Peter Mutharika atangazwa mshindi Uchaguzi Mkuu Malawi

Peter Mutharika atangazwa mshindi Uchaguzi Mkuu Malawi

"Mgombea urais anayetetea kiti chake akishindwa kwenye uchaguzi jua ni mzembe"(Underuse of available resources i.e Tume ya Uchaguzi,Mahakama na Jeshi) Robert Mugabe
 
joyce banda kawaaibisha wanawake wote wa africa
 
View attachment 161635 Anaweza kafikiri hwa wahesabu kura wamehongwa View attachment 161636

Joyce Banda pamoja na jitihada zake kutaka kusitisha kuhesabu kura ameangukia pua, jamani maumivu ya kuiacha Ikulu kumbe makubwa hivi.

Nimependa hiyo ya Jaji wa Malawi kuwa The Law is very clear! Hakuna kupepesa macho kwenye Sheria halali! The rule of Law shall prevail! Tanzania tujifunze kutoka Malawi, sheria lazima ifuatwe!
 
Mahakama Kuu ya Malawi imetupilia mbali matakwa ya kuhesabu upya kura. Akitoa hukumu, saa 3 usiku jana, kwa saa za Malawi, Jaji Kenyata Nyirenda, alisema kwamba kifungu cha 99 cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, kinaeleza kwamba matokeo hayana budi kutangazwa ndani ya siku nane, ambazo mwisho wake ulikuwa jana 30.5.14, na kwamba sheria haitoi nafasi ya kuongezwa muda huo. Hivyo akaiagiza Tume ya Uchaguzi, kutangaza mara moja matokeo rasmi ya Uchaguzi. Muda mfupi baadaye, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (MEC), Jaji Maxon Mbendera, alimtangaza rasmi, Profesa Peter Mutharika wa chama cha Upinzani cha DPP, kuwa mshindi kwa kupata 36.4% za kura. Aliyefuatia, ni Mchungaji Lazarous Chakwera wa chama cha MCP, aliyepata 27.8%. Aliyekuwa Rais, Joyce Banda, amekuwa wa tatu kwa kupata 20.2%, na wa nne, ni Atupele Muluzi wa UDF, aliyepata 13.7%. Baada ya kutangazwa matokeo hayo, maelfu ya wafuasi wa DPP walijimwaga mitaani kusherehekea ushindi, na muda mfupi baadaye, Joyce Banda aliyakubali matokeo. Profesa Peter Mutharika ataapishwa kuwa Rais, saa 4.30 asubuhi hii, kwa saa za Tanzania, katika viunga vya Mahakama Kuu ya Malawi.
 
wamalawi inaonekana wanajua matatizo yanayowakabili ndio maana wanathubutu kubadikisha uongozi kuonyesha kwamba wanamtafuta kiongozi bora .Afrika rasilimali zipo tele tatizo ni uongozi na sheria zinazo wafanya wananchi kuwa waumini na watawala kuwa miungu.
 
joyce banda kawaaibisha wanawake wote wa africa

Hapana kawaaibisha watawala wote wa Afrika.Ninachokiona ukishapata sukari ya kutawala kuiachia huwa ngumu sana.Pole kwa watawala wote wa Afrika.
 
Huyu Prof na chama chake cha DPP ni mtu hatari ktk mzozo wa ziwa Nyasa sidhani kama tutakwepa kutumia Jw kumaliza mzozo huo.
 
Mahakama Kuu ya Malawi imetupilia mbali matakwa ya kuhesabu upya kura. Akitoa hukumu, saa 3 usiku jana, kwa saa za Malawi, Jaji Kenyata Nyirenda, alisema kwamba kifungu cha 99 cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, kinaeleza kwamba matokeo hayana budi kutangazwa ndani ya siku nane, ambazo mwisho wake ulikuwa jana 30.5.14, na kwamba sheria haitoi nafasi ya kuongezwa muda huo. Hivyo akaiagiza Tume ya Uchaguzi, kutangaza mara moja matokeo rasmi ya Uchaguzi. Muda mfupi baadaye, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (MEC), Jaji Maxon Mbendera, alimtangaza rasmi, Profesa Peter Mutharika wa chama cha Upinzani cha DPP, kuwa mshindi kwa kupata 36.4% za kura. Aliyefuatia, ni Mchungaji Lazarous Chakwera wa chama cha MCP, aliyepata 27.8%. Aliyekuwa Rais, Joyce Banda, amekuwa wa tatu kwa kupata 20.2%, na wa nne, ni Atupele Muluzi wa UDF, aliyepata 13.7%. Baada ya kutangazwa matokeo hayo, maelfu ya wafuasi wa DPP walijimwaga mitaani kusherehekea ushindi, na muda mfupi baadaye, Joyce Banda aliyakubali matokeo. Profesa Peter Mutharika ataapishwa kuwa Rais, saa 4.30 asubuhi hii, kwa saa za Tanzania, katika viunga vya Mahakama Kuu ya Malawi.
safi sana Tanzania tukae mkao wa kula
 
Malawi bado wachanga sana sana....hapa Tanzania CCM ndio wababe wao..hawafurukuti.
 
Yaan, Huyu mama amekaa madarakani miaka miwili tu??? Kumbe ni mwepesi sana...
 
No one mess up with the United Republic Of Tanzania and go unpunished! Pole sana Joyce Banda.
 
Ataikumbuka sana Tanzania kuhusu mkwara wake wa Ziwa Nyasa kuwa eti lote ni mali ya Malawi. Mwl J. K. Nyerere alishasema ubaya wa kujitenga au ubaguzi. Tunamkaribisha kwa mikono miwili Gentleman Peter Mutharika, bila shaka siku akija kwa State Visit atafahamu vizuri Watanzania kuwa walimchoka JB.
 
Wao hawana sheria ya 50% + 1?????

Hii imekaa sio poa kabisa rais amechaguliwa na wachache sana kati ya waliopiga kura ingependeza round ya 2
 
Back
Top Bottom