Pengo amtolea uvivu Kikwete

Pengo amtolea uvivu Kikwete

Wakatoliki walishamuambia Kikwete 'njoo utukamate kama tunahusika'.

Wakaongeza kuwa ukimya wa Kikwete kutowakamata wauza madawa ni usaliti.
exactly mkuu, mtu anayevunja sheria lazima ashughulikiwe. Haijarishi yeye ni askofu au padri au nani. Rais hatakiwi kudebate na mtu kwenye uvunjifu wa sheria. Mesage gani anatupa anavyoenda kulialia mbele ya watu bila kuchukua hatua? Is this country a failed state?
 
Nitoe shukrani zangu za dhati kwa msimamo wa kanisa katoliki. Tunaomba msikate tamaa kuibana serikali mpaka itoe hayo majina hadharani. Wao wanafikiri wananchi hawajui wauza madawa ya kulevya, mbona wanajulikana tu.

Kwa hali iliyopo inaonyesha serikali inataka kujificha kwenye kivuli cha kanisa na inadhihirisha hii nchi inaendeshwa na hawa wajamaa. Tunasubiri jibu la serikali kuhusu hii barua watuambie, au wawachukulie hatua hao wanaouza hayo madawa. Hatuhitaji tena malumbano tunahitaji vitendo zaidi, kanisa limeshasema linatoa ushirikianao popote watakapoona panahusika.

Sasa kazi kwenu nyinyi wauza makesi kwa wananchi tulisha wazoea. Mungu atatuletea mtu wakusimamia haki ya watanzania siku moja.
 
well done kanisa ,
serikali inakuwa legelege sana walisema maaskofu mara sasa vijana anyway si wawataje?
 
Ushauri, hii video si ioneshwe kwenye vyombo vya habari i.e. TV ili wananchi wote tuione na tutafakari,
La sivyo serikali ni waoga kwa waza madawa ya kulevya au wao ndi washiriki wa biashara hii,
 
baba Ridhi ni extrovet si wakuumiza nae kichwa. ndio maana hata issue ya jairo imekuwa hivi. anatenda halafu kufikiri baadae
 
Well done!! Hili la huyo mtoa mada Ghost kwenye semina za wabunge mimi nadhani ni kamechi tu kakuigiza ili amkomboe mkuu wa nchi na aibu ya kuropoka kule songea bila ushahidi... huku ni kupakana matope kusikuwa na sababu ila kwa wenye akili tumeshaelewa nini kinaendelea hapo.
 
pale bakwata wametajwa tu isionekane kuna ubaguzi,kwanini mfano ukawa wa kuwagusa wakatoliki pekee? Sijui tunapelekwa wapi! Kama wapo hata kama ni pengo si wakamatwe? Tuache porojo wakuu
 
Serikali haiwezi kuwaweka hadharani wauza madawa kwani kuna viongozi na matajiri ambao nimaswahiba na viongozi wataumbuka ndio mana hawataji majina. Kama kweli Serikali inapambana na mihadarati iwataje si Kanisa Katoliki limewapa ruhusa yakuwataja wanaogopa nini?
 
Are we really sincere in fighting against drug trafficking war? Otherwise we should shut up and remain silence forever. Sheria ziko wazi, kwanini hazitumiki kama mkatoliki au bakwata wamejihusisha na biashara ya madawa ya kulevya? Vinginevyo ni yale yale tuliozoea ya hadithi zisizo kwisha, hata kwenye mambo ya hatari kabisa na uwepo wetu

Tunataka sheria ichukue mkondo wake..hawa watu wanatuharibia SANA kaka na dada zetu.
 
CCM wanahaha tuu iyo ni gear wanayoitumia kulipoza kanisa ili wasiwe wanaikemea serikali kwenye maovu yao!
 
hawawezi kulipoza kanisa,kanisa ni zaidi ya pengo,kilaini n.k hakuna wa kulijenga wala kulibomoa kwakuwa hakuna aliyelijenga hivyo unashindana na kitu(naogopa kulitaja bure!) wanasayansi huita super natural power! Je unaweza kuipoza super natural?
 
