Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!

Umeiweka vizuri..Pengo yuko juu ya malumbano ya aina hii! Hakupaswa kutafuta sympathy kwa watu!

Sijui kwa nini Pengo amejisikia kutoa kauli ya aina hiyo hadharani. Kwanza hajatajwa rasmi katika suala hilo. Pili, nilidhani yuko juu zaidi ya malumbano ya aina hiyo. Mie navyofahamu hii habari ya viongozi wa dini kuhusishwa na madawa ya kulevya tuliletewa kama mkakati wa watu fulani kujiimarisha kisiasa kwa mashabiki wao (whoever they are). Nailinganisha na kauli ya "uchaguzi wa 2010 kutawaliwa sana na udini". Hizi zote ni hoja muflisi za watu kutafuta nafasi za kisiasa miongoni mwa jamii yenye uelewa mdogo.

Sikufurahishwa na Rais kuzidi "kutoa onyo" kwa viongozi wa kidini (ambao alidai anayo orodha yao na ushahidi) kuachana na biashara ya madawa ya kulevya kama vile hatuna utawala wala mifumo ya kisheria inayofanya kazi inavyopasa. Halafu mjinga mmoja Ikulu alipoulizwa kwa nini basi hatua rasmi hazichukuliwi akajibu kuwa eti Rais ni mtu mwema sana anachofanya ni kama kumpa tahadhari jirani kwamba kuna nyoka ndani ya nyumba yake! Hivyo, busara ni kujisafisha badala ya kudai hatua zichukuliwe.

Kwa Pengo kusema alichosema labda tuseme anatafuta kuonewa huruma na jamii bila sababu za msingi. Alitegemea akishambulia viongozi wa kisiasa basi asiguswe kabisa? Angalau mtu kama Sitta na wenzake wenye malalamiko ya aina hiyo mara kwa mara inajulikana wanachokitafuta. Yeye kama kiongozi wa kanisa anatarajia nini hasa? Basi akae kimya kabisa.
 
Mwadhama Askofu Mkuu akauze mihadarati ili akapate nini zaidi anachokikosa? Mtu angemtaja Marehemu Hassan Diria wala nisingeleta ubishi wowote ule.
 
Mwadhama Askofu Mkuu akauze mihadarati ili akapate nini zaidi anachokikosa? Mtu angemtaja Marehemu Hassan Diria wala nisingeleta ubishi wowote ule.

Hassan diri hayupo tena mzee,bado ungependa aendelee kutajwa kujihusisha na mihadarati mpaka sasa?kwanini mnafanya jitihada za kuhamishia story kwa wengine wakati mhusika hapa ni bwana pengo?mnasababu zozote za kuhusisha watu wengine kwenye hili labda?
 
ni ushauri nasaha tu kutokana na tatizo lako,ukiufuata unaweza kupona au kupata nafuu!

Ungejikagua vizuri, vurugu za maono na kutojua unachofanya ni zigo linalokutesa. Nakuonea huruma lakini kwa kuwa bado hujaikubali hali hiyo sina jinsi ya kukusaidia. Nafikiria kukuacha tu ili uangamie.
 
Hassan diri hayupo tena mzee,bado ungependa aendelee kutajwa kujihusisha na mihadarati mpaka sasa?kwanini mnafanya jitihada za kuhamishia story kwa wengine wakati mhusika hapa ni bwana pengo?mnasababu zozote za kuhusisha watu wengine kwenye hili labda?

Walikufa Mitume na Manabii. Wafuasi wao bado wapo kedekede!
 
Leo tutasikia mengi si unajua aliyeguswa anawatetezi wengi.Hebu chukulia mtu kama Maalim Ally Bassalehe angihusishwa na hii maneno unadhani ni nini ingekuwa hatma ya mjadala? Nadhani Ingekuwa kejeli ,dhihaka na dharau si tu kwa mwenyewe Maalim Bassalehe bali kwa uuislam na waislam kwa ujumla.Kwenye huu mjadala itoshe tu kusema Jiwe likirushwa gizani atakaye piga kelele limempata,asitafutwe mchawi.

Kwi kwii acha kunichekesha why firing around the bush? Maalim Ally Bassalehe anaweza kuhusishwa na Boko Haram, Al Shabaab kwasababu uhalifu huo (ugaidi) ndiyo yuko likely kuufanya. Na mbaya zaidi atadai anaufanya huo uhalifu kwaajili ya UISLAMU, na hutasikia BAKWATA au muislamu hata mmoja akikanusha hayo madai.

I stand to be corrected
 
[h=1][/h]
John Daniel

pengo220.jpg

Kardinali Pengo

HALI ya vitisho imeendelea dhidi ya baadhi ya viongozi wa dini nchini, ambao wamejitokeza kufichua siri za magenge yasiyo na maadili kitaifa yanayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, Raia Mwema, imeelezwa.

