Philip Mpango ana anything special?

Philip Mpango ana anything special?

Ww nae sio lazima mtu awe mchumi ndio ajue budget ni mbovu kuna vitu basic katika uchumi ambavyo mtu anaweza akaelewa sio lazima awe mbobevu kwenye uchumi
Kwaiyoo ukisikia bajet mpaka uwe mchumi hii nchii ni tatizo sana
Kwaiyoo wabunge wote wanajadili bajet wachumiii
Tunasafari ndefuu sana
 
Ni kama strategy ya serikali kwenye bajeti hii ni kuongeza makusanyo ya kodi na kubana matumizi tu. Hakuna strategy ya maana kwenye growth.
 
Ana elimu ya madesa he is not creative and I don't think Kama ata survive for a long time within that ministry.
 
Na hapo ndipo tatizo lilipo, na hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya sisi Waafrika na jamii nyingine, jamii nyingine kama jambo halifahamu atakwambia siwezi kuongelea kwa sababu sifahamu lkn sisi ni wataalamu kila kitu, nitakupa mfano wakati STRABAG wanajenga DART kila mtu alikuwa mtalaamu wa kukosoa mtu hata siyo engineer hata kuandika neno lenyewe hawezi lkn ni mtalaamu wa kukosoa DART kwamba umekosewa sijui mabasi hayawezi kupishana blah blah, mradi uliodesigniwa na na Wataalamu wa Kimataifa na kuidhinishwa na Benki ya Dunia ndiyo wakatoa fedha lkn mtu anajifanya yeye ndiyo anajua kwamba umekosewa, na wale woote waliotoa fedha Benki ya Dunia ni wajinga ila yeye ndiyo anajua zaidi, leo hii hao hao ndiyo wa kwanza kukimbilia mabasi ya DART, na hapo ndipo tatizo kubwa lilipo ni shida ya intelligence tu, ni mtu mwenye intelligence ndogo ndiyo huongelea mambo ya kitalaamu ambayo hana ujuzi nao yaani siyo fani yake ...
Hili la DART nakuunga mkono. Waliibuka structural/design engineers wengi jf, kila mtu akisema mradi ni big failure. Lakini mwisho wa siku we've seen one of the best design na structural set-up ambayo kama ingekuwa implemented Dar yote wengi wangeifurahia.

Mimi sipingi kukosia, coz that's the only way utamuonyesha mtu wapi amekosea, but kama mtu hajui kitu, ni vyema kukaa kimya.
 
Intension yako inajulikana tangu watu wabadili gia angani na wewe umebadili gia angani (unajaribu kuzunguka tu)
Its clear tangu JPM ameingia ikulu kila anachofanya lazima uanzishe maada kupinga,ulianza na Prof Muhongo,
Bahati mbaya Muhongo ni one of the best cabinet members. Bahati mbaya sana[emoji12] [emoji12]
 
Mimi nadhani tupige kimya tu. Tuachane kabisa na haya mambo ya kuikosoa serikali, hiyo kazi ya ukosoaji itafanywa viziri zaidi na akina Lizaboni na akina Faizafox kuliko tufanyavyo sisi.
Ni suala la muda tu.
 
Let's wait, give enough time and wait for the results
 
Wapinzani walipoteza nafasi ya kuleta budget mbadala.

Nina maana ya budget mbadala sio bla bla za kisiasa all the time. Ingekuwa na figures zake kabisa. Vyanzo vya mapato, vyanzo vipya, uwiano wa fedha ya matumizi ya kawaida na ile ya maendeleo. Vipaumbele vyao kama ni elimu afya nk.

What a lost opportunity!
 
Ukawa wanatafuta pa kutokea. Polepole keshaingia dar. Sasa hapa tunataka kazi tu.

Hizo mbwembwe zenu pelekeni moshi.
jadili hoja ilioko mezani kama hunachakuchangia pita kimya,fananisha akili yako ndogo na mambo yaliyo anikwa hapo alafu ujipime
 
Ni kama tunafukuza watalii sasa

Mfanyabiashara asiye mjuvi huitafuta faida kubwa kwa kuongeza bei, matokeo ni kukimbiza wateja.

Mfanyabiashara mjuvi huongeza varieties za bidhaa, matokeo yake turn over huongezeka na mapato huongezeka.

