Peter Msigwa: Kumbe sio Kila John ni Yohana

Peter Msigwa: Kumbe sio Kila John ni Yohana

Hujaelewa hoja,either kwa kujitoa ufahamu au kwa kuvaa miwani ya mbao!
Hapa hoja ya mleta mada iko wazi!

John wa pili amevurugwa na hotuba ya John wa kwanza!
Hukumuona JJ Mnyika aliposimama na Kumsujudia Rais Magufuli?!...... Unajua maana ya kusujudu kiitifaki na kiimani!.......ndio maana kila siku Lowassa anawapa darasa sema mna vichwa vigumu!......na ndio maana mtu anaruka dhamana kwa mambo yake binafsi mnamuita mfungwa wa kisiasa Ufipa ni bure kabisa!
 
Nimewahi kumsoma Yohana Mbatizaji kwenye Biblia. Yule ambaye kwa kimombo huitwa John the Baptist. Lakini leo pia nimepata bahati ya kuwasikia John wawili wakitoa hotuba. John mmoja ametoa hotuba fupi sana, nzito sana, ya kinyenyekevu sana lakini ya kijasiri sana. Kwa uzito wa hotuba ya John wa kwanza, imelazimu hotuba ya John wa pili kuwa ndefu sana. Niliposikia hotuba ya John wa pili nikagundua kuwa hotuba ya John wa kwanza ni kama imefanya ubatizo kwa hotuba ya John wa pili....maana maneno mengi ya hotuba ya John wa Pili yametokana na maneno machache tu ya hotuba ya John wa kwanza. Wote ni John.... lakini kumbe sio kila John ni Yohana!!!.
Na pengine wanajuta kumualika John wa kwanza, na zaidi kumruhusu "kusalimia". Bahati mbaya salamu zikawafikia hasa. Waendelee kumualika Mzee EL tu, hawa wengine " wanaharibu" shughuli.
 
Sasa tunapeleka azimio Kk ya ccm kupinga kuwaalika wabunge Wa Chadema kwenye shughuli za mkubwa Sizonje kwani wakati sie tunamsifia na kuwaponda wao na kuwakashifu, wao wanatummia dakika 3 kuzungumza kwa unyenyekevu na hekima kutu pre empty hadi Makonda na Mzee baba wanajikuta hawajui wanaongea nini.
Kwa kweli hawa Chadema wanahazina ya vijana wenye akili.
Quote; Kada Wa ccm
Ukiona hawa vijana wa chakubanga alio wamwaga huku jf wana pambana kupunguza nguvu kile Mnyika alicho kifanya leo hatawafanyeje wamekwama kwasababu hata John mkubwa ameonyesha dhairi kwamba John mdogo kamwaribia siku kabisa
 
Yaaa rea ameaffect kabisa hotuba ya john wa pili tena kwa maneno machache ya busara hajasema walipwe like n haki yao bali mtukufu atangulize humanity katika suala hlo kwani hali n mbaya kwa watu wale
 
John wakwanza amemfanya john wa pili na poul wa kwanza wa dar waweweseke nakusahau mantiki ya uzinduzi
Hongera john wakwanza
 
Asee tulikua tunaangalia na jamaa flani wa CHAGADEMA akaniuliza hivi tufanye DOGO asingeongea Mwenyekiti wenu angetoa hotuba gani...

Nikabaki kusema tu hiiiiiiiiiiii!!!!!
Ni Kama tumeikosa hotuba halisi ya president kwa kweli.
Tehetehe!
 
Nimewahi kumsoma Yohana Mbatizaji kwenye Biblia. Yule ambaye kwa kimombo huitwa John the Baptist. Lakini leo pia nimepata bahati ya kuwasikia John wawili wakitoa hotuba. John mmoja ametoa hotuba fupi sana, nzito sana, ya kinyenyekevu sana lakini ya kijasiri sana. Kwa uzito wa hotuba ya John wa kwanza, imelazimu hotuba ya John wa pili kuwa ndefu sana. Niliposikia hotuba ya John wa pili nikagundua kuwa hotuba ya John wa kwanza ni kama imefanya ubatizo kwa hotuba ya John wa pili....maana maneno mengi ya hotuba ya John wa Pili yametokana na maneno machache tu ya hotuba ya John wa kwanza. Wote ni John.... lakini kumbe sio kila John ni Yohana!!!.

Haya ndio mambo yanayoendelea kutuchelewesha kufika tunakotaka kwenda. Ni dhahiri kwamba Roho Mtakatifu anatujalia kila mmoja wetu kipaji au talanta tofauti na mwenzake. Lililo la muhimu ni kila mtu kutambua namna alivyopendelewa na Roho.

Pale hayakuwa mashindano ya hotuba Bali namna ya Kueleza mahitaji ya watanzania. Mnyika hakuweza kueleza mambo muhimu kwa Maneno machache kwa sababu aliigiza jina la YOHANA MBATIZAJI.Jina lina nafasi ndogo sana katika kumfanya mtu afanikiwe au ashindwe.

Tujifunze kupongezana pale kila mmoja anapofanya vizuri. Mbona hata Magufuli kasema baadhi ya mambo kwa mantiki tu. Kwa nini Msigwa hajachukua upande Wa kusifu ya kila upande?
 
Nilivyo ona mimi siku za John Mnyika kuhamia CCM zina hesabika baaada ya kukunwa vizuri na mambo makubwa yanayo fanywa na Rais JPM, tuache ushabiki maandazi wengi wanamkubali kimyakimyaaaa. Japo wanaogopa kusema bayanaa
 
Haya ndio mambo yanayoendelea kutuchelewesha kufika tunakotaka kwenda. Ni dhahiri kwamba Roho Mtakatifu anatujalia kila mmoja wetu kipaji au talanta tofauti na mwenzake. Lililo la muhimu ni kila mtu kutambua namna alivyopendelewa na Roho.

Pale hayakuwa mashindano ya hotuba Bali namna ya Kueleza mahitaji ya watanzania. Mnyika hakuweza kueleza mambo muhimu kwa Maneno machache kwa sababu aliigiza jina la YOHANA MBATIZAJI.Jina lina nafasi ndogo sana katika kumfanya mtu afanikiwe au ashindwe.

Tujifunze kupongezana pale kila mmoja anapofanya vizuri. Mbona hata Magufuli kasema baadhi ya mambo kwa mantiki tu. Kwa nini Msigwa hajachukua upande Wa kusifu ya kila upande?
Mkuu akiwa unaandika jaribu kushirikisha 'kichwa' ili ueleweke. unatakiwa uwe unaweka ushabiki pembeni kuliko mihemko yako.
 
Back
Top Bottom