Pengo: Nchi imeoza!

Pengo: Nchi imeoza!

Wewe unayejidai una akili lakini unashindwa kuelewa kwa nini all of a sudden nchi imegawanyika kidini namna hii kwenye awamu hii kuliko wakati mwingine wowote! Nyerere pamoja na mapungufu yake yote aliwafanya watz kujiona kitu kimoja! Nilimsikia anayejiita Prof Lipumba kwamba kwa asili watz ni watu wa amani bila kujua kwamba amani iliyopo imetengenezwa na haijaja yenyewe!

Unajua UDINI ni sumu mbaya sana. Yaani umeshajiona ni mtu wa kukejeli UProfessor wa Lipumba kwa kuwa yeye ni musilamu na huamini kwamba muislamu can make a qualified professor. Ninatofautiana sana na siasa za Lipumba na anaposema watanzania ni watu wa amani haina maana kuwa anadhani kuwa amani watanzania wamezaliwa nao. Imejengwa tena kwa kumwaga damu nyingi sana kwa upande wa waislam na wakristo wote. Lakini kukejeli USOMI wa Prof Lipumba mwenye rekodi iliyochukua milongo kadhaa kuvunjwa UDSM na hata kule Princeton ni upofu uliojaa prejudices.. Hizi prejudices ndio zinafanya watu wa aina yako, upande wa wakristo na waislamu pia kujenga mitizamo ambayo imejaa USISI na UWAO.....

Mnakumbuka utanzania pale tu inapoendana na maslahi yenu binafsi....

Hatujafika tulipofika all of the sudden....Huu ni muendelezo wa safari ndefu ya kubomoa utanzania ambayo wazazi wetu na sasa sisi wenyewe tunaiendeleza kutokana na prejudices tulizojazwa vichwani kuona sisi ndio wenye haki zaidi ya wengine just because either we are waislamu ama wakristo..
 
Peleka udini wako huko uarabuni, elewa kuwa Tanzania haitakaa iwe nchi ya kiislam hata kama Kikwete akigeuza baraza zima liwe la waislam pekee.

Huo ndio usongo mliokuwa nao wa kuwa JMK ni muIslam na anendesha mambo vizuri kama alivyoigeuza nchi Mwinyi, mkamuandama mkashindwa na sasa mnamuandama JMK, hamtoweza. Na mashule atajenga na mavyuo anajenga na ataendelea kujenga na waIslam watasoma sasa bila kuwa na sababu ya kuchaguana. Janja yake panya sisi kwisha tambuwa!
 
Ama kweli tunakoelekea kubaya ... kama Omari naye amefikia pa kulinganisha waraka wa kikatoliki na kile alichofanya Ponda na wenzake wakati wa utawala wa Mkapa.

unapondea wanachoandika wenzako wakati na wewe unafanya kile kile tu walichofanya wenzako.

Kipi nilichofanya mimi? Nilipinga waraka kama ninavyopinga muongozo. Yote kwangu ni petrol kwenye moto unaofuka....

Ninchosema ni kuwa kama ilivyokuwa sawa kuwashughulikia kina Ponda then na pia ni sawa kuwashugulikia kina Pengo na Ponda sasa.....Wote wanacheza na misingi ya utaifa wetu whatever the justifications they have...Misingi ipo kwa ajili ya kutumika wakati wote haswa pale ambako tunadhani kuwa tuna haki ya kuivunja...

omarilyas
 
Huo ndio usongo mliokuwa nao wa kuwa JMK ni muIslam na anendesha mambo vizuri kama alivyoigeuza nchi Mwinyi, mkamuandama mkashindwa na sasa mnamuandama JMK, hamtoweza. Na mashule atajenga na mavyuo anajenga na ataendelea kujenga na waIslam watasoma sasa bila kuwa na sababu ya kuchaguana. Janja yake panya sisi kwisha tambuwa!

