Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,367
- 2,404
Kimsingi mimi sitaki Taasisi, Jumuiya, mtu binafsi au NGO yeyote ile kutoa waraka au Muongozo juu ya kuwaelimisha wananchi kupiga kura. Nikifahamu wazi kuwa suala hili lipo very sensitive, bila ya kuangalia maudhui yaliyomo kwenye waraka au muongozo.Huu waraka sio mara ya kwanza kutolewa, ule wa mwanzo haukuleta matatizo kama inavyosemekana yatakuja kusababishwa nao. Zawadi kama ungetaka kubalance story ungezungumzia hatari ya MWONGOZO wa waislamu hata kama umekuja baada ya waraka wa wakatoliki. MWONGOZO huo umeji-isolate zaidi kwamba wafuasi wake watapiga "kura maslahi." Sasa linganisha na waraka ambao unataka watu wachague viongozi waadilifu! Usipobalance story hata kama una pointi nzuri namna gani huna tofauti na wale ambao unawalaumu kimakosa kwenye thread hii huku na wewe unayafanya yaleyale, kwa maana hiyo unajihukumu mwenyewe!
Katika hili suala la kwanza linalojitokeza ni nani kautoa huo waraka au muongozo. Lazima tufahamu kuwa kama Katoliki na waislam wanaweza kutoa waraka basi hata mtu binafsi akiwa na pesa zake anaweza kufanya hivyo. Hali kadhalika kwa NGO.
Hapa ni lazima ikumbukwe kuwa kila mmoja ana mawazo yake juu ya nani ni kiongozi mzuri. Kama waraka ungeandikwa na Mchungaji Mtikila angeandika waraka wake, basi ni wazi kuwa kigezo No 1 angeseama kuwa MAGABACHORI msiwachague kuwa viongozi. Tusingeweza kumkataza kwa sababu hivyo ndivyo afikiriavyo.
Ukiliona tatizo hili utakubaliana nami kuwa jukumu la kuwaelimisha wananchi kuwachagua wagombea waadilifu ni la serikali. Lazima tukumbuke kuwa hili ni jambo la kudumu na inabidi liwafikie wananchi wote kwa fedha ya walipa kodi.
Pamoja tuaendelea, tusikimbilie utatuzi wa harakaharaka. Dalili ya mvua ni mawingu.