Nimewahi kumsoma Yohana Mbatizaji kwenye Biblia. Yule ambaye kwa kimombo huitwa John the Baptist. Lakini leo pia nimepata bahati ya kuwasikia John wawili wakitoa hotuba. John mmoja ametoa hotuba fupi sana, nzito sana, ya kinyenyekevu sana lakini ya kijasiri sana. Kwa uzito wa hotuba ya John wa kwanza, imelazimu hotuba ya John wa pili kuwa ndefu sana. Niliposikia hotuba ya John wa pili nikagundua kuwa hotuba ya John wa kwanza ni kama imefanya ubatizo kwa hotuba ya John wa pili....maana maneno mengi ya hotuba ya John wa Pili yametokana na maneno machache tu ya hotuba ya John wa kwanza. Wote ni John.... lakini kumbe sio kila John ni Yohana!!!.