JMushi1,
Mkuu hapana utanisamehe sana, sitokubaliana na wewe ktk hili kwa sababu hata mimi nataka sana JK aondolewe madarakani lakini sio kwa njia hii ya Udini na ufitini.. Hapa inaonyesha wazi UDINI wanaojaribu kuupandikiza hawa jamaa zangu na kama unaweza rudia kusoma hoja za watu humu.. It's all about JK being a Muslim na Pengo Mtukufu wa kikristu kamtolea uvivu JK ktk jambo ambalo halipo.. That is the deal.
Ukweli upo wapi? rudia kasome kichwa cha mada hii..Soma malalamiko ya Pengo with an open mind, halafu tazama maelezo ya Lukuvi akiwa bungeni utaona hapakuwa na sababu kabisa ya malumbano.. Hii mada mkuu wangu hadi sasa hivi imetazamwa na watu zaidi ya 7,000 kwa sababu gani kama sii Majibu ya Kardinali Pengo!.. na tunaendelea kulumbana sababu gani? kama sii hamtaki kuamini Pengo kafanya PIA makosa.. wamefikia hata kuhalalisha Unga ktk vikao vya kidini ati visizungumziwe.. Hapana mkuu wangu, hata sisi tutumie logic ya kwamba haitakuwa vizuri kama JK angetaka kuhalalisha biashara ya Unga ktk jukwaa la dini yoyote lakini sii kuwakanya vionmgozi wanaofanya vitu hivyo waache! where else angeweza kuupeleka ujumbe kama huu kwa viuongozi wa dini kama sii ktk majukwaa ya dini..
Haya utasikia kwa nini liwe jukwaa la Kikatoliki, I mean jamani toka lini tunakuwa na utengano kwa sababu ya madhehebu? Hivi kweli rais akizungumza swala la Ukabila akiwa Mwanza basi kawatukana wasukuma.. kwa nini asizungumzie akiwa Chalinze?.. Noo mkuu wangu ubaguzi tunauanza sisi wenyewe..
Kwa kila tunachomlaumu JK ndicho Pengo kakifanya lakini yeye sii mnafiki kwa sababu gani?.. kama sii utukufu wake kwa wakristu. JK asizungumze maswala ya unga ktk sherehe za kikristu, Kardinali anakuja ktk jukwaa la dini kama lile analopinga yeye kuzungumzia maswala ya wauza unga na JK wakati angeweza kabisa kwenda Ikulu na kuonana na rais na tusingekuwa namalumbano hapa JF..
Kwa nini JK haruhusiwi kuzungumzia hayo jukwaa la wakristu, sipati jibu zaidi ya mila na desturi ambazo JK hazijui. Kwa nini Pengo anataka majina ya wauza unga - sipati jibu isipokuwa JK kashindwa kuwataja! yaani vurugu tupu hakuna tunachosimamia na chenye kuingia akilini. Mkuu wangu, kama wapo wauza unga rais anaruhusiwa kuwasema popote pale na kama sii mila za Kikristu basi hata Pengo hakuruhusiwa (kumtolea uvivu JK) zungumzia maswala ya Unga ktk sherehe za Kikristu..
Acha khili la kanisani, ni JK huyu huyu alipopewa list ya wauza Unga na Marehemu Amina Chifupa ktk moja ya sherehe za Kitaifa alisema anayo list ya wauza unga na kuonya wanaofanya vitendo hivyo.... Alisema nakumbuka vizuri na tukaanza kusubiri lini ataifanyia kazi..Sasa tunachoweza kumlaumu ni kwa nini hajaifanyia kazi hadi leo hii na uzembe wake utokane na kutoifanyia kazi siii kwa sababu alisema ktk mkutano wa Kitaifa kwamba anayo list na majina ya wauza Unga!..Na hili halihitaji mkuu wa dini yoyote kutufahamisha kwamba JK sii rais mzuri tunalijua sana kuliko hawa viongozi wa dini ambao wote kwa ujumla wao walimpa support JK ktk chaguzi zote mbili zilizopita... Siii viongozi wa kiiislaam wala wakristu.
Hivyo mkuu wangu namalizia kwa kusema hivi, hoja nzima ya kumkashifu JK haina mshiko isipokuwa ni UDINI unaoendeshwa na vuyombo vya kidini.. Na samahani sana nitarudia kusema JK anachukiwa ktk hili sii kwa sababu nyingine isipokuwa yeye ni Muislaam kawakashifu wakristu na maswala ya kuuza unga ingawa kweli wapo waliokamatwa.. Ilitakiwa Usiri fulani, sio kuyasema maswala ya unga hadharani kwani sii utamaduni wa kanisa -Sawa na mtu kumwambia mzazi aliyejamba - Umejamba, hili ni kosa la kitamaduni...