Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,667
- 25,700
John Daniel
HALI ya vitisho imeendelea dhidi ya baadhi ya viongozi wa dini nchini, ambao wamejitokeza kufichua siri za magenge yasiyo na maadili kitaifa yanayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, Raia Mwema, imeelezwa.
Mimi nafikiri hapa ndio penye kujadiliwa kwani wale wanaotoa vitisho ni lazima wajulikane na watambuliwe.
Pili hao viongozi wa dini ambao labda mzee Pengo ni mmojawao pia ni lazima wajulikane.
Halafu ndio tufahamu juu ya magenge hayo ambao yanafanya hizo shughuli za uuzaji na usambazaji wa hayo madawa na madudu mengine yasiyo na maana ambayo yanaondoa kabisa neno maadali kwenye jamii yetu.
Utaratibu huu ukifuatwa hapatakuwa na haja ya majadiliano kama haya ambayo yanakuwa yakizungukazunguka.
Biashara ya madawa ya kulevya inalipa sana na bado kuna magenge yanajishughulisha na biashara hiyo haramu duniani na inafanywa kwa uangalifu mkubwa sana.