JK =

Richmond/Dowans
Buzwagi
EPA
Matumizi yasiyo na maelezo ikulu
Mikataba feki ya madini
Inflation ya kutisha
Na mengine kibao.

JK kafanya ufisadi mwenyewe na watu wakaujua na wakaanza kumsema. Hayo mengine ni ya kwako.

Mwinyi=

Loliondo
Stella
Dhahabu airport
ongezeko kubwa la deni
matumizi ovyo ya serikali
viwanja vingi vya serikali kuuzwa kwa wahindi kinyemela
wizi BOT na kuchomwa BOT
Vifo vya kutatanisha vya Katabalo na wenzake
 
Kipi nilichofanya mimi? Nilipinga waraka kama ninavyopinga muongozo. Yote kwangu ni petrol kwenye moto unaofuka....

Ninchosema ni kuwa kama ilivyokuwa sawa kuwashughulikia kina Ponda then na pia ni sawa kuwashugulikia kina Pengo na Ponda sasa.....Wote wanacheza na misingi ya utaifa wetu whatever the justifications they have...Misingi ipo kwa ajili ya kutumika wakati wote haswa pale ambako tunadhani kuwa tuna haki ya kuivunja...

omarilyas

Huwezi kulinganisha alichofanya Pengo na kile cha Ponda. Ni vitu na mambo mawili tofauti. Hakuna kokote kule Pengo alipochochoe wakatoliki wafanye fujo dhidi ya serikali yao kama alivyokuwa akifanya Ponda wakati wa Mkapa.

Come on Omari, unajua hili vizuri sana.
 
Hoja ya mimi ninayempinga Pengo ni kama ifuatavyo.

Pengo hakuzungumza kama raia wa kawaida kama wewe na mimi, amezungumza kama kiongozi wa dini.

Katika mazungumzo yake amekemea ufisadi-sasa ninakuuliza, katika Biblia wapi waumini wameamrishwa kukemea maasi na maovu?

Kuna faida gani ya kumsikiliza wakati Paulo ameshasema ndani ya Biblia kwamba sasa sheria haina nafasi mbele ya Mungu?Rejea aya nilizozileta.
Paulo amesema 'kupona (salvation)' hakutegemei vitendo wala utii wa amri Mungu, kupona mbele ya Mungu kunategea imani kwamba Mungu amekufa msalabani kwa ajili ya midhambi ya waumini, sasa hoja ya kufuata 'the law' inatoka wapi?

Of course common sense inasema corruption ina athari. Je, wewe uko tayari kukiri kwamba sheria za kikatoliki zinatungwa na common sense hata kama hazina support ya kitabu (Bible)?Kama ni hivyo, je hizo zitaitwa sheria za Mungu ama za binaadamu?Kama za kibanaadamu kwa nini zisiwe challenged?

Kama angekuwa Muislamu ningemuelewa kwa sababu kitabu cha Waislamu kinasema wazi kwamba Mungu hapendi ufisadi na mafisadi na pia waumini wa Kiislamu wanaambiwa wazi wazi wakatazane mabaya na kukumbushana mema.

Wapi ndani ya Biblia waumini wameamrishwa kukatazana mabaya? Tuanze na hapo ili tuone kama kweli kauli yake imekuwa motivated na Biblia ama maoni binafsi.

Tukikubali maoni binafsi yatangazwe hadhadhari na viongozi wa dini kwa kutumua kivuli cha dini ni sawa na kuwakubalia magaidi wafanye vitu vyao na kusingizia dini.

Punguza muda unaoutumia kwenye al arabiya labda utaelewa anachokisema Pengo.
 
JK =

Richmond/Dowans
Buzwagi
EPA
Matumizi yasiyo na maelezo ikulu
Mikataba feki ya madini
Inflation ya kutisha
Na mengine kibao.