Mmoja wa viongozi hao wa dini ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye wiki iliyopita, aliwaeleza vijana wa kanisa hilo aliokutana nao jijini Dar es Salaam kuwa, naye amekuwa akifanyiwa njama za kunyamazishwa ili asiharibu maslahi ya genge la wafanyabiashara ya dawa za kulevya.

Katika hali isiyo ya kawaida, Kardinali Pengo aliwaeleza vijana wa kanisa hilo katika misa maalumu ya ufukweni inayowakutanisha vijana kila mwaka jijini Dar es Salaam kuwa kumekuwa na kundi la watu wanaoamini anaharibu mwenendo wa mipango yao katika biashara kulevya.

Kutokana na hali hiyo, Pengo aliwaonya vijana kutoendelea kutumika kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu katika biashara hiyo. Hata hivyo, hakuwa tayari kutaja majina ya wahusika wa genge hilo ambalo ameeleza kuwa wamekuwa na mipango ya kumnyamazisha.

Kwa mujibu wa Pengo, stahili wanayotumia kutaka kumnyamazisha ni pamoja na kutaja jina lake katika orodha ya wafanyabiashara ya dawa za kulevya, hali ambayo amesema haitamnyamazisha na badala yake ataendelea kuzungumza kufichua ukweli kuhusu wahusika katika biashara hiyo haramu.

Aliwataka vijana kutukubali kutumika kwa manufaa ya baadhi ya watu hao wachache ambao kwa sasa wameonyesha mwenendo wa kuchukizwa na watu wengine wanaowakosoa.

“Ninyi vijana msikubali kutishwa,” alieleza Kardinali Pengo na kuweka bayana kuwa watenda maovu wakiwamo wanaouza dawa za kulevya wako radhi kuwatumia vijana kufanikisha malengo yao huku wakiwa tayari kuwatishia viongozi wa dini wanapojaribu kukemea uovu wao huo.

Aliwahimiza vijana kupingana na magenge wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya akisema; “Mnao uwezo wa kuwa askari kupigana nao, silaha yenu si bunduki bali ni ukweli.”

Kauli hiyo ya Kardinali Pengo imekuja miezi kadhaa baada ya kuwapo kwa malumbano kati ya baadhi ya viongozi wa dini na Serikali, kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete, alipowaomba viongozi wa dini kusaidi vita dhidi ya dawa za kulevya.

Katika mwendelezo wa kauli hiyo ya Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi, aliwahi kuwaonyesha wabunge picha za video zinazoonyesha baadhi ya wahusika wa dawa za kulevya, wakiwamo baadhi ya viongozi wa dini wa baadhi ya makanisa yasiyo maarufu nchini.

Katika hatua nyinginePadre wa Kanisa Katoliki nchini, Baptist Mapunda, wa Parokia ya Manzese Dar es Salaama, amezungumza na gazeti hili na kumtahadharisha Rais Jakaya Kikwete, kuchukua hatua za haraka kunusuru amani ya nchi iliyopo shakani kutokana na sababu mbalimbali.

“Katika kipindi hiki tatizo la udini limezidi kuwa kubwa sana, kuna makundi yameibuka kutukana dini nyingine hadharani, kauli za kutishia amani za wanasiasa, polisi kupiga raia, ubambikizaji kesi, wananchi kuchukua sheria mkononi, hivi vyote ni viashiria hatari sana kwa amani ya nchi, ninapata shaka,” alisema Padri Mapunda.

Katika kile kinachoonyesha kuwa hali ya kutiliana shaka baina ya viongozi wa dini na viongozi wa serikali, hivi karibuni Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, aliwataka viongozi wa dini kuendelea kukosoa Serikali katika hali ya staha.

Nimepitia hii thread kwa umakini wa hali ya juu lakini sijaona sehemu yoyote Kardinali Pengo, kafichua hiyo siri.
 
Nimepitia hii thread kwa umakini wa hali ya juu lakini sijaona sehemu yoyote Kardinali Pengo, kafichua hiyo siri.

ritz hapa umenena kweli.nilidhani kuna kitu kipya kumbe ni kama ile thread nyingine kuhusu kauli ya pengo.
 
kumbe ndio hawa walikuwa wakitajwa...Pengo anauza nini!!? Hawa viongozi msiwaamini wala nini kama wanaweza kuwa na mahawala wanashindwa nini kuuza!!??....aje aseme vizuri hapa ajatoa siri yeyote wanafiki wakubwa wanaosha kikombe nje huku ndani kimejaa kila aina na uchafu na unyanganyi..!!
 
nimepitia hii thread kwa umakini wa hali ya juu lakini sijaona sehemu yoyote kardinali pengo, kafichua hiyo siri.
hana list yeyote bwana yeye alikua anajisemea tu kama tahadhari...
 
Siri imefichuka siri imefichula kosa la mesenja kaleta balaa!!!
 
