Viktor Orban Ashindwa Uchaguzi huko Hungary

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,839
Reaction score
24,529
43beb6bf-4bc8-4262-ab45-b9047bc3437a.jpeg

Uchaguzi wa Hungary umekwisha na aliyekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 16, Viktor Orban, kipenzi cha Trump na Putin, na mwiba mkali kwa European Union na Ukraine amepigwa chini vibaya sana.

Kwenye bunge lenye viti 199, chama cha mpinzani wake, Péter Magyar, kimejizolea zaidi ya viti 135 ambayo ni zaidi ya theluthi mbili itakayowapa mandate ya kufanya mabadiliko ya katiba bila kuzuiliwa.

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, chama cha Viktor Orban kilipata hiyo super majority na kubadili katiba iliyofanya awe anashinda viti hata kama anapata kura chache ikiwamo pamoja na kupunguza viti kwenye miji mikubwa ambako alikuwa na ushindani na kuongeza viti kwenye maeneo ya vijijini ambako alikuwa anawarubuni kirahisi ingawa majimbo hayo yana watu wachache kulinganisha na mjini.

Kufuatia mabadiliko hayo aliendelea kushinda mara tatu zaidi na hivyo kukaa madarakani miaka 16.

Utawala wake ulijaa rushwa na upendeleo sana huku hali ya uchumi wa nchi ikiwa inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.

Sijui kama hilo linaweza kufanyika Tanzania.

======

Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orbán, amekubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, Aprili 12, 2026, na hivyo kuhitimisha utawala wake wa miaka 16. Orbán amekiri kuwa matokeo hayo yana "maumivu" lakini yako wazi, na amesema yeye pamoja na chama chake cha Fidesz sasa watalitumikia taifa wakiwa upande wa upinzani.

Uchaguzi huo umeshindwa na chama cha Tisza, kinachoongozwa na Péter Magyar. Kwa wasiomfahamu, Magyar alikuwa mshirika wa karibu wa zamani wa Orbán kabla ya kugeuka na kuwa mkosoaji wake namba moja.

Dondoo Muhimu za Uchaguzi Huu:

Mshindi: Chama cha Tisza cha Péter Magyar kipo kwenye mwelekeo wa kupata ushindi wa kishindo (landslide victory). Kinatarajiwa kujizolea viti 137 na kupata theluthi mbili ya wingi wa wabunge (supermajority) bungeni.

Waliojitokeza Kupiga Kura: Uchaguzi huu umeweka rekodi ya kihistoria kwa kuwa na asilimia 77% hadi 78% ya watu waliojitokeza kupiga kura. Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi katika historia ya Hungary tangu nchi hiyo ilipoondokana na mfumo wa Kikomunisti.

Vipaumbele vya Kampeni: Kampeni ya Magyar ilijikita katika mapambano dhidi ya rushwa, mageuzi ya kiuchumi, na kuboresha sekta za afya na elimu. Pia aliahidi kurejesha uhusiano mzuri kati ya Hungary na Umoja wa Ulaya (EU).

Athari Kimataifa: Kushindwa kwa Orbán kunatazamwa na wengi kama pigo kubwa kwa washirika wake wa karibu, wakiwemo Rais wa Urusi Vladimir Putin na Donald Trump wa Marekani. Kwa upande mwingine, viongozi wa Ulaya kama Ursula von der Leyen wamepongeza matokeo haya na kuyaita "wakati wa kihistoria kwa demokrasia ya Ulaya".
 
View attachment 3571650

Uchaguzi wa Hungary umekwisha na aliyekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 16, Viktor Orban, kipenzi cha Trump na Putin, na mwiba mkali kwa European Union na Ukraine amepigwa chini vibaya sana.

Kwenye bunge lenye viti 199, chama cha mpinzani wake, Péter Magyar, kimejizolea zaidi ya viti 135 ambayo ni zaidi ya theluthi mbili itakayowapa mandate ya kufanya mabadiliko ya katiba bila kuzuiliwa.

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, chama cha Viktor Orban kilipata hiyo super majority na kubadili katiba iliyofanya awe anashinda viti hata kama anapata kura chache ikiwamo pamoja na kupunguza viti kwenye miji mikubwa ambako alikuwa na ushindani na kuongeza viti kwenye maeneo ya vijijini ambako alikuwa anawarubuni kirahisi ingawa majimbo hayo yana watu wachache kulinganisha na mjini.

Kufuatia mabadiliko o aliendelea kushinda mara tatu zaidi na hivyo kukaa madarakani miaka 16.

Utawala wake ulijaa rushwa na upendeleo sana huku hali ya uchumi wa nchi ikiwa inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.

Sijui kama hilo linaweza kufanyika Tanzania.

======

Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orbán, amekubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, Aprili 12, 2026, na hivyo kuhitimisha utawala wake wa miaka 16. Orbán amekiri kuwa matokeo hayo yana "maumivu" lakini yako wazi, na amesema yeye pamoja na chama chake cha Fidesz sasa watalitumikia taifa wakiwa upande wa upinzani.

Uchaguzi huo umeshindwa na chama cha Tisza, kinachoongozwa na Péter Magyar. Kwa wasiomfahamu, Magyar alikuwa mshirika wa karibu wa zamani wa Orbán kabla ya kugeuka na kuwa mkosoaji wake namba moja.

Dondoo Muhimu za Uchaguzi Huu:

Mshindi: Chama cha Tisza cha Péter Magyar kipo kwenye mwelekeo wa kupata ushindi wa kishindo (landslide victory). Kinatarajiwa kujizolea viti 137 na kupata theluthi mbili ya wingi wa wabunge (supermajority) bungeni.

Waliojitokeza Kupiga Kura: Uchaguzi huu umeweka rekodi ya kihistoria kwa kuwa na asilimia 77% hadi 78% ya watu waliojitokeza kupiga kura. Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi katika historia ya Hungary tangu nchi hiyo ilipoondokana na mfumo wa Kikomunisti.

Vipaumbele vya Kampeni: Kampeni ya Magyar ilijikita katika mapambano dhidi ya rushwa, mageuzi ya kiuchumi, na kuboresha sekta za afya na elimu. Pia aliahidi kurejesha uhusiano mzuri kati ya Hungary na Umoja wa Ulaya (EU).

Athari Kimataifa: Kushindwa kwa Orbán kunatazamwa na wengi kama pigo kubwa kwa washirika wake wa karibu, wakiwemo Rais wa Urusi Vladimir Putin na Donald Trump wa Marekani. Kwa upande mwingine, viongozi wa Ulaya kama Ursula von der Leyen wamepongeza matokeo haya na kuyaita "wakati wa kihistoria kwa demokrasia ya Ulaya".

uyo Orban alikuwa kiongozi wakwanza ktk umoja wa Ulaya kumkaribisha NETANYAHU pale Hungary !!

pamoja na Ukweli kuwa NETANYAHU alikuwa anatafutwa na ICC !! So pia ni Pigo kwa Israel✍️
 
Back
Top Bottom