Philip Mpango ana anything special?

Philip Mpango ana anything special?

Ww nae sio lazima mtu awe mchumi ndio ajue budget ni mbovu kuna vitu basic katika uchumi ambavyo mtu anaweza akaelewa sio lazima awe mbobevu kwenye uchumi

Na hapo ndipo tatizo lilipo, na hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya sisi Waafrika na jamii nyingine, jamii nyingine kama jambo halifahamu atakwambia siwezi kuongelea kwa sababu sifahamu lkn sisi ni wataalamu kila kitu, nitakupa mfano wakati STRABAG wanajenga DART kila mtu alikuwa mtalaamu wa kukosoa mtu hata siyo engineer hata kuandika neno lenyewe hawezi lkn ni mtalaamu wa kukosoa DART kwamba umekosewa sijui mabasi hayawezi kupishana blah blah, mradi uliodesigniwa na na Wataalamu wa Kimataifa na kuidhinishwa na Benki ya Dunia ndiyo wakatoa fedha lkn mtu anajifanya yeye ndiyo anajua kwamba umekosewa, na wale woote waliotoa fedha Benki ya Dunia ni wajinga ila yeye ndiyo anajua zaidi, leo hii hao hao ndiyo wa kwanza kukimbilia mabasi ya DART, na hapo ndipo tatizo kubwa lilipo ni shida ya intelligence tu, ni mtu mwenye intelligence ndogo ndiyo huongelea mambo ya kitalaamu ambayo hana ujuzi nao yaani siyo fani yake ...
 
Mwaka huu kukosa sera mtaongea vitu hata wananchi wa kawaida hawataki kuvisikia.

Ila shida yako hutaki kulipa kodi tu!!
 
Maamuzi yake ni ya kushangaza
Mangi vipi umezoea kukwepa kodi. Sasa hivi lazima tuwanyooshe. Mmezoea kuibia raia. Kwikwikwikwi. Kama hukushiba awamu iliyopita kipindi hiki ni kila mmoja kujipatia kipato halali.

Kwikwikwi. Mangi bana.
 
Ukawa wanatafuta pa kutokea. Polepole keshaingia dar. Sasa hapa tunataka kazi tu.

Hizo mbwembwe zenu pelekeni moshi.
Mkuu mbona hoja zipo clear kabisa, kwa nini usizijibu hizo alizotoa jamaa na sisi tusiojua tupate kufahamu na kuelemika ili kuonyesha hizo mbwembwe kama unavyodai.
 
Kweli ECONOMICS za bajeti mpya ni za kumuumiza mtu masikini kweli kweli, badala ya Serikali ku systematically kusaidia baadhi ya Sector za wanyonge kupitia Tax Incentives kwenye baadhi ya mambo wao wanakamua kodi tu, matokeo yake Small businesses zitakufa, Yaani Vifremu vilivyoibuka kama uyoga na kuwapa ahueni ya maisha Wananchi kipindi cha Kikwete vitaanza kufungwa muda si mrefu.
Watanzania walishaanza kuwa wajanja wa Ujasiriamali, lakini kwa mipango ya uchumi ya huyu Dr Mpango Watanzania watarudi kufanya vibarua tu badala ya kuown business zao.
Inaonekana Dr Mpango yuko very Impressed kukusanya Mapesa tu yaende hazina badala ya kuangalia kwa kufanya hivyo anaziumiza boashara ndogondogo na za kati kwa kiasi gani.
Chukulia mfano wa kodi ya ATM na kodi ya miamala ya M-Pesa/Tigo-Pesa, Impact yake ni watu kuendelea kupoteza muda kwenye Foleni kwenye mabenki kuchukua pesa na kufanya miamala badala ya kufanya kazi.
serikali ilitakiwa iyabane makampuni ya Simu hizi M-Pesa ziwe ni biashara za Faida Ndogo mno kwa Muamala ili ziwe Services zaidi kama ilivyokuwa imekusudiwa awali kuliko kuzijengea mazingira ya kuwa Lucrative business kwa kuzitoza makodi ambayo eventually ni Mlalahoi tu ndo atayalipa.
Kiufupi Bajeti ya Dr Mpango inamkamua ng'ombe aliyehoi badala ya kumuwezesha atoe maziwa mengi.
 
