Pengo amtolea uvivu Kikwete

Pengo amtolea uvivu Kikwete

Mkirua, naona umeguswa pabaya sana. Ukitaka kulia lia, ukitaka kujinyonga jinyonge lakini nchi yetu hamtaiuza kamwe, si kwa madawa wala kwa Rozari. Wewe ni mshika mkia tu wala hujui kinachoendelea, tena uko nyuma sana hata kukusaidia ni kazi kwewli kweli.

Ungekuwa ni nyama ungeiva kwa umeme tu na kidogo kwa Gasi. Maana kichwa chako ni kigumu sana kuelewa, na hata ukielewa ni mwepesi sana kusahau. Fuatilia historia ya kanisa karoliki kwq kipindi cha miaka 30 tu iliyopita na angalia mabaya walyoyafanya bila kufichuana wenyewe kwa wenyewe. mKIRUA polleeeee!

1. Tatizo lako kubwa unadhani wote wanaotetea kauli ya pengo humu ni Wakatoliki na Wanamtetea Kikwete ni Waisilamu. Haya ni mawazo mepesi sana pengine ukaendelee kule Face Book .Kama hata utambuzi wa jambo dogo kama hilo huna sitegemei kuwa unaweza kuelewa kingne chochote.

2. Kwenye hoja yako ya kuuza nchi ungetuambia wewe ni nani na sisi tunaotaka kuuza nchi ni kina nani ili nijue naongea na nani though wenye akili tumeshakujua ni Masalia.

3. Ushauri wako wa kufuatilia Kanisa Katoliki kwa miaka 30 iliyopita anzisha Thread weka hoja upewe majibu.

4. Mwisho nasisitiza hoja ya msingi hapa ni Pengo kampasha Kikwete Live. Najua kiongozi wa dhehebu lako hana ujasiri wa Pengo na wala hathubutu na hata akisema ukiweka Thread humu hakluna atakayechangia na hicho ndicho kinachokuumiza zaidi na kuishia kujadili watu badala ya hoja. Huo ni mwanzop tu ndio faida ya kuwa na viongozi wa dini ambao wamekwenda shule...

Kanisa katoliki ni jasiri duniani kote na itabaki hivyo ... Subiri mazito zaidi kwani kwa Serekali lege lege inayoogopa hata kuwataja wahalifu sembuse kuwashughulikia haiwezi kutufikisha popote. Ningekuona shujaa ungetumia jina lako halisi hapa halafu tukuchunguze miaka 30 iliyopita na sio Kanisa Katoliki kama unavyotaka wewe. Anza kwako binafsi.
 
Deconstructing this from 360 degrees.

Pengo nimemuelewa anavyompaka Kikwete kwa kutumia kanisa kama bullpit ya wanyonge, liberation theology and all. Nimeshaongelea hayo mwanzo huko, Kikwete kachemsha kwa kuendekeza kauli na kushindwa ku act zaidi.

Lakini ana maana gani anapoongelea "utukufu" ? Anaongelea katika context ya greatness au kuna religious connotations?

Kuna mtu ka mention hapo juu. Ana maana gani anapoongelea "kutawala" mataifa mengine? Ana maana ya "dominance" as in economic and social/cultural au some type of neo-neo-colonialism ?

Na kwa nini Kardinali msomi aseme maneno ambayo yanaweza kuwa misinterpreted kirahisi hivi?
 
