Philip Mpango ana anything special?

Philip Mpango ana anything special?

Mpango is more of a theoretician than a practioner; kodi yeyote katika nchi ni lazima iweze kulipika na iwe rahisi kukusanywa!! Sasa unapoongeza kodi katika kila kitu ukidhania utakusanya fedha nyingi matokeo yake ndio unakusanya kidogo kwani wananchi wanashindwa kulipa!! Mwishowe wataanza kutumia polisi kukamata wale ambao hawajalipa kodi kwani mlolongo wa kodi hautekelezeki!!


Ngoja tumkumbushe huyu Mpango kuwa kwenye TAXATION kuna concept ya UNYAMBULIKIO yaani ELASTICITY pia!!!

Si tuliambiwa huyu ni mtaalam wa kodi pia?
 
I don't believe that, mwanzo mbaya siku zote hukupa mwisho mbaya, pia poor planning results into poor output..


Tatizo ukiwabana Sana kwa maswali husema mbona anamiezi nane Tu. Kwa hiyo tumpe muda ili visingizio visiwepo
 
The Boss

I think bajeti haiandaliwi na waziri tu, yeye ni mtu wa mwisho na hata his position ni political, I would look into PS wa wizara na washauri wakuu (technical leads) wa kila kitengo hasa cha mipango na kwa kushirikiana na idara za uchumi na mipango za wizara zote kabla ya kumnyooshea vidole mpango

To me, tatizo sio Mpango, bali system nzima ya mipango, pesa na uchumi wa tanzania - shida ni uchumi, wachumi na mfumo mzima wa uchumi (macro na micro)
 
Ni mbinifu sana katika kukamua walala hoi
Tawala zote zilizopita kuanzia Utawala wa Nyerere mpaka Magu, kauli ninayoisikia ni "tukaze mkanda". Siri.kali za kugawa umasikini kwa wadanganyika. Ni wajanja wachache tu ndio wanakwapua na kufisidi rasilimali za nchi na mali za umma.
Watawala wanakuja na kauli za kisiasa, tutawashughulikia wala rushwa, tutawapeleka mahakamani mafisadi, kauli za kuwahadaa na kuwapiga changa la macho wadanganyika.

Siku ikitungwa na ikipitishwa sheria ya kupiga risasi hadharani au kuwanyonga wataotiwa hatiani wala rushwa na mafisadi ndio nitaanza kupata imani kuwa iko siku nchi hii itaanza kukaa sawa.
 
Kabla hajateua baraza la mawaziri..weghine tulishauri humu Magufuli awe makini mno na waziri wa Fedha atakaemteua.

Sababu waziri wa fedha na mipango ndo tunaweza kusema anakuwa in charge kwenye uchumi

Sasa Magufuli akamteua Phillip Mpango, binafsi nilijizuia kusema chochote hadi alete bajeti yake ya kwanza tuione

Baada ya kuleta hii bajeti ambayo binafsi naiona ni bajeti ya kuongeza umasikini.

Kwa kuongeza kodi kila sehemu na kodi zingine za ajabu ...kama vile kuwakomoa watu.

Na kuinyima serikali mapato, mfano ile ya wanaotaka kuweka majina kwenye magari

Kutoka milioni 5 hadi 10 kiasi karibu kila alieweka mwanzo hataki tena...wakati wangepunguza si ajabu watu maarufu zaidi wangejitokeza na serikali kupata zaidi.

Achilia mbali ile sheria ya ajabu na aibu ya kutaka kumfunga mtu asipodai risiti.

Na mengi tu ya kushangaza...kodi ya gesi kuongezwa.Ushuru wa mbuga za wanyama kuongezwa na kadhalika.

Swali ambalo bado najiuliza ni je huyu Philip Mpango ni mtu sahihi 'ku run the economy'?

Je, ana chochote special kipya ambacho tunaweza sema atasaidia kuitoa hii nchi na kuipeleka mbali?

Hasa kwa masuala ya uchumi?

Binafsi namuona 'hamna kitu'....ubunifu hakuna.....na sitashangaa uchumi wa nchi ukiyumba zaidi kwa maamuzi yake.

Bajeti yake ni kama 'one of the worst'
hakuna 'new measures'
hakuna ubunifu mpya
hakuna mbinu za ku boost 'new economy'

Je, nyinyi mnamtazamaje huyu Philip Mpango?
Kaka idara zote zimepwaya!
Kuna shida wataalam wetu huwa wanawaangusha viongozi waliowateua!
Watu hawatoi ushauri wa kitaalam wana swing na rizm za Mkuu!
Magufuli ana hardcore approaches ktk mambo mengi, ikiwemo jinsi ya kutumia na kupata pesa ktk kila source! Sasa yeye si mchumi, anaweza akawa na approaches zake anazoziamini Ila wenye uelewa na uchumi wanaweza wakaweka strategies zilizosahihi kulingana na principles za uchumi!
Ni sawa na issues za elimu bure, kuchangia huduma za afya sasa watu wanataka hata zile za ukimwi, etc!
Ila tuwape muda, labda wanaweza kurejea ktk their senses na kujua kuwa nafasi zao wameteuliwa kwa merits za taaluma zao, then watende Yale taaluma zao zinavyowaelekeza na sio ilani ya chama na utashi wa watu binafsi!
 
Ukawa wanatafuta pa kutokea. Polepole keshaingia dar. Sasa hapa tunataka kazi tu.

Hizo mbwembwe zenu pelekeni moshi.

