Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

masonic faith?eti siku izi ndo fasheni..

Tatizo lenu watu wa ABRAHAMIC religions ni kujipenda kupita kiasi na kujiona nyie ndio mko sahihi zaidi ya wengine katika kuabudu,hili ni tatizo kubwa.
 
Kwa hiyo unataka kusema kila taarifa sahihi lazima itolewe na taasisi inayolishughurikia. Na vilevile hakuna taarifa inaweza kuvuja kabla haijatolewa na taasis hiyo na taarifa hiyo ikamfikia mlengwa, mlengwa huyo akaitoa na hivyo taarifa hiyo ikawa ni sahihi? Issue nyingine unataka tuamini kila taarifa inayotolewa na taasisi za serikali ni sahihi na hakuna foul play?

pengo mwenyewe hapo amewataka vijana waiamini taarifa za mitandaoni,hii ina maana kwamba hata hiyo taarifa yake hatutakiwi kuiamini kwa kuwa nayeye kaiona mtandaoni japo anaonekana kuiamini!!!!!!!!!!! ndio maana mimi nikasema nitaiamini taarifa itakayotolewa na wataalam wetu kwa kuwa tunawalipa kwa kazi hiyo ambayo wameisomea!
 
Baada ya sakata la viongozi wa dini na tuhumu za madawa ya kulevya kusimama kwa muda sasa limerejea tena baada ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo kueleza jana masikitiko yake ya kutaka kunyamazishwa kwa kuhusishwa na sakata hilo kama njia ya kumnyamaziaha.

KUJIKANGANYA KWA SERIKALI 1. Wakati wa baraza la Idd, Rais Kikwete alisema kauli yake ilieleweka vibaya, akasema taarifa alizopewa ni za mchungaji mmoja wa Kanisa la Biafra Kinondoni na Shehe mmoja, na hakumaanisha viongozi wote.

2. Waziri Mkuu Pinda wakati akijibu swali la Susan Lyimo (MB.) alisema Rais alieleweka vibaya kwani waliokamatwa, kwa kauli yake ni "wachungaji waswahili wa vikanisa vidogo" na wala si maaskofu kama ilivyochukuliwa na vyombo vya habari. Wakati propaganda hii ikizidi kushika kasi, mtu yeyote makini lazima azingatie yafuatayo.

Kwanza, kwa mfumo wa Kanisa Katoliki, haliitaji kusubili intelijensia ya wabongo iwaambie kiongozi fulani amekengeuka.Kanisa lina intelijensia yake ambayo hata CIA pamoja na nguvu zote wanalitambua hilo.Kiongozi yeyote hata awe Papa akikengeuka kwa issue nyeti kama hii anathibitiwa mara moja,Kwa wale wanaomjua Askofu Koda wa Same waulize leo hii yuko wapi'

Pili, kwa mfumo wa kanisa Pengo kama kiongozi hata nguo zake hajui bei yake. Matunzo yake yote yanafanya na kanisa hadi anakufa, yeye kama yeye haruhusiwi kumiliki hata hela bali alichonacho chote ni mali ya kanisa na hakuna anachokosa.

Tatu
, kanisa aligawi vyeo kwa kujuana wala promotion, ni integrity yake, kwa hiyo hadi Pengo anachaguliwa kuongoza kanisa la Tanzania, integrity yake ni beyond any reasonable doubt. Hata akikengeuka upo mfumo wa kudeal naye hata before intelijensia ya bingo kubaini. Kwa ufupi, Kanisa Katoliki limekuwepo takriban miaka 2000 na litaendelea kuwepo kwa sababu ya misingi yake kiimani na mfumo wake wa kumdhibiti yeyote.

Ni mwendawazimu tu atakayedhani serikali hii ya awamu ya nne itapambana nalo kwa kuzusha tuhuma za kitoto ili kuwanyamazisha viongozi wake. Kwa ushauri tu, serikali zote (na vyama vyao) zilizojidai kupambana na kanisa zimefall apart (revise your history), fanyeni tu wanayowakemea for your political survival.

