Pengo amtolea uvivu Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo amtolea uvivu Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkodoleaji, Aug 14, 2011.

 1. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fredy Azzah na Ibrahim Yamola

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema Watanzania wanasherehekea miaka 50 ya uhuru huku kukiwa na makundi ya viongozi na vigogo nchini wanaojineemesha kupitia migongo ya wananchi bila kujali wanawasaliti, wanawaongezea umaskini na kuwaua.

  Kardinali Pendo alilaani akisema: "hayo yamekuwa yakitendeka kinyume na misingi iliyoainishwa na waasisi wa taifa wakati wakidai uhuru kutoka kwa wakoloni ambapo walitamani kujenga Tanzania yenye utukufu.

  Kardnali Pengo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya Tanzania, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme Parokia ya Tabata.

  "Waasisi wetu walipokuwa wanapigania uhuru wa taifa hili, lengo na maono yao yalikuwa kutengeneza taifa lenye utukufu, lenye kutawala mataifa mengine …," alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

  "Katika miaka 50 tunayoikamilisha, kumekuwa na mafanikio na changamoto nyingi tu, inabidi tujipange ili watakao kuja kuadhimisha miaka 100, au hata miaka 25 ijayo wasije wakasema afadhali wakati wa mkoloni."

  Katika ibada hiyo ambayo pia ilitumika kuliombea taifa, Pengo alisema wakati wa kupigania uhuru lengo ilikuwa ni kulifanya sehemu salama na bora ya kuishi watu wake.

  Kardnali Pengo alitahadharisha akisema: "Lakini sasa Taifa lina makundi ya watu wasaliti, wenye ubinafsi na ambao wako tayari kujitafutia utukufu hata ikibidi kuwakandamiza na kuwaua wenzao".

  Kwa sababu hiyo akawataka Watanzania kutafakari katika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, wajiulize wamekuwa wakijitafutia utukufu binafsi au ule ulioasisiwa na taifa wa wananchi wote kufaidi matunda yake.

  Kwamba, tumepata utukufu wa aina gani?" Alisema Kardinali Pengo na kuonya; "Baadhi ya watu wanapata utukufu bila hata kujali kama watu wengine wanakufa, jambo ambalo ni hatari kwa taifa."

  Kardinali Pengo aliwaonya waliopewa dhamana ya uongozi na kutumia nafasi hiyo kujitajirisha, kuwa ni usaliti kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.

  Tuhuma za dawa za kulevya
  Katika hatua nyingine, Kadinali Pengo, alilaumu mtindo wa viongozi wa Serikali na dola kutotaja hadharani majina ya watu wanaowatuhumu kuhusika na biashara ya dawa za kulevya huku wakiendelea kulalamika kuwa wapo na wamewakamata.
  Alisema hali hiyo haionyeshi nia yao ya dhati katika kupambana na biashara hiyo haramu.

  Akikumbushia kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete wakati wa Sikukuu ya kumwekwa wakfu na kumsimika Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini huuza dawa za kulevya, alisema alitakiwa kuwataja.

  Kardinali Pengo alisema kitendo cha Rais Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi waliojitokeza kuzungumzia suala hilo huku wakisema hawawezi kuwataja kwa majina, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.

  "Haiwezekani mtu mkubwa tu, wala siyo mdogo kuja katika eneo la Kanisa la Katoliki, kukiwa kumejaa Maaskofu kutoka karibu nchi nzima, unasema maneno haya halafu unasema, siyo nyie ni viongozi wa makanisa madogomadogo," alilalamika Kardinali Pengo.

  Aliongeza kwamba: "Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa uje kuyasema maneno hayo katika eneo la Kanisa Katoliki."

  Akasisitiza: "Mapadri, watawa; naomba tujiangalie kama sisi tunaguswa na hii kauli, kama haitugusi tumshukuru Mungu, lakini ni vyema hawa watu wakatajwa.

  Hata kama ni mimi njoo uniambie, ukisema hunitaji kwa sababu ni kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa."

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi, aliwahi kuliambia Bunge hivi karibuni kuwa Serikali ina safari ndefu katika kufanikisha mkakati wa kukomesha biashara hiyo haramu.

  Alisema Serikali inaamini kuwa vita ya kuwakamata wanaojihusisha na dawa za kulevya ni ngumu lakini akasisitiza kuwa anaamini mwishowe watashinda uhalifu huo.