Hawa wakinyamaza mawe yatapiga kelele. Alihamua kumpa muda muheshimiwa ili atekeleze agizo la CCT lakini wapi. Akadhani angetumia busara awataje lakini wapi. Ukumbuke kuwa Pengo alikuwa akihutubia ibada ya Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwahiyo alikuwa huru kuzungumzia lolote lililomkera zaidi kwa miaka 50 ya uhuru wetu. Think Loud.
Yaani Pengo anampa muda rais wa Jamhuri ya Tanzania muda wa kutekeleza AGIZO la CCT.. jamani nyie mko wapi haswa! mbona mnataka kuiteka nchi hii kwa maneno yenu ya dharau kiasi hiki kwa rais wetu as if hii ni nchi inaongozwa chini ya viongozi wa dini.. JK hakuikashifu dini wala kanisa ila kasema wapo viongozi wa dini wanaojishughulisha na biashara ya Madawa ya Kulevya. Waache tabia hiyo, na sio hivyo tu majina yalikwisha tajwa na wengine tayari wameisha kamatwa na kesi zao zipo mahakamani (Lukuvi akihutubia bunge).. Sasa walokamatwa hao sii viongozi wa dini isipokuwa awe Askofu?..Kama hamridhiki na matokeo hayo basi yaonyesha mnayo majina zaidi ya waliokamatwa.

Na ipo wapi sheria ambayo inamtaka rais awataje wahusika na sii serikali yake kuwakamata?.. Pili wamekazania JJK awataje laa sivyo ni msaliti wa taifa mbona wao kisheria hawaruhusiwi kuwataja WAHALIFU walioungama..Je, ina maana hata wao husaliti Taifa!...

Sniper,
Mkuu wangu sina sababu ya kurudi nyuma kujaribu kukufahamisha kitu ambacho wewe hutaki kukielewa. Nakuomba soma kichwa cha habari, soma hoja za Pengo hasa pale zilipokuwa Highlighted kisha yatazame majibu yote ya Lukuvi bungeni..Hoja hapa ni hotuba ya JK kuhusiana na viongozi wa dini wauza Unga. Walikwisha kamatwa wahusika na kesi zao zipo mahakamani, leo Kardinali Pengo anamtaka JK awataje majina wauza unga kwa sababu ati CCT ilimpa muda (Ultimatum kind of a political game) awataje viongozi hao hata kama sii wa kanisa hilo.

Na kama sii wa kanisa hilo kwa nini alizungumzia kwenye sherehe za Wakatoliki.. Excuse me, kama ilikuwa hairuhusiwi JK angejuaje yote hayo.. Na kati ya matamshi ya JK siku hiyo na majibu ya Mchungaji Mokiwa wa KKT kulitokea mvutano mkubwa sana wa kidini ambao haukuwa na sababu kabisa. Udini ukatumika sana hadi ikafikia JK kuzungumzia usiri wa fedha kibao ambazo serikali yake inawapa makanisa.ikawa kuvuana nguo na matusi kiimani. Watu tukapiga makelele weee yakaisha, tukapumzika...

Haya hatujakaa sawa mara Pengo huyo kuendeleza libeneke ati JK awataje viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya. Jamani JK akiwataja hao viongozi huyo Pengo atawafanya nini?. Kwa nini Pengo anakazania JK awataje hao wauza Unga atakuwa kafanikisha kitu gani kama sii ubabe na kuwafurahisha kanisa lake mwenyewe.. Kuna siasa za ushindani wa kidini nchini na nina hakika kabisa Kardinali Pengo anajua fika walokamatwa ni viongozi wa makanisa mengine sio kanisa lake, pengine anachotaka watajwe ili wananchi wapoteze imani zao ktk makanisa hayo.. Mimi sijui, lakini sioni kabisa sababu ya maana kuwataja wauza unga badala ya kukamatwa kwa wauza unga. Mika yote intelijensia ya kesi za jinai kama kuuza unga hufanyika kwa usiri mkubwa sana hadi the all cartel imegundulika. Kuwaaja wahusika ni kupoteza ama kuharibu ushahidi mapema kabla hawajakamatwa.
 
Scarface ndio nani usije kuwa unatutajia wahuni wa Marekani wakati sisi tunajadili vitu vya msingi hapa

Angalia neno, usiangalie jina. Hata muhuni wa Marekani anaweza kukufundisha kitu, sio kila siku mashairi ya Shaaban Robert na Shakespeare tu.

Somo hapa ni, "Actions speaks louder than words".

Act Mr. President, we are tired of the empty talk.
 