"kwa mfumo wa Kanisa Katoliki, haliitaji kusubili intelijensia ya wabongo iwaambie kiongozi fulani amekengeuka.Kanisa lina intelijensia yake ambayo hata CIA pamoja na nguvu zote wanalitambua hilo.Kiongozi yeyote hata awe Papa akikengeuka kwa issue nyeti kama hii anathibitiwa mara moja,Kwa wale wanaomjua Askofu Koda wa Same waulize leo hii yuko wapi'"

Mbona kwenye yale mauaji ya rwanda intelijensia ya kanisa katoliki haikuweza kuzibaini nyendo za yule kiongozi wakanisa hilo kujihusisha na mipango ya kuangamiza waumini wake (watutsi)mpaka mauaji yalipotokea?
 
Nadhani hapa hoja ni kua je ni kweli....na je hawezi kujua haki zake Kama kiongozi mkubwa Kama yeye anasingiziwa na je kwanini wasijitokeze nyie mnaokataa kumtetea kuprove kwa umma jamani haya mambo yapo na Chombo cha haki na mahakama kama amechafuliwa na ni clean why tryin to sympathize with the public..... It is an issue that needs to be addresed well na sio kutafuta huruma ya jamii.... It's typical legal matter.....MPOOO?


Ukipenda chongo huita kengeza:lol:

umeandika vizuri sana,watu inabidi tuamke sasa na tuelewe hakuna alie juu ya sheria!haki ya mtu hupatikani mahakamani kule ndio mbivu nambichi hujulikana na wala sio kwa kuongea na vijana ufukweni,haisaidii sana!
 
"kwa mfumo wa Kanisa Katoliki, haliitaji kusubili intelijensia ya wabongo iwaambie kiongozi fulani amekengeuka.Kanisa lina intelijensia yake ambayo hata CIA pamoja na nguvu zote wanalitambua hilo.Kiongozi yeyote hata awe Papa akikengeuka kwa issue nyeti kama hii anathibitiwa mara moja,Kwa wale wanaomjua Askofu Koda wa Same waulize leo hii yuko wapi'"

Mbona kwenye yale mauaji ya rwanda intelijensia ya kanisa katoliki haikuweza kuzibaini nyendo za yule kiongozi wakanisa hilo kujihusisha na mipango ya kuangamiza waumini wake (watutsi)mpaka mauaji yalipotokea?

Hivi kuna ulingano wa kumbaini mtu aliyetoa mimba na aliyekunya? Tumia akili acha ushabiki bwana mdogo
 
MWASHAM BABA ASKOFU SI WEWE TU KUNA WATANZANIA WENYE FIKRA HURU KIBAO WAMEINGIZWA TAYARI KWENYE LISTI YA SIRI YA MIHADARATI NA ORIJINO KUENDELEA KUKUSANYA VUMBI MAGOGONI

Serikali ya Wauza Unga inapogeuzia santuri SAUTI HURU kwa tuhuma juu ya madhambi wayatendao wao wenyewe miaka nenda rudi!!

Idadi ya wauzaunga waliojipenyeza mjengoni Dodoma kwenda kutunga sheria inatisha! Lakini bahati tu ni kwamba tangu jumuiya ya kimataifa ifahamu picha zima, biashara yao imeyumba sana tena sana.

Na hilo ndilo siri mojawapo sehemu kubwa ya hao waliojiingiza kazi ya ubunge kwa maslahi ya kibiashara zaidi leo hii wakaamua kuliingizia taifa hasara kubwa kwa kudai kiwango cha posho ambacho hata kwa mataifa tajiri halipwi mtu.

Lengo ni kufidia kulikoyumba maana kujitoa ubunge kama Rostam Azizi kwa hivi sasa wanaona ni so.