Mimi nilichojiuliza, najiuliza na nitaendelea kujiuliza: HIVI MAPATO YA NCHI HUTOKANA NA KODI TU?
 
Mimi nimejiuliza anapokea 'orders' kutoka kwa Magu bajeti iweje?
au ni yeye yuko full in charge?

manake kuna vitu ni aibu kwa mtu kama yeye kuvleta kwenye bajeti na kavileta...
The Boss unaweza kufafanua kidogo hapo? Najua wewe ni mpinzani wa Rais Magufuli.
 
Wapinzani walipoteza nafasi ya kuleta budget mbadala.

Nina maana ya budget mbadala sio bla bla za kisiasa all the time. Ingekuwa na figures zake kabisa. Vyanzo vya mapato, vyanzo vipya, uwiano wa fedha ya matumizi ya kawaida na ile ya maendeleo. Vipaumbele vyao kama ni elimu afya nk.

What a lost opportunity!

Bajeti kivuli huwa inakuwa implemented? Au na wewe unaokoteza jambo la kusema?
 
Hawa jamaa ni wasomi sio wanasiasa Tanzania mtu akishakuwa na Phd their qualification entitles them to any governmental role without having necessary work experience.

Mwanasiasa anajua wananchi wanaishi vipi anapozunguka huko kwenye kuomba kura anajionea shinda zenyewe, lakini mawaziri kama akina Mpango wakisikia kuna kulipa madeni ya serikari (asilimia kubwa ya mapato wanatumia kufanya hivyo bila ya kujali huduma za jamii), wakiambiwa kukuza viwanda basi wanakuja na mawazo ya ajabu kulazimisha hayo mambo yanatokea bila ya kujali athari za jamii, wakitaka kuongeza mapato wanakamua kila kona bila kujali jinsi gani jamii inaumia; leo wanaolalamika shida ni wale wale serikari inayolenga kuwasaidia.

Kikubwa kwa watu kama bwana Mpango ni kumridhisha raisi kwa mwonekano wanalenga kufuata maagizo wakati aina ya utekelezaji wao unawaumiza wananchi kwa namna nyingine na kuwaacha worst off kuliko walivyo wakuta. Leo hii kuanzia raisi na mawaziri wote wa maendeleo; uchumi, kilimo, viwanda, utalii na uchukuzi wanategemea either direct foreign investment or other purchases/services as part of income to help their sectors. Wakati huo nchi ina sera ya kulazimisha growing businesses to sell their shares to the public, mwingine anadai atutaki watalii maskini, mwingine kodi kila sehemu. All those measures are put off to a majority of businesses and tourists in the world of competition.

Ndio unajiuliza hivi hawa jamaa wanadhani tourist destination ni Tanzania tu or nchi pekee inayohitaji FDI ni sisi tu kiasi kwamba atuhitaji kuwa na sera za ushindani kuwasaidia watanzania; kwenye vichwa vyao inaonekana kuna assumption za kwamba Tanzania is a special country so may be it will receive special treatment. Facts ni kwamba Tanzania is a special country indeed political stable, ina kila aina ya malighafi, imebarikiwa vivutio vya utalii wa nchi kavu na baharini ambavyo vingi duniani havipo, tatizo ni hawa tunaowaita Phd ni watu ovyo kweli wengi wao. As days go this guy Mpango is becoming more of a liability than an asset to the government to me he has already showcased his limited creativity in planning.
 
Ana elimu ya madesa he is not creative and I don't think Kama ata survive for a long time within that ministry.
Creativity ni janga kwa nchi hii, watanzania wengi tunaelimu ya kukariri tu, vyeti vinangaa lakini kudeliver ni sifuri.
 
Hapa kazi tu !!!!
Hiyo slogan (HAPA KAZI TU) inatumika ndivyo sivyo ... punda anafanya kazi sana lakini maisha yake magumu mmno.

Nafikiri anaweka wasioweza kazi ili awatumbue na kujiongezea idadi ya watu alowatumbua akiwa madarakani.
 