Nakubaliana na wewe sana tu. Unajua ktk mikutano ya Umoja wa Mataifa ni rahisi sana kuwasikia Marekani wakitukana nchi zote na marais wao hata kuwapigia kura za veto lakini isitokee rais wa nchi nyingine azungumze maneno mazito dhidi ya serikali zao. Wao kwa mtindo wao hutoka nje na kusema ubaya wote wa matamshi ya huyo rais iwe kuhusu Ubeopari mamboleo ama Israel..

Labda nikuulize wewe kitu kimoja, Hapa tuna malumbano kutokana na kauli ya nani? JK kaifanya miezi miwili mitatu ilopita na wananchi wameisha sahau tunazungumzia maswala ya Umeme, maji na ufisaid unaoendelea. Huyu Mh. Kardinali katoka huko alikojificha siku zote kafumua donga ambalo angeweza kabisa kulitafutia ufumbuzi bila kupanda jukwaani na kumkashifu rais..

Pengo anamkashifu rais na maneno yake yamejaa dharau kubwa sana kwa sababu tu rais anawajua viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Na yawezekanakweli JK hakutakiwa kusema ktk mkutano huo.. Hata Obama kawahi kukosea kuzungumzua vitu mbele ya Malikia ambavyo hakutakiwa kusema, lakini alielekezwa. JK ni rais wa nchi na kama alifanya makosa kusema pale mbele ya mkutano wa maaskofu kwa sababu Kanisa huwa lina mambo ya Kisiri kisiri angefahamishwa.. lakini sioni kosa hata kidogo kwa rais kuwaonya wale wanaofanya vitendo hivyo waache kwa sababu Mapadre ni mfano mzuri wa viongozi wa jamii zetu.

Kama Pengo asingesimama majuzi na kusema yote haya, malumbano haya yasingekuwepo hivyo tufahamu kwamba Pengo ndiye sababu ya mada yoote hii na kutoelewana, jambo ambalo watu wanafanya uetetezi kwa sababu kiimani wanaamini Pengo hawezi kufanya makosa sii binadamu ni chaguo la Mungu na mwenye utume... Ni imani yenu na Naiheshimu!
- Nilikuwepo...
mkuu mkandara bado upo humu...! Mkuu ile kauli ya kikwete ilitukwaza sisi wakatoliki wote ...kwa hiyo ondoa kabisa katika mawazo yako eti kwa sababu tu Pengo kasema ndiyo maana tunamtetea kwa sababu tunaamini yeye hawezi kufanya makosa! Pengo ni binadamu na ana mapungufu yake mengi tu kama binadamu. Sema kauli yake kama kiongozi wa kanisa katoliki ina uzito fulani kama vile ya Kikwete ambaye ni rais wetu.
 
Angalia neno, usiangalie jina. Hata muhuni wa Marekani anaweza kukufundisha kitu, sio kila siku mashairi ya Shaaban Robert na Shakespeare tu.
Somo hapa ni,;Actions speaks louder than words
Act Mr. President, we are tired of the empty talk.

Muhuni, Mshenzi hawana nafasi kwangu ya kunifundisha kitu chochote! nadhani nafasi watapata kwako ndio mna utaratibu huo na sasa hivi Ibada zenu zinaendeshwa na wahuni Mapdri Mashoga!na hilo mnakubaliana nalo. Kama unavyosema muhuni anaweza kuwa na mawazo mazuri tu, lakini sio kwangu
 
mkuu mkandara bado upo humu...! Mkuu ile kauli ya kikwete ilitukwaza sisi wakatoliki wote ...kwa hiyo ondoa kabisa katika mawazo yako eti kwa sababu tu Pengo kasema ndiyo maana tunamtetea kwa sababu tunaamini yeye hawezi kufanya makosa! Pengo ni binadamu na ana mapungufu yake mengi tu kama binadamu. Sema kauli yake kama kiongozi wa kanisa katoliki ina uzito fulani kama vile ya Kikwete ambaye ni rais wetu.
Haswaa hili ndilo nilitaka kusikia.. Na wala sintawalaumu wakristu ikiwa watakuwa wakweli ktk imani na hisia zao za utukufu wa Pengo. Ni sawa na sisi waislaam unapozungumzia swala la Ugaidi huwa tunakwazwa sana na muhimu sana kwa mtu anapolizungumzia swala sensitive kama hili awe makini na kauli zake...