Kabla hajateua baraza la mawaziri..weghine tulishauri humu Magufuli awe makini mno
na waziri wa Fedha....atakaemteua...
Sababu waziri wa fedha na mipango ndo tunaweza kusema anakuwa in charge kwenye uchumi

Sasa Magufuli akamteua Phillip Mpango......binafsi nilijizuia kusema chochote hadi alete bajeti
yake ya kwanza tuione

Baada ya kuleta hii bajeti ambayo binafsi naiona ni bajeti ya kuongeza umasikini
kwa kuongeza kodi kila sehemu na kodi zingine za ajabu ...kama vile kuwakomoa watu
na kuinyima serikali mapato....mfano ile ya wanaotaka kuweka majina kwenye magari

kutoka milioni 5 hadi 10 kiasi karibu kila alieweka mwanzo hataki tena...wakati wangepunguza
si ajabu watu maarufu zaidi wangejitokeza na serikali kupata zaidi.....

Achilia mbali ile sheria ya ajabu na aibu ya kutaka kumfunga mtu asipodai risiti......

Na mengi tu ya kushangaza...kodi ya gesi kuongezwa
ushuru wa mbuga za wanyama kuongezwa na kadhalika....

Swali ambalo bado najiuliza ni je huyu Philip Mpango ni mtu sahihi 'ku run the economy'?

Je ana chochote special kipya ambacho tunaweza sema atasaidia kuitoa hii nchi na kuipeleka mbali?
hasa kwa masuala ya uchumi?

Binafsi namuona 'hamna kitu'....ubunifu hakuna.....na sitashangaa uchumi wa nchi ukiyumba
zaidi kwa maamuzi yake......

Bajeti yake ni kama 'one of the worst'
hakuna 'new measures'
hakuna ubunifu mpya
hakuna mbinu za ku boost 'new economy'

Je nyinyi mnamtazamaje huyu Philip Mpango?
Hivi ulitegemea Magufuli ataifanya Tanzania iwe kama Marekani ? Punguza propaganda zisizokuwa na mantiki,ulikuwa ni mmoja ya watu waliokuwa wanaponda serikali ya JK(now kina Meghji, Mkulo,Mgimwa,Sada Mkuya wanaonekana bora) ,Unachoshangaza watu siku hizi umekuwa ndio unasifia kila alichofanya JK na kuponda alichofanya Magufuli
 
Hapa mada inamhusu Philip Mpango
wewe unakuja na JK na Mgufuli
soma uelewe
 
Mkuu mbona hoja zipo clear kabisa, kwa nini usizijibu hizo alizotoa jamaa na sisi tusiojua tupate kufahamu na kuelemika ili kuonyesha hizo mbwembwe kama unavyodai.
Wewe rais wa moyo wako ni lowasa na upo yupo Silinde waziri kivuri. Nenda kamuulize huyo na rais wa mioyo yenu.

Hapa sasa hivi ni kazi tu. Hizo bra bra peleka moshi na hai.

Mangi vipo? Kodi lazima kulipa sasa hivi zama zimebadilika. Acha kuiba wewe utaumizwa. Jipatie kipato halali. Mambo mengine ni mbwe mbwe tu. Ila kusema ukweli mmekabwa. Sio mda mrefu magonjwa ya shinikizo la damu yatawaua.

Na vijana wengi wa ccm sasa wamemwagwa kuwa wakuu wa wilaya. Watawanyoosha mpaka mkae.
 
Namuona huyu jamaa kama yuko too bookish.

Mipango mingi anayoiweka iko theoretically good, lakini anasahau kuwa lazima mipango hiyo itestiwe kwanza kama practically inaweza kuwa applicable.

Ni msomi mzuri na uzalendo wake ni mzuri sana, tatizo he is too bookish.
 
Kabla hajateua baraza la mawaziri..weghine tulishauri humu Magufuli awe makini mno
na waziri wa Fedha....atakaemteua...
Sababu waziri wa fedha na mipango ndo tunaweza kusema anakuwa in charge kwenye uchumi

Sasa Magufuli akamteua Phillip Mpango......binafsi nilijizuia kusema chochote hadi alete bajeti
yake ya kwanza tuione

Baada ya kuleta hii bajeti ambayo binafsi naiona ni bajeti ya kuongeza umasikini
kwa kuongeza kodi kila sehemu na kodi zingine za ajabu ...kama vile kuwakomoa watu
na kuinyima serikali mapato....mfano ile ya wanaotaka kuweka majina kwenye magari

kutoka milioni 5 hadi 10 kiasi karibu kila alieweka mwanzo hataki tena...wakati wangepunguza
si ajabu watu maarufu zaidi wangejitokeza na serikali kupata zaidi.....