Tatizo sisi WatanZania ni watalaamu kila kitu, hata kama jambo hatulifahamu na hatuna utalaamu nao kwa sababu siyo fani yetu lkn bado unataka kujifanya watalaamu na wachambuzi, jifunzeni kwa Wazungu ambao siku zote mnajaribu kuwaiga ingawaje hamuwaelewi, Mzungu kama jambo halifahamu atakwambia ,,I can not talk about/ discuss about that, because I have no idea ..." sasa wewe nina uhakika siyo Mchumi na wala abc za Uchumi achilia mbali hata jinsi Bajeti ya nchi inavyotengenezwa lkn unakuja hapa unataka kuleta uchambuzi wa Kiuchumi, kwa nini tuko hivi?

Waziri Mpango(PhD) ni mtalaamu wa uchumi, amefanya kazi mpaka IMF alikuwa mchumi wa IMF, kwa nini usimpe muda afanye anavyonuia kufanya halafu uje umuhukumu kwa matokeo ya kazi yake?
Bajeti hata haijaanza kutekelezwa lkn tayari unakuja na ukosoaji kwamba ameshindwa wkt wewe hata abc za uchumi hauna, hii ni ajabu sana, una haraka gani? Ni Waafrika tu ndiyo tuko hivi sijui ni kwa nini?
kuna nyakati unaweka kichaa pembeni na kutoa point ambazo hata kama sikupendi lakini pointi zinakuwa zimebamba ile mbaya.

hongera kwa hili na wazo lako naamini watalifanyia kazi waleta uzi mfu hawa
 
Tatizo sisi WatanZania ni watalaamu kila kitu, hata kama jambo hatulifahamu na hatuna utalaamu nao kwa sababu siyo fani yetu lkn bado unataka kujifanya watalaamu na wachambuzi, jifunzeni kwa Wazungu ambao siku zote mnajaribu kuwaiga ingawaje hamuwaelewi, Mzungu kama jambo halifahamu atakwambia ,,I can not talk about/ discuss about that, because I have no idea ..." sasa wewe nina uhakika siyo Mchumi na wala abc za Uchumi achilia mbali hata jinsi Bajeti ya nchi inavyotengenezwa lkn unakuja hapa unataka kuleta uchambuzi wa Kiuchumi, kwa nini tuko hivi?

Waziri Mpango(PhD) ni mtalaamu wa uchumi, amefanya kazi mpaka IMF alikuwa mchumi wa IMF, kwa nini usimpe muda afanye anavyonuia kufanya halafu uje umuhukumu kwa matokeo ya kazi yake?
Bajeti hata haijaanza kutekelezwa lkn tayari unakuja na ukosoaji kwamba ameshindwa wkt wewe hata abc za uchumi hauna, hii ni ajabu sana, una haraka gani? Ni Waafrika tu ndiyo tuko hivi sijui ni kwa nini?
Mawazo ya mtu layman ni ya muhimu pia kwani serikali inapata picha kwamba wananchi wa kawaida wanaionaje na wasomi wanaionaje, wachumi wetu wengi (sio Waziri Mpango) yaani hao unaowaona wanafaa kuzungumzia budget wengi wao wanazungumzia nadharia tu za uchumi lakini machungu na practical experience ya uchumi mwananchi wa kawaida kama The Boss anaweza akaizungumzia vizuri kuliko hata huyo msomi japokuwa hataweka terms za kiuchumi sijui
 
Kwa idea ya 40% development hiyo ni innovation tayari. Lakini pia wamekata sana kwenye matumizi ya anasa kama ununuzi wa magari, furniture, per diems na posho. Lakini pia kwa ambition ya kuongeza trilion karibu nane kwenye bajeti ilikuwa lazima kuongeza baadhi ya kodi. Nadhani tumpe muda tuone ambitions zake kama zitafikiwa halafu ndio tumhukumu at least May mwakani. Binafsi nampongeza kwa kujaribu 40% development, zamani bajeti zilikuwa ni matumizi tu na utekelezaji unakuta maendeleo less than 10%
Kwa taarifa yako hakuna hata mwaka mmoja fedha za maendeleo wala za matumizi ya kawaida zimewahi kutolewa katika wizara zote kama zilivyo katika bajeti ukiondoa bajeti ya Ikulu!

Kwa kifupi hizo Tril.29.5 ni za kwenye makaratasi tu na kamwe serikali haiwezi kuzipata!!
 
Back
Top Bottom