Lakini tuache yoote hayo, JK hakufanya kosa kabisa kwa sababu alikuwa na report ya viongozi wa dini kukamatwa (Wanigeria) na sii rahisi kuwatuhumu viongozi wa dini hasa ya Kikristu pasipo kujua connections zao za kimakanisa.. Na kama JK angemtaja mtu pale basi ingekuwa noma zaidi kwa sababu huyo mtu angedai ushahidi na ingeonekana vibaya zaidi kwa nini serikali yake isimkamate kwanza ikamfungulia mashtaka badala yake anakuja mbele ya hadhara ya watu ktk sherehe ya Kikristu kumtaja mhalifu!

Hivi kweli hata wewe unaona mantiki ktk hili yaani JK kuwataja wauza unga mkutanoni badala ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka! ikiwa hivyo kina Dr.Slaa watafanya nini?.. Believe me, hii ingekuwa mbaya zaidi lakini katumia kauli hafifu ya kuwaomba viongozi wa dini waache biashara ya unga (diplomacy) yaani mwenyewe kajishusha na kuwa mdogo kwa sababu biashara ya unga ni cartel iliyojipanga vema na ina mlolongo wa vyanzo, middle hadi soko. Hatab huku majuu nmarais huwaonya gangs leader wa Mafia, bikers na Mexican na kadhalika kwa sababu sii rahisi kujua nani yupo ndani nani yupo nje..

Hivyo kujishusha kwake ndio huyo mchungaji Dr. Mokiwa wa KKT akapata nguvu na kumpa Ultimatum rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ati awataje hao wahusika wa madawa ya kulevya laa sivyo sijui ndio wangemwondoa ktk madaraka au!. Na from that day, ilikuwa dharau tupu kwa rais kama vile Church is above the government.. I'm sorry bob hii ni imani yenu na mna kila haki ya kuchukizwa na maneno ya JK lakini msisahau kwamba JK ni rais wa watu wote hata kama hapendeki....Na kumbuka pia hatumpendi sote kama utawala wake lakini sii ktk swala hili la viongozi wauza unga kwa sababu wapo kweli...
 
Bada ya kuufuatilia huu mjadala, nimegunduwa JK alifanya makusudi tu kuanzisha haya yote. Nimegunduwa kuwa si kwamba tu kauli ile hakuisemea pahala pake, bali pia ni kauli mbovu. Nina sababu nyingi tu za ku back up hayo makosa yake mawili makubwa tu. Wengine wameshafanya hapo nyuma.

However sidhani kama kuna atakayebadili mawazo kwasababu issue kama imeingilia upinzani wa kidini.

JK knows what he is doing.
 
Hoja ya wengi wanaomtetea Rais Kikwete hapa ni kwamba Kardinali Pengo “kamdharau” Rais. Be that as it may, lakini kama Rais anafanya kitu kinachoweza kumletea dharau basi ni haki kumdharau. Hatuko tena kwenye zama za utawala wa kiimla ambapo akishasema Rais kila mtu anafyata mkia.

Rais akikosea ni ruhusu kumkosoa. Akisema kitu cha kujidharaulisha ni ruksa kumdharau. Ni haki yetu kumdharau Rais inapobidi.
Kiongozi “kusaliti” wananchi maana yake ni to let them down, na si vinginevyo. Stop spinning people! Haina maana ya treason.

Tuache kabisa hii kasumba ya akina Mkandara ya kusema hatuwezi kumdharau Rais. Kwanini tusiweze? Akijidhalilisha lazima tumdharau.

.Na kumbuka pia hatumpendi sote kama utawala wake lakini sii ktk swala hili la viongozi wauza unga kwa sababu wapo kweli...