Achilia mbali ile sheria ya ajabu na aibu ya kutaka kumfunga mtu asipodai risiti......

Na mengi tu ya kushangaza...kodi ya gesi kuongezwa
ushuru wa mbuga za wanyama kuongezwa na kadhalika....

Swali ambalo bado najiuliza ni je huyu Philip Mpango ni mtu sahihi 'ku run the economy'?

Je ana chochote special kipya ambacho tunaweza sema atasaidia kuitoa hii nchi na kuipeleka mbali?
hasa kwa masuala ya uchumi?

Binafsi namuona 'hamna kitu'....ubunifu hakuna.....na sitashangaa uchumi wa nchi ukiyumba
zaidi kwa maamuzi yake......

Bajeti yake ni kama 'one of the worst'
hakuna 'new measures'
hakuna ubunifu mpya
hakuna mbinu za ku boost 'new economy'

Je nyinyi mnamtazamaje huyu Philip Mpango?

naamini katika system, mpango hafanyi kazi peke yake. pia hiyo bajeti kila waziri aliandaa bajeti yake. tuache kuatack mtu, tujadili content.
 
Hapa mada inamhusu Philip Mpango
wewe unakuja na JK na Mgufuli
soma uelewe
Intension yako inajulikana tangu watu wabadili gia angani na wewe umebadili gia angani (unajaribu kuzunguka tu)
Its clear tangu JPM ameingia ikulu kila anachofanya lazima uanzishe maada kupinga,ulianza na Prof Muhongo,
 
Namuona huyu jamaa kama yuko too bookish.

Mipango mingi anayoiweka iko theoretically good, lakini anasahau kuwa lazima mipango hiyo itestiwe kwanza kama practically inaweza kuwa applicable.

Ni msomi mzuri na uzalendo wake ni mzuri sana, tatizo he is too bookish.
Nyie mpo na mawaziri wenu wa mioyo yenu. Waliweka mpira kwapani wakakimbia bunge na kuanza kujiziba makaratasi midomoni.

Hapa sasa unaleta ni upuuzi tu.
Nakuona kama mtu fulani ambae hafikirii vizuri. Mda mlikuwa nao tangi mwezi wa kwanza kupeleka mawazo yenu.

Design ya budget ilitolewa January. Mkaweka mpira kwapani. Sasa hivi kaa kimya. Uache kuropoka ropoka. Sisi hapa kazi tu. Na kama hamtaki basi serikali itatekeleza sehemu ya majimbo ya wabunge wanaotaka maendeleo.
Pyuuuuuuuu!!!
 
Tumeumia. Hawezi chochote.

Kwanza kalazimishwa kuwa waziri, hana wito wa utumishi wa umma na hajali. Alikuwa world bank, haraka haraka akaenda Ikulu, TRA halafu Hazina. Sijui hata kama anajua bei ya kilo ya unga au nauli ya dala dala, hayamhusu.

Na huyu ndio alichukuliwa maalum, hakuwa elected jimboni, ungedhani ni mtu very special. Hadi gesi nayo anapandisha kodi. He is just too old to grasp hayo mambo yenu ya gas and the new economy!

Nchi za wenzetu mpaka upewe kuandika bajeti ya nchi ujue huko nyuma usha bump heads na wachumi, ushaandika ma peer reviewed papers yenye ma idea yako ya ku spur the economy na ma idea mengine yalishakuwa adopted na yaka work.

Huyu wa kwetu, challenge aliyopata na feedback aliyotumia kurekebisha budget draft yake ameipata kwa Mbunge wa Mtera, Kibajaji, na Mbunge wa Ulanga, ambae alikuwa very prominent kwenye budget debates, huyu aliyesema mbunge mwanamke wa CHADEMA anamtaka.
 
Dr. Mpango ni bomu. Si yeye peke yake, na hata naibu wake. Sijaona bajeti ovyoo kama hii. Rais ameshaziba mianya ya kukwepa kodi, sasa yeye badala ya kupunguza kodi ili wengi walipe yeye anaongeza! Ajabu sana!Principles of good taxation zote kasahau!!! Badala ya kupanua wigo wa kodi-tax base, mchumi wetu Mpango kang'ang'ana kucheza na tax rate!!!! Kwa mtindo huu, si ajabu tukashuhudia tax avoidance kila eneo linalowezekana, itakaposhindikana, purchases zitapungua sana. Kumbuka kuwa tax evasion imeshadhibitiwa na Rais mwenyewe. Anayejipenda hatacheza na tax evasion bali avoidance. Kwa upande wa bandari, si ajabu imports zikahamia bandari za nchi jirani. Kwa mtindo huu, tax revenue kuongezeka Kama Dr. Mpango anavyotaka tuamini itakuwa kizungumkuti. Tusubiri tuone.
 
