Peter Mutharika atangazwa mshindi Uchaguzi Mkuu Malawi

Peter Mutharika atangazwa mshindi Uchaguzi Mkuu Malawi

Kila mtu ana taarifu ya nani ametangazwa kuwa rais, haina haja ya kukuambia kuwa vice versa is true, we mwenyewe utajua,
 
mkuu sjaelewa funzo ni lipi hapo kwamba chama tawala kimeendelea kutawala au
 
Mada kama hizi sidhani kama zinastahili kuwepo humu
 
Kila mtu ana taarifu ya nani ametangazwa kuwa rais, haina haja ya kukuambia kuwa vice versa is true, we mwenyewe utajua,

ndugu mjumbe.....kama ukiona umekosa mada ya kuweka mezani....ni heli umelizie kunywa kahawa yako...kuliko kujaza server...naomba mwenyekiti ndugu mwenyekiti achague mjumbe mwingine aweke mada mezani....huyu mwenzetu ameshalewa na kahawa.....ila kabla ya kuweka mada mezani....ndugu wajumbe kuna kahawa...hapaa inachemka kikombe...50..huyu mleta mada ameshavurugwa...na ukawa
 
mleta mada kavurugwa,sijui sembe la lumumba linamzingua!???
 
Dikteta ameaibishwa na Demokrasia

Mama Banda KASHINDWA na Tume huru ya uchaguzi SIO UPINZANI!!

Mzee Lububa HAWEZI kufanya kama alichofanya Jaji Mkongwe Maxi Chimbendera wa Malawi!Bila Tume huru mwakani HUWEZI ishinda CCM
 
Sherehe ya kumwapisha Mutharika kama Rais wa tano wa Maawi ndiyo tayari imekamilika. Imefanyika katika jengo la mahakama kuu Blantyre. Imefanyika haraka ile mbaya.
 
Hivi Tanzania imewakilisha na nani wakati wa kuapishwa nasikia anaapishwa leo au kwa vile kipenzi cha CCM JB kaangukia pua.
 
Je, Unazifahamu siasa za Malawi mpaka unaanza kuzilinganisha na siasa na utawala nchini.

Unawafahamu movers and shakers wa Malawi au ndiyo yale yale ya bendera fuata upepo?.

Fanya kwanza homework ndiyo upate uwanja mpana wa fikra katika kujenga hoja kuhusu siasa na utawala wa Malawi.

Kama Malawi INGEKUKUWA na Tume ya uchaguzi kama hii ya Tanzania ambayo Rais JK anaweza kumfukuza kazi Mwenyekiti wake siku yyt hata masaa kabla HAJATANGAZA matokeo Rais Banda ANGESHINDA!

Rais Banda kahangaika wewee kutoka kusema uchaguzi urudiwe,kuamuru Tume iache kutangaza matokeo,jana kasema kaipa Tume siku 30 za re count kote huko kashindwa maana Tume ya Malawi ukiiteua ikipitishwa na Bunge Rais HUNA tena nguvu ya kuingilia kazi zao!

2015 Tanzania tuwe na Tume yenye nguvu huru kama hii ya Jaji Chimbendera wa Malawi,Jaji Lubuva na wenzake ni boya tu pale wanahofia kupoteza kazi zao!
 
Je, Unazifahamu siasa za Malawi mpaka unaanza kuzilinganisha na siasa na utawala nchini. Unawafahamu movers and shakers wa Malawi au ndiyo yale yale ya bendera fuata upepo?. Fanya kwanza homework ndiyo upate uwanja mpana wa fikra katika kujenga hoja kuhusu siasa na utawala wa Malawi.
Whatever the case ni funzo tosha kwa chama tawala, JB kakaa madarakani kwa kipindi cha miaka 2 tu lakini ufuska alioufanya ni wa kutisha na kuwasahau wananchi. Leo Mutharika kaapishwa sijui kama CCM imekumbukua hata kutuma mwakilishi kule.
 