Sawa lakini hiyo ilikuwa chini ya hadhi yake kama Rais. Matamshi ya namna hii alipaswa kutoa kiongozi au viongozi wa Polisi kama Inspector General Said Mwema et al., siyo Rais wa Jamhuri. Hapo ni wazi Kikwete alikuwa anatumia ujanja wa "red herring" ku-divert attention ya Watanzania kutoka matatizo yao ya msingi kama ukosefu wa nishati ya umeme, na kadhalika.

Na amini usiamini wapuuzi wachache wameingia mkenge kama ilivyokuwa na ule utapeli wa "Babu wa Loliondo". Halafu nadhani hii kauli yake vilevile ina elements fulani za udini. Its obvious it was aimed at Christians only, and he was trying to take a swipe at them for reasons he knows best.
 
Augustine Moshi,
Mkuu wangu karibu tena na nadhani itabidi nikupe heshima yako kwanza mwalimu..Good Evening Sir!..

Kuhusu mada hii kama umegundua imejijenga ktk hisia za Udini na sii swala la watu kumtetea JK ila ni swala la watu kukataa Pengo ahakufanya makosa...na hii yote inatokana na Udini yaani kiongozi kama Pengo hawezi kufanya makosa na sii swala la JK ambaye tunajua vizuri kwamba hafai anaweza fanya makosa yoyote na wakati wowote.. Huyu hana Mjadala hata kidogo.
Kinyume cha hapo hakuna anayepinga kwamba kulingana na mila na desturi za kikanisa, PENGINE JK alifanya makosa kusimama pale jukwaani ktk sherehe za kidini na kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa dini kujishughulisha na madawa ya kulevya hata kama kulikuwa na UKWELI..Ni makosa ya kutofahamu mila na desturi za kikristu.

Kwa hiyo hii ndio issue mkuu wangu na hakuna mtu anayemtetea JK isipokuwa hatuoni uzito wa hoja nzima kuifanya iwe lazima JK awataje wahusika! na niimeuliza mara kumi kidogo.. Mnataka JK awataje wahusika ili ijewe? sijapata jibu muda wote..Na nyie ndio mnamtetea Pengo na kama mnakubali Pengo kafanya naye makosa basi mjadala huu umekwisha na tuufunge. Lakini hilo sidhani kama linawezekana! hakuna mmoja wenu yupo tayari kusema hivyo na hamna sababu zaidi ya nguvu ya Kardinali Pengo ktk imani ya dini..Kwangu mimi swala hili lilikwisha siku nyingi na watu tulishalisahau mawe ya Udini waliyorushiana siku JK alipotoa kauli hiyo hadi aliposema viongozi hao walishakamatwa na wapo mahakamani - Case closed..

Tulikuwa poa kabisa na pengine tumesahau kabisa Udini Kitaifa, mara Pengo kaamsha mizimu iliyolala, ghafla kuchaganya madawa ili kwamba JK aonekane sii kiongozi bora Kitaifa kwa maswlam ya kikanisa hapo ndipo anapokosea. Swala la viongozi kuuza unga jingine na kweli wapo viongoizi waliojihusisha na biashara za Unga na swala la udhaifu wa JK kuongoza nchi yetu jingine ambalo sote tunamlaumu bila wino wa Pengo au Mokiwa..Statement ya JK hakuitoa jana wala juzi siku miezi imepita na kama Pengo angetaka majibualikuwa na muda wa kufanya hivyo kiofisi maanake yeye ni Mkuuwa kanisa la katoliki na balozi wa Vatican hivyo anaweza kuingia Ikulu kama anaingia chooni tu..
 
Statement ya JK hakuitoa jana wala juzi siku miezi imepita na kama Pengo angetaka majibualikuwa na muda wa kufanya hivyo kiofisi maanake yeye ni Mkuuwa kanisa la katoliki na balozi wa Vatican hivyo anaweza kuingia Ikulu kama anaingia chooni tu..

Huyo Kikwete alifanya makusudi kabisa kutumia wadhifa wake na occasion au hafla husika, ambayo ilikuwa mbele ya "waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga wakati wa ibada maalumu ya kupewa daraja la uaskofu" kuja na kauli zake ambazo mpaka leo ameshindwa kuthibitisha licha ya kutakiwa kufanya hivyo na walengwa.

Kwa hiyo, kutokana na mazingira kama haya, ni nini cha kushangaza kwa hatua hii ya Kadinali Pengo kama Mkuu wa Kanisa Katoliki ku-react kwa kutoa kauli ya wazi kwa Watanzania wote kama alivyofanya Kikwete mbele ya umma ya Watanzania wote? Tunasubiri Kikwete atoe kauli kama hiyo mbele ya Iddi Baraza ijayo dhidi ya wauza unga wa Kislamu ambao kwa miaka mingi wamekithiri na wamekuwa wakitumia kivuli cha kwenda hijja Mekka kuingiza madawa kutoka nchi za Kiislamu kama Afghanistan, Iran na Pakistan.
 
Sawa lakini hiyo ilikuwa chini ya hadhi yake kama Rais. Matamshi ya namna hii alipaswa kutoa kiongozi au viongozi wa Polisi kama Inspector General Said Mwema et al., siyo Rais wa Jamhuri. Hapo ni wazi Kikwete alikuwa anatumia ujanja wa "red herring" ku-divert attention ya Watanzania kutoka matatizo yao ya msingi kama ukosefu wa nishati ya umeme, na kadhalika.

Na amini usiamini wapuuzi wachache wameingia mkenge kama ilivyokuwa na ule utapeli wa "Babu wa Loliondo". Halafu nadhani hii kauli yake vilevile ina elements fulani za udini. Its obvious it was aimed at Christians only, and he was trying to take a swipe at them for reasons he knows best.
Hapana mkuu wangu hata Obama huku huja ktk sherehe zetu na kuzungumzia mambo ya drugs na sii kiongozi wa Polisi au Mwema licha ya hivyo Mwema hakualikwa. Na kama angesema Mwema sii ndio angeikosa hata kazi yake maana kanisa lingeshinikiza afukuzwe kazi ! haaa haa! true though!

... Kusema kweli Kama Mkapa angekuja na usema kuna baadhi ya Masheikh wanajihusisha na biashara za Unga iwe siku ya Maulidi au sijui Idd Fitr , mimi sioni makosa unless Mkapa ktk hotuba yake ahalalishe matumizi ya Unga. Kisha sioni sababu ya kumtaka JKK ataje majina kwa sababu majina hayo ndio yanafanyiwa uchunguzi wa kukamatwa wahusika wate na akitwaja tutakuwa tumeharibu upelelezi wote..

Kitendo cha Pengo kumtaka rais awataje wahusika ni chini ya hadhi ya Kardinali na pia ni dharau kumpa ultimatum rais wetu kutoa majina ambayo hana kazi nayo ila isipokuwa kutunisha misuli kuonyesaha nguvu ya kanisa (utanisamehe ktk hili) kwani hata mimi ambaye sina elimu na hekima kama yeye sioni nje - anayataka majina hayo ili ijewe na hakuna mtu aliyeweza kunifahamisha..
 
Hapana mkuu wangu hata Obama huku huja ktk Hood na kuzungumzia mambo ya drugs na sii kiongozi wa Polisi au Mwema licha ya hivyo Mwema hakualikwa. Na kaa angesema Mwema sii ndio angeikosa hata kazi..kanisa lingeshinikiza afukuzwe kazi...

Kusema kweli Kama Mkapa angekuja na usema kuna baadhi ya Masheikh wanajihusisha na biashara za Unga iwe siku ya Maulidi au sijui Idd Fitr , mimi sioni makosa unless Mkapa ktk hotuba yake ahalalishe matumizi ya Unga. Kisha sioni sababu ya kumtaka JKK ataje majina kwa sababu majina hayo ndio yanafanyiwa uchunguzi wa kukamatwa wahusika wate na akitwaja tutakuwa tumeharibu upelelezi wote..