Tangu Iran iingie hati hati ya kivita na Magharibi na Rostam Aziz kusogezewa tochi ya kimataifa kwa jirani zaidi na shingo lake, kuna uwezekano mkubwa sana kwamba vijana wetu wengi wakapona kwa kukosa madawa ya kulevya zaidi kwa kuwa usambazaji wake utaanguka zaidi na zaidi kote Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

Mwasham Baba Askofu, jitulize roho yako. Ni wachache tu hdi hivi sasa ndio hawajui mchezo mzima na jinsi ambavyo serikali ya sasa inavyotumia tuhuma za mihadarati kama silaha ya kuwanyamazisha sauti huru.

Sera yao hivi sasa ni 'Kama vipi basi aheri Tukose wote'. Tutawaumbua wote wahusika halisi muda mwafaka utakapowadia na kuweka hadharani data lukuki hapa.

kwani kasema jina lake limetajwa na nani?mbona mnaweweseka kabla hata ya kumuelewa pengo alichokosema?maneno kajisemea yeye mwenyewe pengo kina rostam wanatokea wapi tena?mnajaribu kuzuia kitu gani kisifanyike?

 
umeandika vizuri sana,watu inabidi tuamke sasa na tuelewe hakuna alie juu ya sheria!haki ya mtu hupatikani mahakamani kule ndio mbivu nambichi hujulikana na wala sio kwa kuongea na vijana ufukweni,haisaidii sana!

Wewe umeandika vizuri zaidi. Nimefurahi kuona kuwa mpo baadhi yenu angalau mnajua mbivu na mbichi hupatikana mahakamani. Sasa kamwambie yule m kw ere aliyeacha kupeleka wahalifu mahakamani na badala yake kuanza kuhubiri majukwaani kuwa haki inapatkana mahakamani. Nakutuma ukamwambie kuwa, wahalifu hawaadhibiwi kwa kuandikwa list na kuihubiri hubiri in such a pathetic manner kwenye majukwaa, badala yake hufanyiwa uchunguzi kimya kimya na kukiwa na ushahidi, hupelekwa mahakamani.
 
Hivi kuna ulingano wa kumbaini mtu aliyetoa mimba na aliyekunya? Tumia akili acha ushabiki bwana mdogo

haya nimekuelewa wewe ni mtu wa aina gani,sasa jibu hoja ya msingi - Mbona kwenye yale mauaji ya rwanda intelijensia ya kanisa katoliki haikuweza kuzibaini nyendo za yule kiongozi wakanisa hilo kujihusisha na mipango ya kuangamiza waumini wake (watutsi)mpaka mauaji yalipotokea?
 
Wewe umeandika vizuri zaidi. Nimefurahi kuona kuwa mpo baadhi yenu angalau mnajua mbivu na mbichi hupatikana mahakamani. Sasa kamwambie yule m kw ere aliyeacha kupeleka wahalifu mahakamani na badala yake kuanza kuhubiri majukwaani kuwa haki inapatkana mahakamani. Nakutuma ukamwambie kuwa, wahalifu hawaadhibiwi kwa kuandikwa list na kuihubiri hubiri in such a pathetic manner kwenye majukwaa, badala yake hufanyiwa uchunguzi kimya kimya na kukiwa na ushahidi, hupelekwa mahakamani.

List ipi unayoizungumzia ambayo haijapelekwa mahakamani?kumbuka hakuna list yeyote official ya polisi ilimtaja pengo,na mimi nakutuma ukamuulize pengo hizo habari yeye kaziokota wapi?mtandaoni ambako anawakataza vijana wasiziamini habari za huko wakati yeye anaonekana kuziamini?
 
Itakuwa waliamuwa kuliondoa...lol

du mzee kwa hiyo umeshajiandaa kumtetea kabisa kwa lolote litalotokea ili tu uihukumu serikali?maana likiwepo jina lake umejiandaa kusema wameliweka ili kumnyamazisha,lisipokuwepo jina lake watakuwa wameliondoa baada ya yeye kujitaja kuwemo kabla!!!! kweli nimeamini mkubwa hakombi mboga akikomba kumsiitiri tunasema kaipenda!
 