JK kafanya ufisadi mwenyewe na watu wakaujua na wakaanza kumsema. Hayo mengine ni ya kwako.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. EPA ni madudu yaliyosukw, kukubaliwa na hata kutekelezwa wakati wa MKAPA na sio JK. Matumizi yasiyo na maelezo Ikulu ni ugonjwa wa miaka yote kwa marais wote. Mikataba feki ni mkataba wa BUZWAGI tu kati ya mikataba zaidi ya sita ya uchimbji mkubwa ndio umesainiwa wakati wa JK. Mingine yote ikiwemo ule wa unyama na aibu wa BULYANHULU ulikuwa wakati wa Mkapa.

Ni ujinga wa hali ya juu kuanza kutuhumu udhaifu wa URAIS kwa misingi ya kidini. Huu ni ujinga wa hali ya juu ambao unatufanya tuwe asusa za wanasiasa hovyohovyo kutupumbaza na kututumia kwa ajenda zao bila ya kuwapima kwa kutumia vigezo makini......

omarilyas
 
EPA ni madudu yaliyosukw, kukubaliwa na hata kutekelezwa wakati wa MKAPA na sio JK. Matumizi yasiyo na maelezo Ikulu ni ugonjwa wa miaka yote kwa marais wote. Mikataba feki ni mkataba wa BUZWAGI tu kati ya mikataba zaidi ya sita ya uchimbji mkubwa ndio umesainiwa wakati wa JK

Not on my opinion!
 
Punguza muda unaoutumia kwenye al arabiya labda utaelewa anachokisema Pengo.

Alichosema kinaeleweka na sikukihoji.
Nimehoji uhalali wa yeye kusema aliyoyasema.
Amri ipi ndani ya kitabu chake inachompa yeye uhalali wa kukemea maovu?
Kama una ushihidi bring it on badala ya kulaumu al arabiya.
 
Ninachokihofia kanisa katoliki linafadhiliwa na Mafias wanapesa nyingi na utajiri wa uchafu, Mungu aepushe wasije wakamhujumu rais wa nchi na nchi yenyewe. Pengo hakusita kuonyesha chuku na hasira yake kwa rais tumeshuhudia maneno yake makali ya utovu wa adabu na ufedhuli aliyoyatoa mbele ya rais Kikwete katika maziko ya askofu Mayalla kule Mwanza, alijuburi na kuonyesha kuwa anamdharau rais na kumfedhehesha mbele ya kadamnasi yeye na serikali yake kwa kuonyesha tu kutopigia magoti wito wa kanisa uliopewa jina la "waraka wa kanisa".
Tusubiri uchaguzi ujao tutaona vituko vya nuuni firauni kwa Pengo na watu wake wanajiita wapiganaji dhidi ya ufisadi wakati wakiwa ndani ya system ya kifisadi.
Mmeona wapi Ibilisi akamuongoza mtu katika ibada?
 
Huwezi kulinganisha alichofanya Pengo na kile cha Ponda. Ni vitu na mambo mawili tofauti. Hakuna kokote kule Pengo alipochochoe wakatoliki wafanye fujo dhidi ya serikali yao kama alivyokuwa akifanya Ponda wakati wa Mkapa.

Come on Omari, unajua hili vizuri sana.

Well, kama unajua socialpolitics za Tanzania ni wazi utang'amua kuwa wanachokifanya kina Pengo ni hichohicho lakini kwa kutumia maneno ya kuvutia na sio ya ghadhabu na makali kama ya kina PONDA...

