Pepsi na Coca ni vinywaji vinavyozeesha haraka kuliko pombe

Hyrax

JF-Expert Member
May 20, 2023
605
1,534
Mimi ni mtu ninayependa kufanya tafiti mbalimbali za maisha kila siku japo si jambo nililosomea ila huwa napenda tu kuchunguza mambo mbalimbali ya maisha kwa ujumla wake iwe kupitia watu wengine au mimi mwenyewe, twende kwenye hoja kuu.

Baada ya kupata kazi yangu ya kwanza mwaka 2010 kwenye mkoa mmoja hapa Tanzania Bara, Mwaka 2012 niliamua kuingia kwenye chama cha wanywa pombe na baadaye nikawa mraibu kwa kiasi na kufikia 2015 nilifanikiwa kuchomoka kwenye chama hicho hata ukiniuliza nilichomokaje sina majibu yake mpaka leo.

Nilipumzika kutumia kinywaji chochote cha viwandani kwa muda wa miezi wa 16 yaani hata maji ya dukani nilikuwa sinunui kwakuwa nyumba niliyopanga kulikuwa na kisima nilikuwa nakunywa hayo hata nikienda kazini nabeba kwenye chupa yangu kiukweli afya yangu iliimarika sana kiasi kwamba hata corona niilisikia kwa wengine tu nilikuwa fresh sana na hata chanjo sijachoma mpaka leo.

Mwaka 2017 nikaanza tena kutumia vinywaji vya viwandani yaani juisi, soda mimi twende baada ya miezi sita afya yangu ikaanza kurudi nyuma yaani haipiti miezi 6 tayari nishapigwa malaria, mafua, kichwa na uchovu usioisha nikaona nipumzike kutumia vinywaji hivyo kwa muda wa mwaka na miezi kadhaa hivi afya yangu ikarudi tena kuwa imara mimi ni matunda, mbogamboga na maji ya kisima tu no soda, no juisi za viwandani.

Mwaka 2020 nikaona nirudi tena kunywa vinywaji vya viwandani safari hii nikasema nisinywe kila kitu niwe selective nikachagua kunywa pepsi nikikosa ninywe coca tu na ratiba ya kunywa hivyo vinywaji ilikuwa mara tatu kwa wiki moja katikati ya wiki na mbili mwisho wa wiki yaani baada ya miezi kama sita hivi nikaanza kusikia mwili unabadilika uzito umeongezeka, tumbo limeanza kuwa kubwa, macho yamepoteza uono yaani mpaka kufikia december 2022 mapigo ya moyo yanaenda mbio kwelikweli bila sababu mbaya zaidi nikijiangalia kwenye kioo ni kama sura yangu imeanza kusinyaa ukiniangalia naonekana ni kama mtu ninayekaribia 55 au 60 wakati mimi ni kijana wa 35 tu nikastuka nikaaamua ikifika januari 2023 niache kunywa hivyo vinywaji na ilipofika 2023 nikarudi kwenye matunda na maji ya kisima mpaka nahamia dar hivi karibuni afya yangu imerejea tena naonekana kijana kabisa sura imerudisha nuru.

Baada ya kutafakari kwa kina nimegundua hata nyakati zile nakunywa pombe mwili wangu haukubadilika sana kama nilivyokuwa nakunywa soda na vinywaji vingine vya viwandani hivi karibuni. Naweza kusema kwamba Soda za pepsi na coca ni hatari kwa afya yako hasa kwa vijana. ukinywa hivyo vinywaji unafungulia milango ya magonjwa mengi hasa ya kisukari, uzito mkubwa na presha isiyoisha jieupeshe navyo.

Note: Tunda nililokuwa nalitumia nikishaacha hivyo vinywaji ni TikiTi maji, passion/machungwa/chenza na ndizi. haya matunda hayajawi kuniangusha kwenye kupunguza uzito, presha kuwa sawa na sukari kurudi kawaida.
 
na co
Mimi ni mtu ninayependa kufanya tafiti mbalimbali za maisha kila siku japo si jambo nililosomea ila huwa napenda tu kuchunguza mambo mbalimbali ya maisha kwa ujumla wake iwe kupitia watu wengine au mimi mwenyewe, twende kwenye hoja kuu;

Baada ya kupata kazi yangu ya kwanza mwaka 2010 kwenye mkoa mmoja hapa Tanzania Bara, Mwaka 2012 niliamua kuingia kwenye chama cha wanywa pombe na baadaye nikawa mraibu kwa kiasi na kufikia 2015 nilifanikiwa kuchomoka kwenye chama hicho hata ukiniuliza nilichomokaje sina majibu yake mpaka leo.

