Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,891
PESA ISIWE KIPIMO CHA UTU; FAMILIA NA TAIFA LITAANGAMIA.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
Nataka watu waelewe kuwa Maisha hayana maana yoyote Kama hautajali utu wako na utu WA watu wengine.
Tafsiri sahihi ya Upendo ni kujijali utu wako na utu wa wanaokuzunguka.
Koo kubwa zote zenye nguvu zilijengwa katika misingi ya utu na kujaliana wao Kwa wao. Mataifa Makubwa yote unayoyaona yamejengwa katika msingi wa umoja, upendo na kujali utu WA binadamu.
Ukitaka familia na Ukoo utakaouanzisha uwe na nguvu basi lazima uujenge katika misingi na kanuni ya kujali utu, kupendana wao Kwa wao na kuheshimiana.
Ni hatari mtu kufanya kazi Kwa ajili ya pesa.
Ni hatari mtu kuwania uongozi Kwa ajili ya pesa.
Nasisitiza ni hatari Sana.
Hakuna taifa linalojengwa Kwa namna hiyo.
Ni hatari Mwanamke kutaka kuolewa na wewe Kwa sababu unapesa.
Ni hatari mwanaume kutaka kukuoa Kwa sababu unapesa.
Ukifika Maeneo ya makazini mwa watu ni rahisi kuelewa hatari ya watu waliojiingiza katika Kazi hizo Kwa sababu ya pesa au mishahara.
Ni hatari kuwa na wanaJeshi ambao wapo Kwa sababu ya pesa/mishahara. Ni hatari.
Ninaelewa nini ninakisema, ninaushahidi usio na Shaka katika Maeneo mbalimbali niliyoweza kufika nikajionea Kwa macho yangu.
Mahospitalini, mashuleni, viwandani n.k huko kote ni hatari kuwakuta watu waendekeza Pesa.
Hata Watu wanaouza nchi Kwa mikataba mibovu ni Kwa sababu ya kuendekeza Pesa.
Sio ajabu wenye uroho wa pesa hawaoni shida kutumia pesa za umma vibaya na kujilimbikizia Mali pasipo kujali utu wa wananchi masikini.
Pesa isiwe kipimo cha UTU.
Pesa iwe sehemu ya kuimarisha utu wa watu na sio kiwe kipimo cha UTU.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam