Mwandishi wa hiyo makala yupo biased, wewe Zawadi Ngoda unataka kutimiza malengo yako ambayo huenda ni ya kidini au yanasukumwa na chuki za kidini.
Kwa baadhi wameenda mbali zaidi na kuona kuwa, waraka huo si tu unailenga CCM, bali ni Rais Kikwete na washabiki wake serikalini kwa kuonekana kutolisikiliza kanisa katoliki kama ilivyokuwepo kwa akina Nyerere na Mkapa.
Kikwete hajasikiliza nini toka katoliki? Je, Mkapa na Nyerere ndo walikuwa wanasikiliza katoliki? Mwinyi je? au kwasababu ni muislam kama Kikwete?
Wataalamu wa mambo ya siasa, wameeleza kuwa nguvu au ushawishi wa kanisa katoliki ndani ya serikali umepungua sana. Na hii imetokana na Kikwete kutaka kutenganisha kabisa dini na serikali kwa vitendo kitu ambacho kitakuwa kipya kabisa toka tukiwa Tanganyika na hatimaye Tanzania. Kwa maana hali hiyo ilirithiwa toka kwa wakoloni na kupewa baraka zote na mataifa ya magharibi.
you are damn wrong! Katoliki walikuwa na nguvu au ushawishi gani ambao hawana sasa? Kikwete kataka lini kutenganisha dini na Serikali? au kwa kutaka kuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba? Ukitaka kujua ukweli, kipindi hiki cha Kikwete ndo kime-attempt kuingiza dini kwenye Serikali kuliko wakati mwingine wowote.
Unasema juu ya mataifa ya magharibi kuingiza dini kwenye siasa, kwanini usisema mataifa ya uarabuni yanayoongozwa kwa kitabu cha dini kama katiba? kuna mataifa yanayoingiza dini kwenye Serikali kama waarabu? Ukiondoa Ujerumani mataifa mengine ya magharibi yametenga dini na Serikali.
Kikwete aliweza kuwashinda kidiplomasia akina Pengo na wafuasi wake, na ndio maana wakathubutu kutamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu. Rais Kikwete alijua wazi kuwa kuna gharama kubwa ya kulipa kwa kuungwa mkono na makanisa yote. Ni vipi alijiandaa na hilo, hakuna ajuaye isipokuwa waliyekaribu naye tu. Kwa vile yeye ni mkongwe wa siasa wa muda mrefu, ninahakika kabisa anaelewa Nguvu na ushawishi wa kanisa Katoliki duniani. Tena liko tayari hata kuleta vita pale ambapo linaona kuwa linapoteza umaarufu, kwa nia ya kujipanga upya.
Hii nayo ni kuweka ice sugar kwenye keki yako unayoipika sasa. Kama unataka kujenga hoja substantiate, pole sana.
Waraka umebabaisha toto kwa kusema imejikita katika kupinga ufisadi. Wasomi wanaona kama lugha nyepesi ya kidiplomasia waliyoitumia, lakini hasira zao ziliibuka pale Serikali ilipoanza mjadala wa OIC na Mahakama ya Kadhi. Hapa ndio ilikuwa mwisho wa urafiki kati ya kanisa katoliki na Rais Kikwete. Na hii ilimlazimu Pengo kufunga safari kwenda Vatikan na kupata ushauri toka kwa Papa. Pindi aliporudi tu, alimwita Waziri Membe na kufanya mazungumzo ya siri. Na hapo ndipo lilipochimbwa kaburi la Mjadala wa OIC na Mahakama ya Kadhi.
ok, ungeandika aya hii tu, ungeeleweka, kwani hiki ndo kiini cha hoja yako.
Hata hivyo kanisa katoliki halikurithika na hilo, ajenda kubwa ilibakia ni kumtoa madarakani Rais Kikwete kupitia wananchi (kura). Kwa katoliki hili ni suala la mpango wa muda mrefu (Long term). Hivyo si lazima Kikwete ang'oke mwaka 2010, bali hata hapo baadaye. Kwasababu nia si kumuondoa Kikwete peke yake bali ni yeye na wafuasi wake wote toka mikoani mpaka ikulu. Kazi amayo itafanyika toka kwenye vigango(ngazi ya chini ya uongozi wa kanisa) mpaka makao makuu ya katoliki.
So, Kikwete kapanga watu wake hadi vigangoni (lowest level)! Naa hao watu wote wanatakiwa kuondolewa! kanisa limeweka mpango wa muda mrefu kufagia Kikwete? lol jamaa kama ni kumtishia nyau Rais unajitahidi. Hivi hao watu wa Kikwete hakuna wakatoliki! kama wapo maanayake wanaweka mpango wa kujiondoa wenyewe? not logical at all.
Rais Kikwete kwa kulielewa hilo ikawatuma akina Kingunge na wafuasi wake kuupinga waraka huo hadharani. Bahati mbaya kukatokea makundi makundi ndani ya Serikali na Bungeni, huku baadhi wakiwa upande wa serikali na wengine upande wa Pengo. Moja kati ya viongozi wa juu waliokuwa upande waPengo ni pamoja na Spika wa Bunge Mh Samwel Sitta. Hili lilikuwa ni pigo kubwa kwa Serikali/CCM, hasa ukizingatia kuwa udini nao ukatawala Bunge na Serikali pia. Hapa ikaonyesha kuwa mahesabu ya Pengo yametimia.
so far unamwongelea Pengo siyo kanisa katoliki? au? ok, Unamaanisha wafuasi wa Kikwete walitumwa wakaupinge waraka lakini on the way wengine wakasaliti na kuunga mkono! Unamaanisha bunge letu limetawaliwa na udini? tena kwa kumuunga mkono Pengo for what?
We jamaa acha viwaraka vyako visivyoeleweka hivi. Unachofanya ni kutaka kutenganisha Watanzania badala ya kuwaunganisha. Kibaya zaidi wahariri tulionao wanaweza kuichapa hii gazetini kama ilivyo ukiwapelekea.
Ninakushauri uachane na chuki za kidini.