Wote ni sawa tu kwani kwao wao kuchanganya DINI na SIASA ni sawa pale inapoendana na matakwa na maslahi yao na ni Haramu pale wengine wanapotumia kuwalenga wale wanaowaona watu wao kama walivokuwa wakifanya kina Ponda kwa Mkapa....Kumbuka hiki tunachokiita hapa WARAKA ukweli ni kuwa kiliandikwa ni ILANI.......ni waandishi ndio wamekuza neno waraka kupunguza makali yake.....I know the story behind WARAKA na najua kuwa halikuwa wazo la PENGO lakini ameubariki kuwaunga mkono RADICALS wa upande wake ambao hawana tofauti na kina Ponda.....

omarilyas
 
Alichosema kinaeleweka na sikukihoji.
Nimehoji uhalali wa yeye kusema aliyoyasema.
Amri ipi ndani ya kitabu chake inachompa yeye uhalali wa kukemea maovu?
Kama una ushihidi bring it on badala ya kulaumu al arabiya.

Pengo haitaji kitabu cha kiarabu ili kukemea uovu. Yeye kama mtanzania ana kila sababu ya kukemea ufisadi wa serikali ya Kikwete na mpango wa kutaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kiislam
 
Ninachokihofia kanisa katoliki linafadhiliwa na Mafias wanapesa nyingi na utajiri wa uchafu, Mungu aepushe wasije wakamhujumu rais wa nchi na nchi yenyewe. Pengo hakusita kuonyesha chuku na hasira yake kwa rais tumeshuhudia maneno yake makali ya utovu wa adabu na ufedhuli aliyoyatoa mbele ya rais Kikwete katika maziko ya askofu Mayalla kule Mwanza, alijuburi na kuonyesha kuwa anamdharau rais na kumfedhehesha mbele ya kadamnasi yeye na serikali yake kwa kuonyesha tu kutopigia magoti wito wa kanisa uliopewa jina la "waraka wa kanisa".
Tusubiri uchaguzi ujao tutaona vituko vya nuuni firauni kwa Pengo na watu wake wanajiita wapiganaji dhidi ya ufisadi wakati wakiwa ndani ya system ya kifisadi.
Mmeona wapi Ibilisi akamuongoza mtu katika ibada?

Kanisa halifadhiliwi na mafia. .... acha kashfa wewe au ndio mambo yale ya kusema misikiti inafadhiliwa na magaidi kama Osama?
 
Well, kama unajua socialpolitics za Tanzania ni wazi utang'amua kuwa wanachokifanya kina Pengo ni hichohicho lakini kwa kutumia maneno ya kuvutia na sio ya ghadhabu na makali kama ya kina PONDA...

Wote ni sawa tu kwani kwao wao kuchanganya DINI na SIASA ni sawa pale inapoendana na matakwa na maslahi yao na ni Haramu pale wengine wanapotumia kuwalenga wale wanaowaona watu wao kama walivokuwa wakifanya kina Ponda kwa Mkapa....Kumbuka hiki tunachokiita hapa WARAKA ukweli ni kuwa kiliandikwa ni ILANI.......ni waandishi ndio wamekuza neno waraka kupunguza makali yake.....I know the story behind WARAKA na najua kuwa halikuwa wazo la PENGO lakini ameubariki kuwaunga mkono RADICALS wa upande wake ambao hawana tofauti na kina Ponda.....

omarilyas

Hapana Omari,

wakatoliki walipomsifia Kikwete kuwa kachaguliwa na mungu, hakuna aliyesema kuwa wanachanganya dini na siasa. Leo wanapinga ufisadi na swala la mahakama ya kadhi ndio kila mtu macho yanamtoka.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. EPA ni madudu yaliyosukw, kukubaliwa na hata kutekelezwa wakati wa MKAPA na sio JK. Matumizi yasiyo na maelezo Ikulu ni ugonjwa wa miaka yote kwa marais wote. Mikataba feki ni mkataba wa BUZWAGI tu kati ya mikataba zaidi ya sita ya uchimbji mkubwa ndio umesainiwa wakati wa JK. Mingine yote ikiwemo ule wa unyama na aibu wa BULYANHULU ulikuwa wakati wa Mkapa.

