Kulikumbatia kanisa sio jibu, hasa ukitaka kuweka mipango ya muda mrefu. Hii itampa kazi hata kama Mizengi Pinda akifanikiwa mwaka 2015.
Kinachotakiwa ni kanisa Katoliki kukubai kujitune, na kuelewa kuwa Tanzania ya Nyerere si sawa na hii ya Leo. Watanzania wamekwenda shule na wanaitumia. Isitoshe vyombo vya habari viko huru, hivyo vinafikisha habari kwa wananchi kwa urahisi zaidi.
Yale maelezo kuwa ukila na kipofu usimshike mkono hayapo tena. Angali, Rais Habyarimana ALIYEKUWA RAIS WA Rwanda alilikumbatia kanisa. Na leo vyombo vyote vya west vimeligeuka.
Jibu wanalo akina Pengo. Nchi hii ni ya wote, w aislam, wakristo, wahindu na wapagani.
Sina haja wala nguvu za kupambana na kanisa. Kwa sababu naamini kuwa kanisa lilikuwepo, lipo na litaendelea kuwepo. Hivyo kupambana na kanisa ni kuongeza matatizo. Ninachojitahidi kufanya kutafuta balance pale ambapo kanisa litaweza kuishi na jamii nyingine (wapagani, waislam, wahindu, materialist, wakomunist na serikali) kwa amani.Zawadi una kazi kubwa sana kupambana na kanisa wewe na watu wako . Kwanza naomba unijibu haya maswali .
1.Utata wa waraka uko wapi kiasi kwamba wewe na Kingunge na Kikwete muanze kuhaha namna hii ?
2.Je una uhakika kwamba issue hii ni ya Pengo na JK ? Waraka kauandika Pengo ? Na JK anakujaje kwa upande wa pili ?
Sina haja wala nguvu za kupambana na kanisa. Kwa sababu naamini kuwa kanisa lilikuwepo, lipo na litaendelea kuwepo. Hivyo kupambana na kanisa ni kuongeza matatizo. Ninachojitahidi kufanya kutafuta balance pale ambapo kanisa litaweza kuishi na jamii nyingine (wapagani, waislam, wahindu, materialist, wakomunist na serikali) kwa amani.
Sina mkononi hii kanuni bado na ndio maana nimeuleta huu mjadala hadharani, nikijua kwamba penye wengi ni rahisi kupata ufumbuzi.
Kuhusu masali yako mawili ningependa kuyajibu kama ifuatavyo:
1) a)Utata wa waraka unakuja pale ambapo, ili upate maudhui yake ni lazima uhudhurie kanisani
b) kuna watu hawana imani na katoliki, hivyo ni vigumu kuuamini waraka huo, wakifikiri kwamba hii ni danganya toto.
c) Italeta mvutano na waumini wengine, kitu ambacho mmeshakiona kimeanza kutokea kwa waislam kutoa wakwao baada ya kuuona ule wa katoliki. Hii si dalili nzuri
d) Serikali inahisi kuingiliwa katika kazi zake.
2) Issue ni ya Katoliki na Serikali. Pengo akiwa ni kiongozi wa katoliki ndiye mwenye kubeba mzigo wa katoliki, na kwa upande mwingine Kikwete naye ni kiongozi mkuu wa Serikali ndie mwenye kubeba mzigo wa Serikali.
Waraka umeandikwa kwa baraka zote za Katoliki (Pengo). Ni vigumu kumueleza mtanzania yeyote kuwa Pengo yuko nje ya barua hiyo. Na mpaka leo tamko la Pengo juu ya barua hiyo huwa na uzito mkubwa kuliko kiongozi/mtu yeyote yule.
JK, Kama utamaduni wa CCM ulivyo ndiye mtarajiwa kugombea nafasi hiyo ya uchaguzi mwaka 2010 kwa tiketi ya CCM. Hivyo barua hiyo inamhusu yeye moja kwa moja na sijui kama analala usingizi. Fikiria kama wewe ndiye ungekuwa mgombea!
Na Mkapa je??JK =
Richmond/Dowans
Buzwagi
EPA
Matumizi yasiyo na maelezo ikulu
Mikataba feki ya madini
Inflation ya kutisha
Na mengine kibao.
JK kafanya ufisadi mwenyewe na watu wakaujua na wakaanza kumsema. Hayo mengine ni ya kwako.
Mwinyi=
Loliondo
Stella
Dhahabu airport
ongezeko kubwa la deni
matumizi ovyo ya serikali
viwanja vingi vya serikali kuuzwa kwa wahindi kinyemela
wizi BOT na kuchomwa BOT
Vifo vya kutatanisha vya Katabalo na wenzake
Na Mkapa je??[/QUOTE]
OH, I was following this topic very well, and I was waiting for something to come; you trapped yourself; read my bolded letters above. You're in Christianity Versus Islam! This is a cultural imperialism which will haunt us and our generations!! Tunaishi kwa taabu sana na hatujui priority zetu ni zipi.
Asiyeweza kusahihishwa ni Mungu pekee! !
Na Mkapa je??
hata kama waraka wao ungekuwa mzuri kiasi gani nitaupinga mbaka kufa,wao ni watu wa dini hivyo wanatakiwa kuwaandaa watu kiroho,wawaelimishe waumini wao namna ya kuishi ili wafike mbinguni na si vinginevyo ndio maana hata yesu alikataa kushugulikia mambo ya duniani hata kama utawala wa kiyahudi ulikuwa mbovu ingawa watu walijua yeye ndiye mfalme lakini yeye alisema hana shida ya ufalme wa duniani yeye ni mfalme wa mbinguni,sasa nyie mnaohangaika na mambo ya dunia ndo biblia ya wazungu ilivyowaagiza hivyo?
Tatizo ni chanzo. Kama Kanisa katoliki lingesikia ombi la Serikali na kufuta waraka huo, hayo ya waislam yasingetokea.Mkuu Zawadi imekuwa nongwa katoliki kutoa waraka mbona waislam wametoa wakwao tena kwa mbwembwe kubwa pale mnazi moja.Waraka wa kanisa katoliki hauwezi kuzuiwa na wanasiasa wanaowafuga na kuwalelea mafisadi,waraka wa kanisa katoliki ni jibu sahihi kwa serekali iliyokuwa tayari kuvunja katiba ili kuanzisha mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC.
Asante kwa kuwa mkweli.
Nilijaribu kujenga hoja kama hii na kuomba ushahidi ndani ya Biblia kama dini ya Kikristo ina support waliyoyasema nikajibiwa eti mambo yanakwenda kwa common sense wakati kauli imetolewa na chombo cha dini.
Ila naomba nikukumbusha jambo moja.Katika dini ya Kiislamu kuna muongozo si tu wa kiroho bali hata wa kidunia na waislamu wameamrishwa kukemea na kupiga vita maovu mbalimbali hapahapa duniani pamoja na uovu wa ufisadi. Kwa hiyo ukisikia waislamu wanapiga vita ufisadi kumbuka kwamba hawa wameamrishwa kufanya hivyo ndani ya vitabu vyao.
Tena, asante kwa kuwa mkweli na muwazi.
Kuwazuia wanawake kuendesha gari na kuwa na nafasi kubwa including Elimu bora pia miongozi ya Uislam mmeamrishwa kufanya ?Kuvaa mabomu na kuua watu ambao hawataki sharia kwa kusema unapigania dini ya Mungu kumbe yote haya mmeamriwa ?Sikuyajua haya asante
Waraka wa Katoliki juu ya kuwaelewesha wapiga kura juu ya uchaguzi wa 2010, umeonekana kama kitendawili kwa serikali. Aidha baadhi ya viongozi wa serikali hawajaomuonea aibu Pengo pamoja na wafuasi wake kumuanika hadharani na kumuomba auondoe waraka huo. Lakini hasa kulikoni ndani ya kanisa Katoliki?
Nyaraka kaama hizo si ngeni kutoka toka kuanza chaguzi za vyama vingi. Lakini hii yaonekana yaonekana kukilenga chama tawala kwa muono wa Serikali ambayo i sawa na kusema CCM kwa sasa hivi. Kwa baadhi wameenda mbali zaidi na kuona kuwa, waraka huo si tu unailenga CCM, bali ni Rais Kikwete na washabiki wake serikalini kwa kuonekana kutolisikiliza kanisa katoliki kama ilivyokuwepo kwa akina Nyerere na Mkapa.
