Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,826
9,533
Nimesoma gazeti la Mwananchi jana lenye kichwa cha Habari ukurasa wa mbele kisemacho
Pombe, 'energy drinks' zinavyomaliza vijana

Kwa mujibu wa hili gazeti wakinukuu wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma ni kwamba:-

1. Vijana Wanne hadi Tisa hufika Hospital hiyo kila wiki Figo zikishindwa kufanya kazi.

2. Watanzania 10 kati ya 100 wana tatizo la Figo

3. Wahanga ni vijana umri kati ya 24-40

4. Gharama za kusafisha Figo kwa mwaka ni wastani wa TZS 31,200,000 Hadi 46,800,000 bila kuweka gharama nyingine kama usafiri

5. Energy drinks ni disaster kwenye moyo kwa mujibu daktari bingwa wa JKCI.

6. Matumizi ya vinywaji hivi yanaathiri pakubwa viungo vitatu ambavyo ni
-Ini,
- Figo na
- Moyo.

7. Wahanga wakubwa ni vijana wa kiume.

MY TAKE:

Vijana acheni pombe, taifa linawategemea. Linda afya yako. Afya ni mtaji.
 
Serikali ipige marufuku hizi energy drinks hasa za kwenye chupa za plastic maana zinauzwa mno bei rahisi.

Kama kuna ulazima ziwepo basi ziwepacked kwenye kopo za Alluminium na moja iuzwe 6,000 ili kuthibiti unywaji holela.

Kama pombe za karatasi za viroba zilipigwa marufuku, Serikali inashindwa nini kupiga marufuku huu ulevi wa energy drink ili kuokoa nguvu kazi ya nchi na kupunguza mzigo mkubwa kwa sekta ya afya?
 
Aisee Mimi bila Energy drinks sijisikii vizuri kabisaaa, 2014 nilikuwa nakunywa mpaka 6 per day lakini Sasa hivi asubuhi kabla sijala chochote lazima ninywe moja baridiii sana ndio nitafute chai Sasa. 🤣🤣🤣
Kuna dereva wa daladala kavuta juzi akiwa kaegesha daladala kituoni. Kaigida akaegemea usukani akakata moto, abiria wanajiuliza nini mbona hatuondoki kumbe suka ashavuta baada ya kubugia eneji drinki. Be careful JKCI wanasema zinaleta madhara makubwa kwenye moyo ni kama viagra
 
Kuna dereva wa daladala kavuta juzi akiwa kaegesha daladala kituoni. Kaigida akaegemea usukani akakata moto, abiria wanajiuliza nini mbona hatuondoki kumbe suka ashavuta baada ya kubugia eneji drinki. Be careful JKCI wanasema zinaleta madhara makubwa kwenye moyo ni kama viagra
Hizo ni myth tu, Mimi niko fresh Sina tatizo lolote kwenye organs zangu zote.
 
Back
Top Bottom