roho' baada ya hapo falsafa itakusaidia kujua roho na mbingu sio physical. Kwa hiyo mambo mengine yafanyike kiroho hata kama physically utaikosa mantiki yake. Lakini yafanyike hivi bila kuathiri vibaya physical world. Mi nnaona zote hizo ni sehemu ya falsafa. Inatusaidia kuufikia na kuuishi ukweli.
Hapana hii sawa sababu Ufunuo unapo sema una roho unakuelezea roho ni nini, na nini hatima yake kwahiyo hapo hapo unajua kutokana na sifa anuai zilizo tajwa na ufunuo Roho si jiwe roho mwili. Labda ufunuo unao ujua wewe haujaelezea kuumbwa kwa ulimwengu na wanadamu. Roho hupulizwa akili tu ishajua roho si kitu Cha kushikika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom