jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,375
- 25,453
Mzee wangu Mkandara,nisome vyema kwenye bandiko langu liliopita.Na bado naona umerudia kosa lile lile,pengine labda ni kwasababu postings ni nyingi na kusoma post smtime kwa umakini it takes time.Haya umeona sasa! wewe imekuwaje utoke kwenye mada hii unakuja na video iliyoletwa na Mkristu mwingine ili ijewe!...Je, nikikuletea video za wachungaji wa Kikristu kina Jimmy Swagat wanaotukana Uislaam na kuita dini ya mashetani - utasema nini?..Sisi Waislaam hatuna muda huo na hakika nyie ndio mnazo video nyingi zinazoukashifu Uislaam lakini huwezi kuta video inayokashifu Ukristu isipokuwa tunakashifu matendo maovu kama kuuza unga, pombe, kula nguruwe n.k... Sasa maadam wewe pengine unawajua wakristu anaouza unga, unafikiri Waislaam wanawazungumzia Wakristu kumbe sivyo - unga ni haramu pande zote mbili..
Anyway nilikuwepo sasa hivi nawaageni endeleeni na mjadala na nawaombea kila la kheri lakini kumbukeni usia wangu.. Mnaiweka mahala pabaya sana Chadema..
Hapo kwenye bold naona umeshindwa kutofautisha kati ya sheria zinazotawala nchi vs zile zinazotawala dini.Wakati kula nguruwe ni uovu ama kosa kwa mujibu wa dini,issue ya madawa ya kulevya certainly ni tofauti.Hayo ni illegal kwa sheria zetu za nchi na mtu anayekula nguruwe hawezi kuchukuliwa hatua sawa na yule anayeuza ama kubwia unga kwa mujibu wa sheria za nchi.Na kudeal na issues hizo ni kwa namna ya tofauti.Sijui kama umeona tofauti hapo mkuu?
Na ndiyo maana nikasema hapo nyuma kuwa,wale wanaochochea udini ni wale wanaounganisha na kufananisha makosa yanayofanywa under mamlaka ya dini ama dhehebu flani vs yale yaliyoko chini ya mamlaka ya serikali pale yanapofanyiwa kazi/uchunguzi.
Katiba ni sheria mama.Sote tunaishi kwa kufuata katiba bila kujali dini zetu.Hilo ndilo la msingi.Issue hii inagusa katiba kwasababu inamgusa rais,serikali yake na vyombo vyake vya dola.Wakati sheria hizo za dini zina govern hayo madhehebu husika pekee.Hii ni iisue yenye maslahi ya kitaifa.Wote bila kujali dini tunapingana nayo.Kula nguruwe hakuathiri maslahi yoyote ya taifa.
Kwa hiyo tusijikute kama crabs in a bucket kwa kuingizwa mkenge na wanasiasa wenye personal agendas.Nchi yetu inahitaji more than this b.s especially these times.
Mkuu Mkandara naamini kabisa kuwa Mh Rais kalianzisha hili makusudi kwasababu anajuwa kuna wanaoendeshwa na emotions.Hiyo ni political tactic.Lakini ukweli ni kwamba badala ya kulishughulikia tatizo hilo,ameamua kulipiga dan dana na kulitumia kimaslahi ya kisiasa.Malumbano ya nini rais mzima?Unawajuwa wauza madawa,wakamate na si ngonjera!Huo ndo ukweli.Route aliyoichagua inaonyesha mawili.
1)Either anawaogopa wauza madawa(listi ni kubwa zaidi ya hao viongozi wachache wa dini)Ina wezekana anawatumia hao viongozi wa dini kama karata ya kuizima issue hii(inawezekana kuna ambao wako protected)
2)Inawezekana pia anawaogopa hao wauza madawa maybe walichangia harakati zake za kuwania urais.(Ili kuwalinda,wamekamata hao vibaka wachache na kuipakazia dini nzima ya ukristo/ukristu kuwa ni ya viongozi wauza madawa.Hili nalo pia litawafanya wafunge mdomo ama ku neutrealize isue nzima.
Under both scenarios.Mh Rais ataumbuka eventually kufuata siasa za kipuuzi.