John Daniel

pengo220.jpg

Kardinali Pengo

HALI ya vitisho imeendelea dhidi ya baadhi ya viongozi wa dini nchini, ambao wamejitokeza kufichua siri za magenge yasiyo na maadili kitaifa yanayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, Raia Mwema, imeelezwa.

Mmoja wa viongozi hao wa dini ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye wiki iliyopita, aliwaeleza vijana wa kanisa hilo aliokutana nao jijini Dar es Salaam kuwa, naye amekuwa akifanyiwa njama za kunyamazishwa ili asiharibu maslahi ya genge la wafanyabiashara ya dawa za kulevya.

Katika hali isiyo ya kawaida, Kardinali Pengo aliwaeleza vijana wa kanisa hilo katika misa maalumu ya ufukweni inayowakutanisha vijana kila mwaka jijini Dar es Salaam kuwa kumekuwa na kundi la watu wanaoamini anaharibu mwenendo wa mipango yao katika biashara kulevya.

Kutokana na hali hiyo, Pengo aliwaonya vijana kutoendelea kutumika kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu katika biashara hiyo. Hata hivyo, hakuwa tayari kutaja majina ya wahusika wa genge hilo ambalo ameeleza kuwa wamekuwa na mipango ya kumnyamazisha.

Kwa mujibu wa Pengo, stahili wanayotumia kutaka kumnyamazisha ni pamoja na kutaja jina lake katika orodha ya wafanyabiashara ya dawa za kulevya, hali ambayo amesema haitamnyamazisha na badala yake ataendelea kuzungumza kufichua ukweli kuhusu wahusika katika biashara hiyo haramu.

Aliwataka vijana kutukubali kutumika kwa manufaa ya baadhi ya watu hao wachache ambao kwa sasa wameonyesha mwenendo wa kuchukizwa na watu wengine wanaowakosoa.

"Ninyi vijana msikubali kutishwa," alieleza Kardinali Pengo na kuweka bayana kuwa watenda maovu wakiwamo wanaouza dawa za kulevya wako radhi kuwatumia vijana kufanikisha malengo yao huku wakiwa tayari kuwatishia viongozi wa dini wanapojaribu kukemea uovu wao huo.

Aliwahimiza vijana kupingana na magenge wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya akisema; "Mnao uwezo wa kuwa askari kupigana nao, silaha yenu si bunduki bali ni ukweli."

Kauli hiyo ya Kardinali Pengo imekuja miezi kadhaa baada ya kuwapo kwa malumbano kati ya baadhi ya viongozi wa dini na Serikali, kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete, alipowaomba viongozi wa dini kusaidi vita dhidi ya dawa za kulevya.

Katika mwendelezo wa kauli hiyo ya Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi, aliwahi kuwaonyesha wabunge picha za video zinazoonyesha baadhi ya wahusika wa dawa za kulevya, wakiwamo baadhi ya viongozi wa dini wa baadhi ya makanisa yasiyo maarufu nchini.

Katika hatua nyinginePadre wa Kanisa Katoliki nchini, Baptist Mapunda, wa Parokia ya Manzese Dar es Salaama, amezungumza na gazeti hili na kumtahadharisha Rais Jakaya Kikwete, kuchukua hatua za haraka kunusuru amani ya nchi iliyopo shakani kutokana na sababu mbalimbali.

"Katika kipindi hiki tatizo la udini limezidi kuwa kubwa sana, kuna makundi yameibuka kutukana dini nyingine hadharani, kauli za kutishia amani za wanasiasa, polisi kupiga raia, ubambikizaji kesi, wananchi kuchukua sheria mkononi, hivi vyote ni viashiria hatari sana kwa amani ya nchi, ninapata shaka," alisema Padri Mapunda.

Katika kile kinachoonyesha kuwa hali ya kutiliana shaka baina ya viongozi wa dini na viongozi wa serikali, hivi karibuni Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, aliwataka viongozi wa dini kuendelea kukosoa Serikali katika hali ya staha.

Kuna tofauti kati ya maelezo yaliyo katika kauli hizo zenye rangi tofauti, hapo kwenye nyekundu inaonekana dhahiri kuwa hiyo ni tafsiri ya mwandishi na ndiyo maana ameshindwa kui quote kama alivyofanya hapo kwenye green.
Aina hii ya uandishi inanipa shaka sana na sijui kama unaipeleka jamii katika njia sahihi.
 
Nimepitia hii thread kwa umakini wa hali ya juu lakini sijaona sehemu yoyote Kardinali Pengo, kafichua hiyo siri.

hahaha
yaani nimetumia mda mwingi kusoma na kurudia kila mstari,mwisho wa siku nilichokuwa nakitafuta sijakiona zaidi ya kusoma mstari unaomtaja Mzee Pengo kukataa kuwataja wahusika,

sasa sijui kukataa kuwataja ndio siri yenyewe? du kazi ipo JF
 
Back
Top Bottom