Mi nadhani, baadhi ya watu wanataka tu kumchafulia jina Kardinali Pengo. Kardinali ni kiongozi wa kanisa na yeye anafuata maadili. Kila mtu anajua kuwa ufisadi si kitu kizuri. Kila mtu anajua madhara ya ufisadi ni nini. Sasa mnaolipinga kanisa katoliki katika suala la kupambana na ufisadi, mnatoa "alternative" gani? Maana mnapinga tu lakini hamna cha maana mnachokizungumzia kuhusu ufisadi, ila mnapinga tu kwa sababu argument ya ufisadi imetoka kwa kanisa katoliki. Kama mnafanya hivi nadhani hamna pointi ya maana. Je mna chuki binafsi na kanisa katoliki kama yule mbunge aliyeanzisha mada hii bungeni?
Hoja ya mimi ninayempinga Pengo ni kama ifuatavyo.
Pengo hakuzungumza kama raia wa kawaida kama wewe na mimi, amezungumza kama kiongozi wa dini.
Katika mazungumzo yake amekemea ufisadi-sasa ninakuuliza, katika Biblia wapi waumini wameamrishwa kukemea maasi na maovu?
Kuna faida gani ya kumsikiliza wakati Paulo ameshasema ndani ya Biblia kwamba sasa sheria haina nafasi mbele ya Mungu?Rejea aya nilizozileta.
Paulo amesema 'kupona (salvation)' hakutegemei vitendo wala utii wa amri Mungu, kupona mbele ya Mungu kunategea imani kwamba Mungu amekufa msalabani kwa ajili ya midhambi ya waumini, sasa hoja ya kufuata 'the law' inatoka wapi?
Of course common sense inasema corruption ina athari. Je, wewe uko tayari kukiri kwamba sheria za kikatoliki zinatungwa na common sense hata kama hazina support ya kitabu (Bible)?Kama ni hivyo, je hizo zitaitwa sheria za Mungu ama za binaadamu?Kama za kibanaadamu kwa nini zisiwe challenged?
Kama angekuwa Muislamu ningemuelewa kwa sababu kitabu cha Waislamu kinasema wazi kwamba Mungu hapendi ufisadi na mafisadi na pia waumini wa Kiislamu wanaambiwa wazi wazi wakatazane mabaya na kukumbushana mema.
Wapi ndani ya Biblia waumini '
wameamrishwa' kukatazana mabaya? Tuanze na hapo ili tuone kama kweli kauli yake imekuwa motivated na Biblia ama maoni binafsi kwa kivuli cha dini. kama ukituthibitishia amri hiyo ipo ndani ya Biblia utaweza kuanza kujenga hoja kwamba anatimiza matakwa ya dini yake.Lakini usisahau kwamba utalazimika kumjibu Paulo vilevile aliyesema 'amri za Mungu kwanzia sasa hazina nafasi'.
Tukikubali maoni binafsi yatangazwe hadhadhari na viongozi wa dini kwa kutumua kivuli cha dini ni sawa na kuwakubalia magaidi wafanye vitu vyao na kusingizia dini.