  Lukuvi alisema mbali na kuwataja hadharani baadhi ya viongozi wa dini, imebainika kuwa wana mtandao mkubwa.

  "Hapa sio kuwataja tu maana kama ni kuwataja tayari Serikali ilikwisha wataja na watu wanajua kuwa kiongozi wao ni yule Askofu wa Nigeria, lakini hapa suala ni namna ya kupambana na kuwajua wengine,'' alisema Lukuvi.

  Hata hivyo, mara baada ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), ilikuja juu na kumpa saa 48 za kuwataja hadharani viongozi wa madhehebu ya dini wanaohusika na biashara hiyo haramu.

  "Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na Serikali," alisema Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa.

  Rais Kikwete alijibu wito huo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwamba, viongozi wa dini siyo malaika kwa hivyo wasijivune kuwa hakuna miongoni mwao ambao ni wahalifu.

  Source: Gazeti la Mwananchi

  My take:
  Kweli Pengp amesummarise vizuri behaviour za Kikwete kuwa ni msaliti maana kuna matukio mengi yametokea na hajatoa kauli wala kuchukua hatua zozote sasa kama huu si usaliti kwa wananchi ni nini?
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  kaul thabit hujenga nchi za kisanii hubomoa,kiongoz awe mfano kwa kutenda mema kwa awaongozao.yaelekea jk huwa anaota aongeapo ndo mana awal 2 twayaona mabaya meng na bado yaja makubwa zaid
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwanini asiliseme hilo kwenye kanisa la lutheran, pentekoste, anglikana, victor gospol church aende akaseme kanisa katoliki? Na ni kwanini akiambiwa awataje viongozi wa dini wanaouza madawa hawataji? HUYU ****** NI MNAFKI SN NIA YAKE ILIKUA KULICHAFUA KANISA KATOLIKI, KUMBUKA DR SLAA NI MKATOLIKI ANAANDAA MAZINGIRA YA KUMTENGENEZEA KESI.
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Sema baba,wape ukweli but kesho utasikia viongozi wa dini wanaingilia siasa.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama yeye Kikwete kashatajwa kuwa ni fisadi anawaongopa nini kuwataja viongozi wa dini kuwa furani anauza madawa ya kulevya huu ndiyo tunauita ulegelege....
   
 6. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hv mkuu wa kaya kasharudi kutoka Namibia?
  Natamani angeyasikia yale aliyokuwa anasema Pengo jana,lakini nafikiri atakuwa amesoma magazeti ya leo.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Asante kardinal Pengo, serikali ya kikwete imejaa uzushi mtupu. Rais anaropoka utadhani yupo kijiweni! hizi sasa ni chuki dhidi ya wakristo
   
 8. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,040
  Likes Received: 7,484
  Trophy Points: 280
  The great thing about Polycap Cardinal Pengo is you cant mess sup with him....He is the Straight shooter, huwezi ukaenda kwake halafu unaanza kumuongelea methali, au mafumbo ya kwenye khanga, he is not of that type and its not his fault thou, cause thats not how we were trained .....
  Hatuna muda wa kuzunguka, tupo nyuma sana, kwa kuanza kuzunguka ni kama kuwajengea watu tabia ya kuishi kwa fununu, badala ya kuwa na uhakika, tuna mambo mengi ya kufanya and we still have so many batlle before us, hivyo its worthy, to start shooting straight to the point and serve our prcious little time and energy we have for other activities.....
   
 9. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,292
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Haya sasa tunasubiri tamko toka BAKWATA. Tuone upande wa pili nao wanasemaje kuhusu jambo hili.?
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ngoja wapambe wake watajibu....
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Swaumu kali tusubiri labda baada ya futuru au daku la saa 12 Alfajiri
   
 12. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  "Jk janga la kitaifa"
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwanini Pengo ilimuuma ile kauli ya Kikwete? au ni mmoja wa washukiwa.

  lakini siku hizo hana uzito wowote kulinganisha na Wakati za Nyerere.
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Huu ndio ujasiri wake Jakaya Mrisho Kikwete rais wa awamu ya nne, Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
   
 15. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa kama Kanisa lilitakiwa kuwa daima kimbilio la wenye shida lakini mpaka tumefika huku,sio kuwa hawawajui baadhi ya waumini waliotufikishia hapa tulipo kiasi kuwa Viongozi wanafikia kusema vijembe ambavyo kwa hadhi ya kanisa la Roman kupewa kijembe na Rais ni Salam kuwa ndiyo Tanzania mpya hiyo ambayo illiasisiwa na vijana wa Mwalimu Nyerere kutoka kuwa Taifa kubwa lenye uwezo wa kusemea mataifa madogo mpaka kuwa Taifa ambalo watu wake hawana hukika wa mlo wao wa siku.