Ni ujinga wa hali ya juu kuanza kutuhumu udhaifu wa URAIS kwa misingi ya kidini. Huu ni ujinga wa hali ya juu ambao unatufanya tuwe asusa za wanasiasa hovyohovyo kutupumbaza na kututumia kwa ajenda zao bila ya kuwapima kwa kutumia vigezo makini......

omarilyas

Omari,

Ni ujinga wa hali ya juu kumtetea raisi kwa misingi ya kidini (nikitumia logic yako hapa).

Pesa za EPA zilisaidia uchaguzi wa ccm na KIkwete. Yeye hakukataa ingawa alijua kila kitu kinachoendelea.

Buzwagi ni ya Kikwete hilo kila mtu analijua.

Mikataba ya madini ingebadilishwa kama Kikwete angekuwa na nia ila kwa vile yeye ni fisadi kama walioisaini basi ameshindwa kufanya lolote kuibadili.
 
Kanisa halifadhiliwi na mafia. .... acha kashfa wewe au ndio mambo yale ya kusema misikiti inafadhiliwa na magaidi kama Osama?

Well kaka nakubaliana nawe kabisa hapa. Lakini ukweli ni kuwa huu ni mfano wa miono ya wengi katika jamii zetu kuhusu dini za wengine...

Sasa katika hali kama hiyo ni dhahiri sio busara kuja na Waraka wala Miongozo. Mazingira tuliyonayo sasa sio ya kucheza na misingi wandungu....

omarilyas
 
Omari,

Ni ujinga wa hali ya juu kumtetea raisi kwa misingi ya kidini (nikitumia logic yako hapa).

Pesa za EPA zilisaidia uchaguzi wa ccm na KIkwete. Yeye hakukataa ingawa alijua kila kitu kinachoendelea.

Buzwagi ni ya Kikwete hilo kila mtu analijua.

Mikataba ya madini ingebadilishwa kama Kikwete angekuwa na nia ila kwa vile yeye ni fisadi kama walioisaini basi ameshindwa kufanya lolote kuibadili.

Ni kweli pesa za EPA zilisaidia uchaguzi wa CCM na JK lakini pia ni Mkapa ndiye aliruhusu na Balali ndiye aliyetekeleza na APSON Mwang'anda ndiye alisimamia.....

Wapi nimekataa kuwa Buzwagi imetokea wakati wa kikwete?

Ulichosema wewe ni kusainiwa na sio suala la kubadilishwa. Na kama kubadilishwa wapo walioanza kukubali kufanya hayo lakini the buck lies with yule aliyeridhia kusainiwa katika hali ambayo hata sasa imekuwa vigumu kuwashurutisha ama hata kuwabembeleza kubadilishwa.

Nimesema ni UDINI uliotumika kutoa hoja yako kwa kuwa umejaribu kuwahusisha viongozi waislam pekee kwa uozo wa nchi hii na kumuacha Mkristo. Je ulikuwa na maana gani kutotaja uozo wa Mkapa na hata kumpa JK uozo usio wake? Nilichoelewa ulikuwa unaonyesha kuwa viongozi waislamu ni wa kuharibu na wakristo ni wa kujenga...Hapo kwa kweli nina tatizo nako sana....huo ni mfano wa mawazo mufilisi yanayotupeleka kubaya watanzania.....na yapo katika pande zote, miongoni mwa waislam na wakristo kwa pamoja

omarilyas
 
Pengo haitaji kitabu cha kiarabu ili kukemea uovu. Yeye kama mtanzania ana kila sababu ya kukemea ufisadi wa serikali ya Kikwete na mpango wa kutaka kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kiislam

Pengo hakuzungumza kama raia, amezungumza kama kiongozi wa dini.
Kama hana 'backing' ya aliyoyasema ndani ya dini yake atakuwa na tofauti gani na wanasiasa?

Inakuwaje mtu ahubiri kwa waumini wake kwamba utii wa sheria hauna faida mbele ya Mungu na hapohapo ahubiri usafi?
 
Back
Top Bottom