Jeep wrangler
JF-Expert Member
- Jan 7, 2024
- 327
- 724
Wakuu habari zenu,
Wakati wa utawala wa Mkapa kuna hali ya ukata wa pesa ulijitokeza tukauita UKAPA.
Wakati wa JK kiasi flani mambo yakalainika japo ufisadi ulikuwa juu sana na mfumuko wa bei. Kila mtu aligeuka dalali. Pale Mnazi Mmoja wakazaliwa madali wenye vitambi na kiburi, huwezi uza gari kupitia wao.
Wakati wa JPM likajitokeza neno VYUMA vimekaza. Mwanzoni mwa utawala wa JPM miradi binafsi na iashara zilidoda, hili hata mimi lilinikumba lakini kuna wakati mambo yalininyookea hatari.
Awamu hii ya mama, tulitegemea mambo yanyooke zaidi kwani kwa kauli kuwa anaifungua nchi tulitegemea neema zaidi.
Mambo yamekuwa kinyume sana. Biashara nyingi zimeyumba, mfano kariakoo hali sio nzuri kabisa.
Makampuni mengi binafsi yako hoi.
Shule binafsi wanalia.
Wananchi huku chini uraiani hali ni tete kuliko maelezo.
Je huko uliko hali ikoje?