Phillip Mulugo ajibu tuhuma za kuchakachua

Phillip Mulugo ajibu tuhuma za kuchakachua

Ukweli ni kwamba,ndugu Amim Agustino(naibu waziri) ametumia majina ya watu wawili tofauti kama ifuatavyo.Alitumia jina na cheti cha Dick Aron Mulungu(bado yupo hai,Mwalimu pale chuoni Mkwawa-Iringa) ili ajipatie ajira katika shule ya sekondari Southern highland,na kwa sasa anatumia jina la mtu mwingine aliyekwishafariki,marehemu Philipo Mulugo. Tunasubiri go ahead tu,tutatoa visibitisho vya kifo cha marehemu Philipo Mulugo.

Shukran.......Mkuu hakuna cha kusubiri "go ahead".................wee nenda ukatuletee picha za Kaburi...au angalau msibani........
 
Nasikia Mulugo halisi ni headmaster wa shule moja pale Morogoro. Utata mtupu!
 
Nasisitiza tena,ndugu Amim Agustino(naibu waziri wa elimu),anatumia cheti na jina la hayati Philipo Mulugo,kama anabisha aje akanushe,akikimbilia mahakamani,sisi tutakimbilia lilipo kaburi la hayati Philipo Mulugo.

Huyo 'original' Philipo Mulugo alikufa lini, na alikuwa na umri gani?
 
angekua baba ako ungemfuatilia hivi.. mwacheni jamani.. ni wakati wake subirini wenu.
 
Mkuu are you serious?

Jambo la naibu waziri wa Elimu Tanzania kutumia jina la mtu mwingine ni kashfa kubwa.Nashauri aachie ngazi.Atake asitake ngoma jinogile atatoka tu hata kama boss wake atamtetea.Ndio maana elimu Tanzania inashuka kila uchwao.Kwa nini tunacheza na elimu kiasi hiki.Si kweli kwamba kufoji ni kosa la jinai?
 
Mambo mengine yanakera sana....

Ndiyo maana hii nchi ipo kama haipo!!
Kama JK ameweza kumteuà naibu waziri wa elimu kihiyo sasa tutaanza kumwamini Tundu Lissu alipodai JK ameteua majaji vihiyo!! TZ as a country is among. the seven wonders of the world!!
 
Nilibahatika kumpata naibu waziri wa Elimu kwenye simu na kumuuliza kuhusu swala la Elimu yake na kuhusu jina lake Hamini badala ya Phillip. Kuhusu swala la elimu yake amesema kuwa hajachakachua chochote na kama kuna yeyote ana shaka na elimu yake basi aende chuo kikuu cha open university atapata majibu yote, na kuhusu swala la jina alisema kuwa kwa hivi sasa yuko njiani anasafiri kwahiyo asingeliweza kulijibu kwa maana hayuko ofisini mpaka atakapofika ofisini jumatatu. Kwahiyo jamani tukaeni mkao wa kula kusikia kutoka kwa mheshimiwa.
mbona mnamsakama huyu kijana wa watu amewakosea nini?Mwacheni afanye kazi ya kuwahudumia watanzania mtamwandamampaka atakosa ujasiri wa kufanya kazi huu ni uonevu kwa kijana mstaarabu kama huyu
 
mbona mnamsakama huyu kijana wa watu amewakosea nini?Mwacheni afanye kazi ya kuwahudumia watanzania mtamwandamampaka atakosa ujasiri wa kufanya kazi huu ni uonevu kwa kijana mstaarabu kama huyu

Afanye kazi gani Kilaza huyu!!!.....wewe unaona sahihi dhamana ya elimu kushikwa na mtu asiyejua hata Muungano uliozaa JMT imetokana na nchi zipi!!!........huyo ndio unataka akafundishe mtoto wako?!.....mtu/Waziri anaulizwa jina lako nani.......anasema subiri mpaka afike ofisini!!........Waziri anajiita Mwalimu wakati hajawahi somea huo ualimu....wewe unaona sawa.....

......kama yeye ni mstaarabu basi aweke elimu yake na majina yake kwa uwazi....otherwise mchukue nenda naye ukanywe naye chai..........
 
Nilibahatika kumpata naibu waziri wa Elimu kwenye simu na kumuuliza kuhusu swala la Elimu yake na kuhusu jina lake Hamini badala ya Phillip. Kuhusu swala la elimu yake amesema kuwa hajachakachua chochote na kama kuna yeyote ana shaka na elimu yake basi aende chuo kikuu cha open university atapata majibu yote, na kuhusu swala la jina alisema kuwa kwa hivi sasa yuko njiani anasafiri kwahiyo asingeliweza kulijibu kwa maana hayuko ofisini mpaka atakapofika ofisini jumatatu. Kwahiyo jamani tukaeni mkao wa kula kusikia kutoka kwa mheshimiwa.