Nitoe shukrani zangu za dhati kwa msimamo wa JK. Asikate tamaa kuibana kanisa na misikiti wazidi kuona aibu na hatimaye kuacha (kama kweli wanafanya hiyo biashara chafu).

Kazi ni ngumu ... kila mtu anajua institutions hizi za makanisa ni za nchi kubwa kubwa za kimagharibi na kupambana nazo lazima utembee kwenye mstari mwembamba sana! Kumbukumbu ya watu wa mungu kubaka watoto bado mbichi (kanisa lilikana sana hili!) na lisemwalo hapa lipo.
 
Hivi ni sababu gani zinampelekea Kikwete kutomwita nyerere baba wa taifa?Huwa anamuita hayati mwalimu nyerere
Makongamano ya kiislam yaliyofanyika Tabora, UDOM, Mwanza na Arusha mapema mwaka huu na CD zake kuenenea kona zote Tanzania watoa mada walisema wazi Nyerere si baba wa taifa bali ni baba wa ukristu. Kikwete alitajwa kama mshiriki na mwezeshaji wa kongamano la waislam hivyo hawezi hata siku moja kumwita Mwalimu Nyerere baba wa taifa na aamini hivyo. Kila siku atamwita "Mzee Nyerere" ingawa kimoyomoyo ataita "baba wa ukristu na muasisi wa mfumo kristu"
 
hawawezi kulipoza kanisa,kanisa ni zaidi ya pengo,kilaini n.k hakuna wa kulijenga wala kulibomoa kwakuwa hakuna aliyelijenga hivyo unashindana na kitu(naogopa kulitaja bure!) wanasayansi huita super natural power! Je unaweza kuipoza super natural?

That is true. Wanasayansi wanasemaSuper Natural Power wakati wataalamu wa mambo ya dini wanaiita Supreme Being. Hii ni kitu kingine huwezi cheza nacho.
 
Hapa kwel tuna serikal?
Kama mpaka mikanda ipo, nin kinasubiriwa?
Ushahidi gan tena?
Kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya wana kaz gan?
Mbona wanasita kuwachukulia hatua?. Nahis watakuwa wanajuana.
 
Viongoz wetu wa BAKWATA tunasubiria kauli zenu. Au mmekubaliana na yanayosemwa?
 
Viongoz wetu wa BAKWATA tunasubiria kauli zenu. Au mmekubaliana na yanayosemwa?
Angeongea hayo mtoto wa mkulima kwa kuwanyooshea BAKWATA kidole angeonja joto ya jiwe, lakini latoka kwa mtoto wa nyumbani wakati anajua namna ya kuwapoza yameshaisha.
 
wana JF hafai kulumbana kidini humu au kutukanana kwa dini zetu nadhani kiimani tutakuwa tunafanya dhambi,ila moja tutambue c wakatoliki tuu wametajwa humu vilevile na ndugu zetu BAKWATA wemetajwa bila hata kutoa sababu za msingi,ukiangalia watu wote wanaoenda nchi za nje huwa wanakaguliwa sasa wememkamata nani? hivi kusema kuwa wanaoenda walioenda kuhiji walikuwa na madawa ya kulevya mwaka 2008 kwanini sasa unasema leo? Na kwa majina yapi na idadi gani? sasa wanataka kuharibu imani zetu cc tunasema SERIKALI KAMA INATAKA PROPAGANDA IKAFANYE HUKOHUKO GAMBANI VINGENEVYO YA LIBYA,MISRI,TUNISIA yakitokea Tanzania nitakuwa mstari wa mbele
 
Viongoz wetu wa BAKWATA tunasubiria kauli zenu. Au mmekubaliana na yanayosemwa?
Mkuu wangu Bakwata waseme nini?.. kama kuna watu wamekamatwa na mkanda upo umeonyesha wauza unga, wao wanatakiwa kujitetea kitu gani... Jamani tuwe wakweli hivyo vyombo vya dini siku hizi ni biashara tupu hakuna cha Saint kamba tupu..kote huko unga na biashara haramu kwa kwenda mbele sii kanisani wala misikitini..Uliona wapi mtu mwenye msikiti au Kanisa ndio hutajirika! - Yaani kanisa au msikiti imekuwa biashara - kwa kuuza kitu gani?
 
Back
Top Bottom