PROFESA MUTHARIKA ATANGAZWA KUWA RAIS WA MALAWI

Joyce Banda amebana, ameachia! Hatimaye mshindi wa kiti cha urais nchini Malawi, Prof Bingu wa Mutharika, aliyesimama kwa tiketi ya chama cha Democratic Progressive Party (DPP), ametangazwa rasmi na tume ya uchanguzi ya Malawi (MEC) kuwa Rais wa Malawi. Katika uchaguzi huo Prof Mutharika aliyepata 34.6% ya kura zote, akifuatiwa na mgombea wa chama cha Malawi Congress Party (MCP), Bw Lazarus Chakwera (27.8%) aliyeshika nafasi ya pili. Nafasi ya tatu ilienda kwa mgombea wa chama cha People's Party (PP), Bi Joyce Banda (20.2%), aliyeangukia pua kwa kushika nafasi ya tatu.

MAONI YANGU
Bi Joyce Banda anastahili kushtakiwa kwa uchochezi wa kukataa matokeo na kusababisha vurugu zilizopelekea polisi kuwaua wanachi kadhaa wa Malawi ktk mji wa Lilongwe na Mzuzu. Lazima nchi za kiafrika zitunge sheria za kuwafikisha mahakamani viongozi ving'ang'anizi kama Joyce Banda wanaosababisha mauaji kwa raia wasiokuwa na hatia kwa sababu tu ya kupenda kuning'inia madarakani.

Aidha Bi Banda anastahili kuchukuliwa hatua kwa kuifukarisha Malawi na kupelekea uchumi wake kushuka kwa kasi ya kutisha, kitendo ambacho kimesababisha wananchi wa Malawi waamue kumpiga chini ili kumpisha Prof wa Mutharika aimarishe uchumi wan chi na kuboresha maisha ya wananchi wa Malawi wanaotopea kwenye umasikini wa kutisha.

FUNDISHO KWA TANZANIA
Uchaguzi huu uwe fundisho kwa wananchi wa Tanzania wanaotopea kwenye ufukara kwa sababu ya utawala dhalimu tulio nao, ili wafanye maamuzi sahihi mwaka 2015 na kuitosa CCM na serikali yake ambao ndio waliotufikisha hapa tulipo. Tusikae tu kulalamikia vitendo vya kifisadi (IPTL, ESCROW, EPA, RICHMOND, DEEP GREEN, KAGODA, UDA, etc) vinavyoisumbua nchi huku tukiwa hatuchuki hatua ya kuutupilia mbali utawala huu dhalimu na dhaifu unaonuka ufisadi.

Nawasilisha.
====================================================================================
OMBI
Mods tafadhali unganisha hii comment na uzi mkuu ili twenda kwa pamoja. Niliandaa uzi kabla ya kugundaua kama tayari uzi mwingine ulishaanzishwa.
 
Kutoka Rais hadi kuwa mshindi wa 3 kwenye uchaguzi,
 
Je, Unazifahamu siasa za Malawi mpaka unaanza kuzilinganisha na siasa na utawala nchini.

Unawafahamu movers and shakers wa Malawi au ndiyo yale yale ya bendera fuata upepo?.

Fanya kwanza homework ndiyo upate uwanja mpana wa fikra katika kujenga hoja kuhusu siasa na utawala wa Malawi.

Mbona unapenda sana kujivua akili na kusahau unayokuwa unayaandika siku za nyuma? Baada ya kushinda Uhuru Kenyata Kenya mlisema ni funzo kwa CHADEMA, pia baada ya kushinda Mugabe kule Zimbabwe Mlisema ni Funzo na salam kwa CHADEMA 2015 na hii ya juzi baada ya ANC(Zuma) kushinda kule South Africa mlizema ni Salam kwa Upinzani hapa nchini na kiongozi wa matamko hayo ni NAPE na nyie wapambe wake mkifuatia sasa je siasa za hizo nchi zinaringana na za hapa Tanzania?
 
Hivi katiba yetu inayopendekezwa imesemaje kuhusiana asilimia za kura anazotakiwa kupata mgombea uraisi, hivi ni simple majority hata ya kura ya mtu mmoja kama ilivyopata kutokea upande uleeee au mshindi lazima apate zaidi ya asilimia 50.

Siku nyingine atakuja patikana mshindi kwa asilimia kumi tu !

Sera za mambo ya nje ya Peter Mutharika wakati akijinadi kwenye uchaguzi wa Malawi zilikuwaje? Na hususani hasa na hii 'issue' yetu na Wamalawi.
 
Back
Top Bottom