Muda wako ndio kipimo cha maisha yako

black-tz

Member
Jul 20, 2021
38
55
MUDA WAKO NDIO KIPIMO CHA MAISHA YAKO

Sekunde ikipita, ndo nitolee!

Kuna vitu vingi duniani unaweza kuvichezea na kusiwe na shida.

Chezea mali utatafuta na kuchuma zingine.

Chezea pesa, utazisaka na kuzipata zingine.

Kuna kitu kinaitwa MUDA.
Huu baba, hauchezeki.

Ukipita, umepita.

REPOST.

Muda ni kipimo cha maisha yako.

Mali unaweza kuchuma kadri unavyoweza na usifikie viwango fulani.

Unaweza ukachuma pesa nyingi tu, lakini bado unaweza ongeza.

Kwa bahati mbaya muda huwa unaisha na haurudi nyuma.

Unapozaliwa unapewa kiwango cha muda.

Unapewa kipimo cha saa 24, siku 7, miezi 12.

Na unakuwa na muda wako maalum wa kuutumia muda wako na kusepa.

Ndio maana kila unaposherekea birthday, basi ni muhimu kukumbuka kuwa umepoteza mwaka mmoja na umesogea zaidi kwenye kifo chako.

Unaweza kula kwa afya na kufanya mazoezi na kufanya uishi muda mrefu zaidi.

Lakini bado utakuwa kwenye kipimo chako kile kile.

Muda hauongezeki.

Muda ukipita umepita.

Muda sio pesa utaenda kopa.

Muda sio mali utapoteza na kurudisha.

Hebu angalia ukiwa barabarani, sek 1 inatosha kukuweka mtaroni na kusahaulika kabisa.

Kila sekunde inayopita kuna watu wanajenga maisha yao na wengine wanayabomoa.

Kwa bahati mbaya masikini huona wako na muda wa kutosha kuchezea.

Anaweza kufanya chochote na muda akijua yuko nao mwingi sana.

Kwa matajiri stori ni tofauti kabisa.

Kila muda una maana yake.

Pesa inatafutwa zaidi ili kuweza kulipia muda wa kuwa huru na kuenjoy maisha.

Kadri unavyokuwa na muda mwingi wa kula maisha, maana yake kuna gharama kubwa umelipia kwenye utafutaji.

Ni rahisi kwa wengi kukupatia kiasi cha pesa,
Kwa sababu hakina thamani sana.

Kwa mtu aliye busy muda ndio asset ngumu sana kuweza kukupatia.

Ndio maana waliofanikiwa hutoza mamilioni ya sh. Kwa muda kiduchu tu wa huduma zao.

Kuna wakati hata appointmnt unaweza usipate.

Utapeli mkubwa zaidi unaweza kujifanyia ni kutumia muda wako vibaya ilihali ukijua sekunde ikidondoka, ndo imetoka hiyo.

Yaani kadri unvyoiona saa iki-tick ndiyo muda wako unazidi kuisha store.

Sijui unaipata hii vzuri?

Uwe ni tajri au masikini.

Muda tunapewa sawa.

Kazi kwako kuamua utakavyoutumia.

Kila mtu anajua jinsi anavyothaminisha muda wake.

Ndio maana kuna watu kuwaona ni bure tu.

Na kuna watu kuwaona lazima ulipe pesa mingi.

Kwa sababu muda wao ni ghali zaidi kulingana na walivyojithaminisha.

Asiyethamani muda:

-Atalalamika siku zote

-Atasubiri serikali ije imkomboe

-Atabet akitegemea kutajirika

-Atashinda vijiweni kupiga stori

-Atashindana ubishi na wana kijiweni

-Atashinda akiangalia muvi

-Atashinda akicheza magemu ya FIFA

-Atashuhudia gemu zote za mpira

-Mtandaoni yeye ndio kinara wa mijadala

-Mteja mzuri wa Mange

Wakati huo kuna mtu:

-Anasoma vitabu kila siku

-Anajifunza ujuzi kila siku

-Halalamiki wa kulaumu

-Anakula kwa fya

-Anafanya mazoezi

-Kila siku anapandisha thamani yake

-Kila siku anazalisha thamani kwa wengine

-kila siku anakutana na marafiki wapya

-kila siku anajenga ndoto yake

-Anatambua kila linalotokea ni kwa sababu yake

Utajiri na ufukara umetengwa na msitari hafifu sana.

Tofauti kubwa imefichwa kwenye namna wanavyothaminisha na kutumia muda.

Ukiutumia muda wako ipasavyo, utazaa matunda.

Ukiutumia muda wako vibaya, hakuna rangi utaacha kuona.

Maiash ni mchezo wa machaguo.

Kile unachoamua kuchagua na kuwa ndicho kinatokea kwenye maisha yako.

Ukichagua kuwa mbinafsi wa muda wako, basi umetambua siri ya maisha.

Siri ya mafanikio iko kwenye machaguo ya maisha.

Ukichagua kuwa mshindi, utakuwa mshindi.

Ukichagua kuwa msindikizaji, utasindikiza kweli.

Usikubali kutumia muda wako vibaya.

Usikubali kutumia rasilimali yako ambayo kila siku inasisha na huwezi kuirudisha.

NB:

Kuwa na busara.

Kuwa mbinafsi kwenye muda wako.

Kadri muda wako inavyokuwa ghali,
ndivyo ukwasi unazidi kukutembelea.

Ndivyo unavyolipwa zaidi.

Poteza pesa, utapata nyingine.

Poteza mali utapata nyingine.

UKIPOTEZA MUDA, HIYO IMETOKA

Repost Iwafikie Wengi!
 
Message nzuri lkn ningeomba kukuomba urudie kuelewa nn maana ya MUDA ingekuwa vzur coz ndani ya MUDA Kuna mali na pesa na vitu vingine vingi so ukichezeq pesa na mali na elimu na v2 vingine Haina tofaut na kuchezea MUDA.
Unavyosema MUDA ni kuwa unamaanisha kutumia nafasi uliyopata Kwa wakati sahihi mfano kama ulikuwa na nafasi ya kusoma na ukawa unafanya mengine, kama ulikuwa na mali, pesa ukazitawanya na hata pale ambapo ulikuwa na nguvu ya kufanya kitu Cha kiutofauti na ukashindwa kufanya hiyo yote na mambo mengine mengi yamebeba maaana ya kucheza na MUDA.
 
Back
Top Bottom