Kitendo cha Pengo kumtaka rais awataje wahusika ni chini ya hadhi ya Kardinali na pia ni dharau kumpa ultimatum rais wetu kutoa majina ambayo hana kazi nayo ila isipokuwa kutunisha misuli kuonyesaha nguvu ya kanisa (utanisamehe ktk hili) kwani hata mimi ambaye sina elimu na hekima kama yeye sioni nje - anayataka majina hayo ili ijewe na hakuna mtu aliyeweza kunifahamisha..

Kwanza kabisa, usijaribu hata kidogo kumlinganisha kiboda kama Kikwete na Obama. There's simply no comparison. Kubali, usikubali, Marekani siyo Tanzania, sawa? Pili, ni wazi hii ishu huielewi, vinginevyo usije kuja na kauli za namna ya "kama Mkapa angekuja na usema kuna baadhi ya Masheikh wanajihusisha na biashara za Unga iwe siku ya Maulidi au sijui Idd Fitr , mimi sioni makosa unless Mkapa ktk hotuba yake ahalalishe matumizi ya Unga."

Pengo siyo tu kwamba amehudhunishwa sana bali pia ni wazi amekosewa heshima na kudhalilishwa na Rais ambaye amechaguliwa na wapiga kura waliyo Waislamu na Wakristo na ambaye alialikwa kwenye shughuli hiyo kwa nia njema, na baadaye kuwageuka walioyomulika kwa kuanza kubwata kuhusu "ufahamu wake wa wauza unga" mbele ya kadamnasi ya Wakristo Wakatoliki tu. Jee, hii inaashiria nini kwa mtu mwenye akili zake timamu?
 
Kwanini Pengo ilimuuma ile kauli ya Kikwete? au ni mmoja wa washukiwa.

lakini siku hizo hana uzito wowote kulinganisha na Wakati za Nyerere.

Mwambie raisi wako amtaje basi, uzito gani sasa, inahusu nini, wewe na hilo kanzu hautajua ni sawasawa na pilipili usiyoila! Au akili yako nzuri inaona hiyo kauli siyo ya kweli, endeleeni kuwauzia unga ndugu zenu Zanzibar huko kwa sababu nyiye ni rizki kuuza madawa ya kulevya.
 
Nakubaliana na wewe sana tu. Unajua ktk mikutano ya Umoja wa Mataifa ni rahisi sana kuwasikia Marekani wakitukana nchi zote na marais wao hata kuwapigia kura za veto lakini isitokee rais wa nchi nyingine azungumze maneno mazito dhidi ya serikali zao. Wao kwa mtindo wao hutoka nje na kusema ubaya wote wa matamshi ya huyo rais iwe kuhusu Ubeopari mamboleo ama Israel..

Labda nikuulize wewe kitu kimoja, Hapa tuna malumbano kutokana na kauli ya nani? JK kaifanya miezi miwili mitatu ilopita na wananchi wameisha sahau tunazungumzia maswala ya Umeme, maji na ufisaid unaoendelea. Huyu Mh. Kardinali katoka huko alikojificha siku zote kafumua donga ambalo angeweza kabisa kulitafutia ufumbuzi bila kupanda jukwaani na kumkashifu rais..

Pengo anamkashifu rais na maneno yake yamejaa dharau kubwa sana kwa sababu tu rais anawajua viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Na yawezekanakweli JK hakutakiwa kusema ktk mkutano huo.. Hata Obama kawahi kukosea kuzungumzua vitu mbele ya Malikia ambavyo hakutakiwa kusema, lakini alielekezwa. JK ni rais wa nchi na kama alifanya makosa kusema pale mbele ya mkutano wa maaskofu kwa sababu Kanisa huwa lina mambo ya Kisiri kisiri angefahamishwa.. lakini sioni kosa hata kidogo kwa rais kuwaonya wale wanaofanya vitendo hivyo waache kwa sababu Mapadre ni mfano mzuri wa viongozi wa jamii zetu.