Askofo pole.usifunge mdomo Mungu yu nawe endelea kupingania haki za waumini wako
 
Askofu alikuwa kwenye mafundisho ya kawaidb na vijana. Aliamua kuwashirikisha experience yake ili waweze kubaini mambo ya ukweli na uongo yatokayo na utandawazi, hajafanya press conference, ila tu neno la mkubwa ni habari.

Gari la kifahari ndugu yangu ni kitu kidogo sana kwa kanisa katoliki, wala Cardinal hahitaji kufanya biashara kupata kitu. Kwa taarifa ni kuwa wadhifa Kardinari usiulinganishe na huyo mhubiri Bhonke!

He has everything he wants on earth. Akiwa mzee mstaafu bado atatunzwa na kanisa. Kanisa katoliki ni system, tena powerful system ambayo bado inawajali watendaji wake.

ina mapungufu ya mtu mmoja mmoja na siyo ya kimfumo.
 
Lile gari ni mali ya kanisa ndugu usipende kukurupuka ukadhani unaongea jambo la maana mbele za watu. Ni kama yale magari ya ikulu, ukiondoka unayaacha pale unless tuamue kukuzawadia. Hata chakula anachokula pale kinalipiwa na kanisa, njoo na lingine hilo la gari ni la jikoni.

Hajui hadhi aliyonayo Kadnari huyo!!!
 
" WEWE NDIWE PETRO, NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU,WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA".
Milango ya kuzimu hapa kwa maoni yangu ni shetani na tawala yake na yote anayotumia kujaribu kuharibu kanisa Moja, Takatifu
na la mitume.
Baba Kadinali Pengo neno hili likutie moyo likufungue kinywa chako uendelee kutetea haki na ukweli katika kanisa la hapa Tanzania
na Ulimwenguni kote.
Shetani alishashindwa pale msalabani Kalvari.
Tuko nyuma yako katika kutetea Jina lile lipitalo kila jina. Jina la YESU KRISTO mwana wa MUNGU wa kweli aliye hai milele hata
milele.
 
Sijui kwa nini Pengo amejisikia kutoa kauli ya aina hiyo hadharani. Kwanza hajatajwa rasmi katika suala hilo. Pili, nilidhani yuko juu zaidi ya malumbano ya aina hiyo. Mie navyofahamu hii habari ya viongozi wa dini kuhusishwa na madawa ya kulevya tuliletewa kama mkakati wa watu fulani kujiimarisha kisiasa kwa mashabiki wao (whoever they are). Nailinganisha na kauli ya "uchaguzi wa 2010 kutawaliwa sana na udini". Hizi zote ni hoja muflisi za watu kutafuta nafasi za kisiasa miongoni mwa jamii yenye uelewa mdogo.

Sikufurahishwa na Rais kuzidi "kutoa onyo" kwa viongozi wa kidini (ambao alidai anayo orodha yao na ushahidi) kuachana na biashara ya madawa ya kulevya kama vile hatuna utawala wala mifumo ya kisheria inayofanya kazi inavyopasa. Halafu mjinga mmoja Ikulu alipoulizwa kwa nini basi hatua rasmi hazichukuliwi akajibu kuwa eti Rais ni mtu mwema sana anachofanya ni kama kumpa tahadhari jirani kwamba kuna nyoka ndani ya nyumba yake! Hivyo, busara ni kujisafisha badala ya kudai hatua zichukuliwe.

Kwa Pengo kusema alichosema labda tuseme anatafuta kuonewa huruma na jamii bila sababu za msingi. Alitegemea akishambulia viongozi wa kisiasa basi asiguswe kabisa? Angalau mtu kama Sitta na wenzake wenye malalamiko ya aina hiyo mara kwa mara inajulikana wanachokitafuta. Yeye kama kiongozi wa kanisa anatarajia nini hasa? Basi akae kimya kabisa.
 
Back
Top Bottom