Nilikuwa nakiujiuliza uchawi ni nini lakini nikisoma maoni yako,napata maana halisi ya uchawi!kuua watu ili wasitoe hoja!Wachawi hawawezi kuua hoja kwa kutoa hoja.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hivi ulitegemea Magufuli ataifanya Tanzania iwe kama Marekani ? Punguza propaganda zisizokuwa na mantiki,ulikuwa ni mmoja ya watu waliokuwa wanaponda serikali ya JK(now kina Meghji, Mkulo,Mgimwa,Sada Mkuya wanaonekana bora) ,Unachoshangaza watu siku hizi umekuwa ndio unasifia kila alichofanya JK na kuponda alichofanya Magufuli
Ubaya wa serikali ya magu haulalishi ubaya wa serikali ya jk.kila serikali ina makosa yake hata na ya nyerere ilikuwa na mazuri na mabaya, kwahiyo tulia yaliyo mabaya yasemwe.
 
yeye ndio alikuwa anahusika kuandaa mipango ya uchumi ya miaka mitano toka wakati wa awamu ya nnelakini tujiulize hiyo mipango pamoja na kuzinduliwa bungeni kwa mbwembwe imafanikiwa kivipi, ni mzuri kumsoma kimaandishi ila kiuhalisia ni mtupu kwa kifupi hana uwezo
 
Tatizo sisi WatanZania ni watalaamu kila kitu, hata kama jambo hatulifahamu na hatuna utalaamu nao kwa sababu siyo fani yetu lkn bado unataka kujifanya watalaamu na wachambuzi, jifunzeni kwa Wazungu ambao siku zote mnajaribu kuwaiga ingawaje hamuwaelewi, Mzungu kama jambo halifahamu atakwambia ,,I can not talk about/ discuss about that, because I have no idea ..." sasa wewe nina uhakika siyo Mchumi na wala abc za Uchumi achilia mbali hata jinsi Bajeti ya nchi inavyotengenezwa lkn unakuja hapa unataka kuleta uchambuzi wa Kiuchumi, kwa nini tuko hivi?

Waziri Mpango(PhD) ni mtalaamu wa uchumi, amefanya kazi mpaka IMF alikuwa mchumi wa IMF, kwa nini usimpe muda afanye anavyonuia kufanya halafu uje umuhukumu kwa matokeo ya kazi yake?
Bajeti hata haijaanza kutekelezwa lkn tayari unakuja na ukosoaji kwamba ameshindwa wkt wewe hata abc za uchumi hauna, hii ni ajabu sana, una haraka gani? Ni Waafrika tu ndiyo tuko hivi sijui ni kwa nini?

Kwanini aliondolewa IMF? Usije kuta ni mpango mbovu tu.
 
Serikali isio kusanya kodi ni ya wala rushwa-Mwl JK Nyerere.

Nyie mnapinga serikali kukusanya kodi...tunawajua agenda yenu kuanzia 2015. Mmekua watetezi wa mafisadi.
 
Magufuli akitaka economy ya nchi ikuwe kwa haraka, awaite wafanya biashara wakubwa na wadogo (wenye mafanikio) ajifungie nao Ikulu mwezi mzima na Mpango awepo kuandika notes, wakitoka hapo mpango akayafanyie kazi tu. Tutaona mabadiliko ya ukuaji uchumi wa ajabu.

Mchumi anaetegemea kuajiriwa, tena serikalini, hata siku moja hana mbinu za kuitajirisha nchi, hata iweje. Yeye sana sana atajuwa formula za hesabu na takwimu tu.

Huo ndiyo ukweli.
 
Ukawa wanatafuta pa kutokea. Polepole keshaingia dar. Sasa hapa tunataka kazi tu.

Hizo mbwembwe zenu pelekeni moshi.
Sasa hii ni mipasho, nadhani Barbarosa katoa jibu sahihi kulingana na mada, c wewe unaetuletea mipasho yako hapa.
 
Ukawa wanatafuta pa kutokea. Polepole keshaingia dar. Sasa hapa tunataka kazi tu.

Hizo mbwembwe zenu pelekeni moshi.
Ndugu umemuelewa mleta mada? au umekurupuka kwa vile katajwa Magufuli...! Ngoja nikukumbushe mleta mada ameuliza Wazir wa Fedha ana ubunifu wowote? yy amepata jibu kwamba hana ubunifu...na ametolea mfano wa Namba za Magari zenye majina ya watu badala ya 5ml ilivyokuwa Mwaka Jana mwaka huu wameweka 10ml kwa namna hii watu siwanaweza kuweka tu namba za kawaida na Serikali kukosa Mapato waliyotarajia? sasa nawewe ulitakiwa impinge kwa Hoja sio Vioja....watu wanasema hivyo sababu kama Kukurupuka kwa Serikali kumepelekea watu kununua Sukari elf 6 Pamoja na mbavu zake lkn wauza Sukari wameibuka washindi wananchi ndio wanaosulubika huku mtaani kwanini wasiwe na Mashaka na maamuzi ya watawala...Unaambiwa anakumulika na Kienge cha Moto mchana ujue usiku anakuchoma kabisa Msitete kila kitu hata kama Maisha yenu yamefungamana na Kijani kuusema ukweli sidhani kama itakupunguzia Posho yako Tafakari....
 
Huyu ndio anaempoteza magu kwenye mambo ya uchumi kwani anajulikana ni ktk pioneers wa Sera za free mkt tokea WB mpk alivorudi tz lkn kwa magu anajifanya ni si mbepari ila atakuja ingiza nchi kwenye crisis kubwa ya kiuchumi na atajuta
hypocrites never suceed
 
naamini katika system, mpango hafanyi kazi peke yake. pia hiyo bajeti kila waziri aliandaa bajeti yake. tuache kuatack mtu, tujadili content.
Waziri wa Fedha sindio anaandaa Bajeti kuu? Baada ya kila Wizara kuleta mapendekezo yake
 
Back
Top Bottom