Wajameni, kwa mwenye kufahamu naomba kujuzwa ni duka gani naweza pata hiyo bidhaa hapa Dar?
Natanguliza Shukrani
Wenu katika Ujenzi wa Taifa,
TANMO.
na yenyewe nayo ina masharti katka kuinunua au nainunua kama njugu!Pepper spray zinapatikana Tanganyika arms,kwa hapa dar sifahamu liko wapi ila naskia skia ni mitaa ya upanga, incase utakosa ilo duka basi duka lingine lolote la silaha utapata
hii kitu nadhani naweza kujilinda na hawa wezi wanao kuja na kudai hela!!hope inafaa au wasemaje kiongozi!!amna haina masharti ,pesa yako 2 unaweka ki2 mfukoni, safi sana kwa akina dada,ila midume tuongeze pushups tu!
mkuu uliwahi kuitumia!!inaweza saidia kujilinda na wezi wakikuvamia!!!Nashukuru kwa ufafanuzi, siku za nyuma tulikuwa tunanunua South Africa.
hii kitu nadhani naweza kujilinda na hawa wezi wanao kuja na kudai hela!!hope inafaa au wasemaje kiongozi!!
hawa vibaka wa uswahilini wanakuwa na nondo namapanga kaka!!wa bastola atakuja kwangu kuchukua nini TV!!!Ukiweza kuwa shap ukamuotea machoni lazima aipate fresh yake,ila thamini uhai ulionao kwanza ,usije kumspray mtu mwenye pistol, ukiingia ,youtube kunao video za wa2 waliozitumia zikawatoa kwenye hatari
mkuu uliwahi kuitumia!!inaweza saidia kujilinda na wezi wakikuvamia!!!
Mke wangu aliwahi kuwapulizia vibaka waliotaka kumpora, iliwaingia katika mfumo wa hewa wakakohoa na kushindwa kuona kiasi walikamatwa naa kupelekwa polisi kama mazezeta. Siku hizi ziko ambazo ni advanced zinaweza kwenda mbali zaidi.
Wajameni, kwa mwenye kufahamu naomba kujuzwa ni duka gani naweza pata hiyo bidhaa hapa Dar?
Natanguliza Shukrani
Wenu katika Ujenzi wa Taifa,
TANMO.
mkuu uliwahi kuitumia!!inaweza saidia kujilinda na wezi wakikuvamia!!!
Nenda Tanganyika Arms hapo Samora jirani na TRA office upande wa leseni!! Ukifika Stesheni ukiulizia duka utaonyeshwa tu!! Unataka pasua nani macho aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!! Zipo na za umeme kabisa, akikukaba kibaka mnampiga moja anaona nyota!! Ila kwa wadada wengi kwenye magari yao ni murua sana wawe nazo hasa kama unapita maeneo ya mlalakuwa darajani wale wa DSM wanajua timbili lake pale!
mkuu nasubiri taarifa iwao itaipata huko ili na wadau wengine twende tukajipatie ulinzi binafsi!!Mkuu nashukuru sana, kesho nitaenda kuisaka pale. Kuelekea msimu wa sikukuu ni muhimu kuwa na hii bidhaa ndugu, manake wezi na wanyang'anyi wameongeza spidi ya kupora ili wapate fedha za kula sikukuu. Kwa mtazamo wangu hii ni nzuri kuliko kisu au sime..