Wataalamu wa mambo ya siasa, wameeleza kuwa nguvu au ushawishi wa kanisa katoliki ndani ya serikali umepungua sana. Na hii imetokana na Kikwete kutaka kutenganisha kabisa dini na serikali kwa vitendo kitu ambacho kitakuwa kipya kabisa toka tukiwa Tanganyika na hatimaye Tanzania. Kwa maana hali hiyo ilirithiwa toka kwa wakoloni na kupewa baraka zote na mataifa ya magharibi.
Kikwete aliweza kuwashinda kidiplomasia akina Pengo na wafuasi wake, na ndio maana wakathubutu kutamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu. Rais Kikwete alijua wazi kuwa kuna gharama kubwa ya kulipa kwa kuungwa mkono na makanisa yote. Ni vipi alijiandaa na hilo, hakuna ajuaye isipokuwa waliyekaribu naye tu. Kwa vile yeye ni mkongwe wa siasa wa muda mrefu, ninahakika kabisa anaelewa Nguvu na ushawishi wa kanisa Katoliki duniani. Tena liko tayari hata kuleta vita pale ambapo linaona kuwa linapoteza umaarufu, kwa nia ya kujipanga upya.
Waraka umebabaisha toto kwa kusema imejikita katika kupinga ufisadi. Wasomi wanaona kama lugha nyepesi ya kidiplomasia waliyoitumia, lakini hasira zao ziliibuka pale Serikali ilipoanza mjadala wa OIC na Mahakama ya Kadhi. Hapa ndio ilikuwa mwisho wa urafiki kati ya kanisa katoliki na Rais Kikwete. Na hii ilimlazimu Pengo kufunga safari kwenda Vatikan na kupata ushauri toka kwa Papa. Pindi aliporudi tu, alimwita Waziri Membe na kufanya mazungumzo ya siri. Na hapo ndipo lilipochimbwa kaburi la Mjadala wa OIC na Mahakama ya Kadhi.
Hata hivyo kanisa katoliki halikurithika na hilo, ajenda kubwa ilibakia ni kumtoa madarakani Rais Kikwete kupitia wananchi (kura). Kwa katoliki hili ni suala la mpango wa muda mrefu (Long term). Hivyo si lazima Kikwete ang'oke mwaka 2010, bali hata hapo baadaye. Kwasababu nia si kumuondoa Kikwete peke yake bali ni yeye na wafuasi wake wote toka mikoani mpaka ikulu. Kazi amayo itafanyika toka kwenye vigango(ngazi ya chini ya uongozi wa kanisa) mpaka makao makuu ya katoliki.
Rais Kikwete kwa kulielewa hilo ikawatuma akina Kingunge na wafuasi wake kuupinga waraka huo hadharani. Bahati mbaya kukatokea makundi makundi ndani ya Serikali na Bungeni, huku baadhi wakiwa upande wa serikali na wengine upande wa Pengo. Moja kati ya viongozi wa juu waliokuwa upande waPengo ni pamoja na Spika wa Bunge Mh Samwel Sitta. Hili lilikuwa ni pigo kubwa kwa Serikali/CCM, hasa ukizingatia kuwa udini nao ukatawala Bunge na Serikali pia. Hapa ikaonyesha kuwa mahesabu ya Pengo yametimia.
Mpaka sakata hilo halijafika mwisho hatujui hatima yake. Lakini moja ni sahihi, kuwa michezo kama hii mwisho wake si mzuri na inaweza kuleta umwagaji damu. Ukimya wa KIngunge nyakati za hivi karibuni si dalili nzuri, kwani simba mwenda kimya ndio mla nyama.
Sina haja wala nguvu za kupambana na kanisa. Kwa sababu naamini kuwa kanisa lilikuwepo, lipo na litaendelea kuwepo. Hivyo kupambana na kanisa ni kuongeza matatizo. Ninachojitahidi kufanya kutafuta balance pale ambapo kanisa litaweza kuishi na jamii nyingine (wapagani, waislam, wahindu, materialist, wakomunist na serikali) kwa amani.