Wewe rais wa moyo wako ni lowasa na upo yupo Silinde waziri kivuri. Nenda kamuulize huyo na rais wa mioyo yenu.

Hapa sasa hivi ni kazi tu. Hizo bra bra peleka moshi na hai.

Mangi vipo? Kodi lazima kulipa sasa hivi zama zimebadilika. Acha kuiba wewe utaumizwa. Jipatie kipato halali. Mambo mengine ni mbwe mbwe tu. Ila kusema ukweli mmekabwa. Sio mda mrefu magonjwa ya shinikizo la damu yatawaua.

Na vijana wengi wa ccm sasa wamemwagwa kuwa wakuu wa wilaya. Watawanyoosha mpaka mkae.
Ok Mkuu nimekuelewa yaishee. aiseeeh.
 
Intension yako inajulikana tangu watu wabadili gia angani na wewe umebadili gia angani (unajaribu kuzunguka tu)
Its clear tangu JPM ameingia ikulu kila anachofanya lazima uanzishe maada kupinga,ulianza na Prof Muhongo,
Huyu ni mpuuzi tu. Ndio wale waliokuwa wanajidai eti piga ua rais lazima atoke kaskazini. Huu ni upuuzi uliopitiliza. Ananishangaza sana huyu jamaa. Ni mtu mzima na watoto halafu anajitoa ufahamu.
 
Nyie mpo na mawaziri wenu wa mioyo yenu. Waliweka mpira kwapani wakakimbia bunge na kuanza kujiziba makaratasi midomoni.

Hapa sasa unaleta ni upuuzi tu.
Nakuona kama mtu fulani ambae hafirii vizuri. Mda mlikuwa nao tangi mwezi wa kwanza kupeleka mawazo yenu.

Design ya budget ilitolewa January. Mkaweka mpira kwapani. Sasa hivi kaa kimya. Uache kuropoka ropoka. Sisi hapa kazi tu. Na kama hamtaki basi serikali itatekeleza sehemu ya majimbo ya wabunge wanaotaka maendeleo.
Pyuuuuuuuu!!!
Dogo tulia, acha mihemko ujibu hoja.

Jifunze kujenga hoja na kuitetea, au kupangua hoja kwa hoja.
 
40% ya bajeti kwenda kwenye maendeleo hili ni jipya. Kuna watu wanalalamikia kodi. Tanzania bado makusanyo ya kodi ni % ndogo sana ya GDP hata ukilinganisha na majirani zetu. kodi kwenye mafuta wala road license haijaongezwa na hii ni mara ya Kwanza. Hivi kodi mnazolalamikia ni zip?? Upinzani enzi hizi utakuwa mgumu sana.

Kodi kwenye utalii inapigiwa kelele! Watu wamezoea kufanya biashara bila kodi. Strategy ya Tanzania kwenye utalii si low price. Tanzania inatengeneza fedha nyingi kwenye utalii kuliko Kenya. Siku zote watalii wanalipa zaidi kwenye attractions za Tanzania kuliko za Kenya. Tanzania target ni high value tourists who pay more and this has proved successful na inasaidia conservation. Wanaopigia kelele VAT kwenye utalii ndo hawana jipya. Vyanzo vyote vya mapato vikiguswa mnapiga kelele halafu mkiulizwa alternative Vyanzo ni vipi?? Philip Mpango's budget is not perfect, but it is the best we have ever had in recent times.
 
Dogo wewe rais wa moyo wako lowassa. Nenda mfuate hukoo. Huu unaoleta hapa ni ushamba. Halafu eti unaniita dogo. Mtu gani mkubwa mwenye akili za kitoto hivi kama yupo primary?

Soma comment yangu vizuri halafu ujione jinsi gani ulivyo.
Pyuuuuuuuu.
teh teh teh

Narudia tena.

Dogo punguza mihemko, jifunze kujenga hoja na kuitetea hoja yako.

Pangua hoja kwa hoja achana na hizi mambo za pyuuuuuuuuuu.

Za kike hizo, jenga hoja dogo.
 
Back
Top Bottom