Kwa hiyo anasubiri afundishwe jinsi ya kujibu. Jina ni swala lake binafsi si lazima kujibu awe ofisini.
 
Nilibahatika kumpata naibu waziri wa Elimu kwenye simu na kumuuliza kuhusu swala la Elimu yake na kuhusu jina lake Hamini badala ya Phillip. Kuhusu swala la elimu yake amesema kuwa hajachakachua chochote na kama kuna yeyote ana shaka na elimu yake basi aende chuo kikuu cha open university atapata majibu yote, na kuhusu swala la jina alisema kuwa kwa hivi sasa yuko njiani anasafiri kwahiyo asingeliweza kulijibu kwa maana hayuko ofisini mpaka atakapofika ofisini jumatatu. Kwahiyo jamani tukaeni mkao wa kula kusikia kutoka kwa mheshimiwa.

Haina haja ya Kwenda Open University , Tuanzie pale aliposoma darasa la kwanza, then Secondari, harafu tucompare na hizo za OUT.
 
Jamani waungwana atajibu nini na wakati jibu liko wazi? Hana la kujibu huyo na bado mwingine anaetumia jina la kuchakachua MWIGULU NCHEMBA
 
ili nishangaza sana kwani swali langu la jina lilikuwa na jawabu moja YES or NO, Swala la kufika kwanza ofisini ndio haweze kunijibu kwa kweli lilinishangaza kiasi fulani lakini let's give him the benefit of doubt.

Jina nalo limekuwa kama takwimu flani naona? sijui ungemwuliza akupe idadi ya wanafunzi walioacha shule kutokana na utoro ingekuaje hapo, (labda angekuambia nitafute June 2013 kama hili la jina amekuambia mtafute jtatu)
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu watanzania hakuna ukweli wowote juu ya hizi tuhuma. Haya mambo yanaongelewa kiushabiki na kuchafuana kisiasa tu.
Labda niwakumbushe tu kwamba, tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo 2015, kuna mengi yata semwa hapa lakini hizi ndio siasa zetu, na siku zote mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe.
Nawasihi tufanyeni kazi kwa bidii, tuachane na hizi propaganda, hazitusaidii lolote.
 
Nadhani jibu la elimu ndio huenda lingehitaji kuwa ofisini ili apitie rekodi zake vizuri kuhakikisha anachojibu kiko sahihi, cha ajabu hilo swali ndio kajibu akiwa nje ya ofisi, kisha swali rahisi la jina inakua tabu? Unaulizwa wewe ni mwanamke au mwanumme unasema unahitaji muda kujibu? Basi huenda pakawa na shida kubwa zaidi ya kuchakachua jina na ni hatari kwa elimu yetu ukizingatia nafasi aliyonayo.
 
Ndugu zangu watanzania hakuna ukweli wowote juu ya hizi tuhuma. Haya mambo yanaongelewa kiushabiki na kuchafuana kisiasa tu.
Labda niwakumbushe tu kwamba, tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo 2015, kuna mengi yata semwa hapa lakini hizi ndio siasa zetu, na siku zote mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe.
Nawasihi tufanyeni kazi kwa bidii, tuachane na hizi propaganda, hazitusaidii lolote.

Bwana Mulugu, haitoshi tu kusema kuwa hizi ni tuhuma, leta usahihi wake. Kwa nini uulizwe kuhusu jina lako udai mpaka ufike ofisini Jumatatu, hujui jina lako kwa uhakika?
Tungeweza kuamini kama hizi ni tuhuma tu kama IQ yako ingekuwa haina walakini, utendaji wako na uwezo wako wa kupambanua mambo ndio unaofanya watu wafuatilie historia yako, na kujiuliza ni namna gani nchi yetu inaweza kuongozwa na kilaza yeyote tu kama wewe.
Unafikiri kwa aibu uliyotutia Afrika Kusini, watu wengine wanatuchukuliaje watanzania? Yaani kama wewe ni naibu waziri uko vile, je wengine wapoje kwenye hiyo nchi? Msione raha tu kuitwa mawaziri, kama anayekuteua anakupa kazi nje ya uwezo wako, mwambie tu.
Wewe ulituaibisha sana na unaendelea kuthibitisha ukilaza wako kila siku.... kuwa mwungwana tu jiuzuru utaonekana mjanja. Hata huo ujasiri wa kuongea na walimu sijui unautolea wapi, kwa taarifa yako ukiwa mbele yao wanasema hebu cheki kilaza huyu anatuambia nini sasa?
 
angekuwa ameulizwa na bwana mkubwa angejibu hta kma yuko bar
 
Back
Top Bottom