  Kardinali kaongea lakini ajue doa la tamko la Rais ndani ya Kanisa la Roman alitofutika kwa watu wote makini ndani na nje ya Nchi.Manake yeye kama Rais ana vyanzo makini na vya uhakika kumpa taarifa sahihi.Hivyo aliyoyasema kama Rais ni picha ambayo wenye uelewa na wajuzi wa matamko wanakili ujumbe ulifika.

  Japo sio sahihi kwa kiongozi Mkuu wa Nchi kutoa tamko la aina hiyo mbele ya kadamnasi kubwa,kwani lilikuwa ni tendo la uamuzi wa Rais kukutana na Kardinali Pengo na kumpa listi yake ya wale ambao taarifa zimemfikishia kuwa wanahusika na biashara ya madawa ya kulevya na kumwambia Kardinali awajibike nao kiutu uzima.Hakika Kardinali kwake angempa msaada mkubwa sana.

  Lakini kitendo cha kuweka wazi kisha kuombwa awataje na atimae kutoa listi ya watu wengine kutoka kwenye makanisa mengine kidogo ni mchezo hatari kwa zama hizi mpya ambayo watu wengi sana wana taarifa tofautii tofauti nyingi,na wengi watapigia mstari kitu ambacho chaweza kuwa ndio ama sio kweli.Ila kwa kuwa yamesemwa na mtu anayeaminika kwa jamii madhara yake ni makubwa sana.

  Ila bado ni mapema kanisa nalo kuludisha imani yake kwaa umma wa waelewa wafanye yote yawezekanayo kuonyesha kuwa yaliyosemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa Viongozi wa Kanisa hilo kubwa kwa waumini sio kweli na kuwa waendelee kusisitiza wanataka Rais aombe msamaaha kwa kauri hiyo.

  Mengi yatakuja natumaini sasa niwakati ule ambao Mungu anataka Ukweli uwekwe ili Taifa liende kwenye kusudio la Mungu kuwa Taifa kiongozi wa Mataifa mengine kama ilivyokuwa zamani na Taifa lenye watu wenye ustawi na wenye kuishi kwa furaha daima.

  Mungu ibaliki Tanzania Mungu wabaliki Watanzania.Ila yatakuja mengi kwa sababu zama huwa hazizuiliki.
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hongera sana Pengo nakujua wewe si mnafiki kijiko inakiita kijiko ndo maana umemtaja Kikwete live bila kuzunguka.
   
 17. M

  Mwenye Hasira Member

  #17
  Aug 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli MR President ni mnafki sana ndio maana anapenda kusafiri kuepuka majukumu na kutoa maamuzi ya Nchi yanamshinda. Kusema kwamba sio nyie ni viongozi wa dini ndogondogo maana yake nini kama sio mchonganishi ndio maana alikimbia Monduli sababu ya uchonganishi huu huu afadhali this time hajaandika barua ya uchonganishi maana ndio zake.
   
 18. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160

  naam mkuu, hapo umenena...,
  Ngoja tuwasikie watasema nn khs hiyo kauli ya Pengo...!,
  its ma hope that, na wao watakuja na kauli thabiti, safi na komavu ya kuijenga nchi yetu....!
   
 19. Jidulamabambase

  Jidulamabambase Member

  #19
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais Muongo na anaweza kuitumbukiza nchi katika vita kwa kauli kama hizi, bahati mbaya Waziri Mkuu wake pia ni muongo. Wakati umefika kwa Rais kuwataja anao wafahamu la sivyo aombe msamaha kwa viongozi wa dini. Ajue tunawaheshimu sana hao viongozi wa Dini!
   
 20. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pengo uzito wake upo palepale.......usitake kumfananisha kabisa na wale jamaa zenu wa kulalama kila siku na kutoa matamko yasiyoeleweka!
   
Loading...