Sina mkononi hii kanuni bado na ndio maana nimeuleta huu mjadala hadharani, nikijua kwamba penye wengi ni rahisi kupata ufumbuzi.
Kuhusu masali yako mawili ningependa kuyajibu kama ifuatavyo:
1) a)Utata wa waraka unakuja pale ambapo, ili upate maudhui yake ni lazima uhudhurie kanisani
b) kuna watu hawana imani na katoliki, hivyo ni vigumu kuuamini waraka huo, wakifikiri kwamba hii ni danganya toto.
c) Italeta mvutano na waumini wengine, kitu ambacho mmeshakiona kimeanza kutokea kwa waislam kutoa wakwao baada ya kuuona ule wa katoliki. Hii si dalili nzuri
d) Serikali inahisi kuingiliwa katika kazi zake.
2) Issue ni ya Katoliki na Serikali. Pengo akiwa ni kiongozi wa katoliki ndiye mwenye kubeba mzigo wa katoliki, na kwa upande mwingine Kikwete naye ni kiongozi mkuu wa Serikali ndie mwenye kubeba mzigo wa Serikali.
Waraka umeandikwa kwa baraka zote za Katoliki (Pengo). Ni vigumu kumueleza mtanzania yeyote kuwa Pengo yuko nje ya barua hiyo. Na mpaka leo tamko la Pengo juu ya barua hiyo huwa na uzito mkubwa kuliko kiongozi/mtu yeyote yule.
JK, Kama utamaduni wa CCM ulivyo ndiye mtarajiwa kugombea nafasi hiyo ya uchaguzi mwaka 2010 kwa tiketi ya CCM. Hivyo barua hiyo inamhusu yeye moja kwa moja na sijui kama analala usingizi. Fikiria kama wewe ndiye ungekuwa mgombea!
[/COLOR]
Njia nzuri ya kuweza kuupamba uongo ni kusema 'wataalamu wa mambo ya siasa wanasema...' Kuandika nyaraka katika Kanisa Katoliki ni kitu cha kawaida sana kwani ni namna mojawapo ya kuwasilisha ujumbe kwa waamini wake au watu wengine wanaokubaliana na ujumbe huo.
Kanisa Katoliki linaamini hakuna imani kama hakuna 'responsible social action' (faith has to be inscribed in responsible social action) - ndiyo maana Kanisa linajishughulisha na yote yanayopiga vita ujinga, umaskini na maradhi na kushirki katika yote yanayoleta maendeleo ya watu na nchi. Katika kufanya hivyo, Kanisa linahubiri habari njema kwa watu.
Baada ya waraka wa Wakatoliki kuandikwa, watu wenye nia mbaya wameweza kupotosha maudhui yake makusudi lakini mtu mweye akili hawezi kupotoka anaona ukweli uko wapi. Binafsi sioni cha ajabu hapo. Ila naona huruma kwamba Watanzania wanalishwa siasa chafu na wanakubali wenyewe kuibugia.
Kati yetu kuna wanaotetea uovu unaolinyonya taifa letu kwa kulinda maslahi yao. Baadhi ya wazushi wanatoa tafsiri kwamba Kanisa Katoliki linataka litawale kila nchi. Hata kwenye waraka, walichosoma wazushi ni waraka/Kanisa Katoliki kuwagawa Watanzania kwa misingi ya dini.
Yaani, walichokisoma ndani ya waraka ni hicho tu! Tunaona pia katika maeneo mengine wazushi wapo: Mfano, matatizo ya mgodi wa North Mara waathirika wanaambiwa ndio walioharibu miundo mbinu ya maji yenye kemikali na pia walishalipwa hela zao zote ili wahame eneo hilo; wanaharakati wanapotetea wananchi wanaonyanyasika Loliondo, wanaambiwa na wazushi waache "ubazazi"; Hakielimu ilipotoa changamoto kwa Serikali ili iboreshe elimu miaka ya nyuma, wazushi walisema kama wanataka Hakielimu iwe chama cha siasa, wajiandikishe kama chama na siyo NGO...
Mbona Watanzania tunapenda kufanya 'intellectual masturbation'?