Nilipumzika kutumia kinywaji chochote cha viwandani kwa muda wa miezi wa 16 yaani hata maji ya dukani nilikuwa sinunui kwakuwa nyumba niliyopanga kulikuwa na kisima nilikuwa nakunywa hayo hata nikienda kazini nabeba kwenye chupa yangu kiukweli afya yangu iliimarika sana kiasi kwamba hata corona niilisikia kwa wengine tu nilikuwa fresh sana na hata chanjo sijachoma mpaka leo.

Mwaka 2017 nikaanza tena kutumia vinywaji vya viwandani yaani juisi, soda mimi twende baada ya miezi sita afya yangu ikaanza kurudi nyuma yaani haipiti miezi 6 tayari nishapigwa malaria, mafua, kichwa na uchovu usioisha nikaona nipumzike kutumia vinywaji hivyo kwa muda wa mwaka na miezi kadhaa hivi afya yangu ikarudi tena kuwa imara mimi ni matunda, mbogamboga na maji ya kisima tu no soda, no juisi za viwandani.

Mwaka 2020 nikaona nirudi tena kunywa vinywaji vya viwandani safari hii nikasema nisinywe kila kitu niwe selective nikachagua kunywa pepsi nikikosa ninywe coca tu na ratiba ya kunywa hivyo vinywaji ilikuwa mara tatu kwa wiki moja katikati ya wiki na mbili mwisho wa wiki yaani baada ya miezi kama sita hivi nikaanza kusikia mwili unabadilika uzito umeongezeka, tumbo limeanza kuwa kubwa,, macho yamepoteza uono yaani mpaka kufikia december 2022 mapigo ya moyo yanaenda mbio kwelikweli bila sababu mbaya zaidi nikijiangalia kwenye kioo ni kama sura yangu imeanza kusinyaa ukiniangalia naonekana ni kama mtu ninayekaribia 55 au 60 wakati mimi ni kijana wa 35 tu nikastuka nikaaamua ikifika januari 2023 niache kunywa hivyo vinywaji na ilipofika 2023 nikarudi kwenye matunda na maji ya kisima mpaka nahamia dar hivi karibuni afya yangu imerejea tena naonekana kijana kabisa sura imerudisha nuru.

Baada ya kutafakari kwa kina nimegundua hata nyakati zile nakunywa pombe mwili wangu haukubadilika sana kama nilivyokuwa nakunywa soda na vinywaji vingine vya viwandani hivi karibuni. Naweza kusema kwamba Soda za pepsi na coca ni hatari kwa afya yako hasa kwa vijana. ukinywa hivyo vinywaji unafungulia milango ya magonjwa mengi hasa ya kisukari, uzito mkubwa na presha isiyoisha jieupeshe navyo.

Note: Tunda nililokuwa nalitumia nikishaacha hivyo vinywaji ni TikiTi maji, passion/machungwa/chenza na ndizi. haya matunda hayajawi kuniangusha kwenye kupunguza uzito, presha kuwa sawa na sukari kurudi kawaida.
ndom zinazeesha sana ukizizoea mkuu
 
Kwahiyo unataka tena kurudi kwenye pombe amaana navyojua mimi pombe nayo inachakaza sana,very soon utaanza kuonekana mzee uliyechoka....
 
Mimi soda nimefanikiwa kuacha kabisa hapo kwenye maji ya kiwandani na konyagi ndio nimeshindwa kwenye Maji ukizangatia niko dodoma
 
Madhara ya kunywa soda yanajulikana Mimi Ni mnywaji wa soda tena nikiwa na walevi soda kunywa umejutahidi sana 3 ila pombe dadeki jamaa zangu wanatandika bia mpaka 15 kwa siku wengi wait tayari wameshaanza kusumbuliwa na kisukari Mimi soda nabalance na soda water au maji kwa wingi na napima sukari mara kwa mara inakuwa 5 au 5.5 pleasure sina wala tatizo la moyo sina machine ipo safi na uti uzima huu goli 2 hata 3 naweza bahatisha ,ila nikifanikiwa kuacha soda ukweli nitafurahi sana
 
Back
Top Bottom