Kama Pengo asingesimama majuzi na kusema yote haya, malumbano haya yasingekuwepo hivyo tufahamu kwamba Pengo ndiye sababu ya mada yoote hii na kutoelewana, jambo ambalo watu wanafanya uetetezi kwa sababu kiimani wanaamini Pengo hawezi kufanya makosa sii binadamu ni chaguo la Mungu na mwenye utume... Ni imani yenu na Naiheshimu!
- Nilikuwepo...
Issue siyo Pengo, wala JK, issue ni hao viongozi wa dini, kama ni waovu watajwe, kama kuna usiri usiri angesema vipi sasa umtaje hata yeye kama ni mmoja wao, sasa unajichanganya tu na unaonyesha inferior-ism yako. Let the point be independent, halafu kuhusu watanzania kusahau sahau ghafla mambo hata km ni mazito, ninyi ndiyo mna-take advantage of that fraud. Hata huoni aibu!
 
Kardinali Pengo alisema kitendo cha Rais Kikwete pamoja na baadhi ya viongozi waliojitokeza kuzungumzia suala hilo huku wakisema hawawezi kuwataja kwa majina, huo ni usaliti mkubwa kwa taifa.

"Haiwezekani mtu mkubwa tu, wala siyo mdogo kuja katika eneo la Kanisa la Katoliki, kukiwa kumejaa Maaskofu kutoka karibu nchi nzima, unasema maneno haya halafu unasema, siyo nyie ni viongozi wa makanisa madogomadogo," alilalamika Kardinali Pengo.

Aliongeza kwamba: "Kama ndivyo hivyo kwa nini sasa uje kuyasema maneno hayo katika eneo la Kanisa Katoliki."

Hivi eneo la kanisa sio Tanzania??
 
Bravo JK umempa vidonge, pengo aoe kisha azae ndipo ataona uchungu wa kuwaona watoto wetu wakitumia madawa ya kulevya
 
kutaja nako kwaitaji hekma jamani tumpatie muda raisi ili ajipange aweze kuwataja kwa wakati muafaka.
 
Haswaa hili ndilo nilitaka kusikia.. Na wala sintawalaumu wakristu ikiwa watakuwa wakweli ktk imani na hisia zao za utukufu wa Pengo. Ni sawa na sisi waislaam unapozungumzia swala la Ugaidi huwa tunakwazwa sana na muhimu sana kwa mtu anapolizungumzia swala sensitive kama hili awe makini na kauli zake...

Lakini tuache yoote hayo, JK hakufanya kosa kabisa kwa sababu alikuwa na report ya viongozi wa dini kukamatwa (Wanigeria) na sii rahisi kuwatuhumu viongozi wa dini hasa ya Kikristu pasipo kujua connections zao za kimakanisa.. Na kama JK angemtaja mtu pale basi ingekuwa noma zaidi kwa sababu huyo mtu angedai ushahidi na ingeonekana vibaya zaidi kwa nini serikali yake isimkamate kwanza ikamfungulia mashtaka badala yake anakuja mbele ya hadhara ya watu ktk sherehe ya Kikristu kumtaja mhalifu!

Hivi kweli hata wewe unaona mantiki ktk hili yaani JK kuwataja wauza unga mkutanoni badala ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka! ikiwa hivyo kina Dr.Slaa watafanya nini?.. Believe me, hii ingekuwa mbaya zaidi lakini katumia kauli hafifu ya kuwaomba viongozi wa dini waache biashara ya unga (diplomacy) yaani mwenyewe kajishusha na kuwa mdogo kwa sababu biashara ya unga ni cartel iliyojipanga vema na ina mlolongo wa vyanzo, middle hadi soko. Hatab huku majuu nmarais huwaonya gangs leader wa Mafia, bikers na Mexican na kadhalika kwa sababu sii rahisi kujua nani yupo ndani nani yupo nje..

Hivyo kujishusha kwake ndio huyo mchungaji Dr. Mokiwa wa KKT akapata nguvu na kumpa Ultimatum rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ati awataje hao wahusika wa madawa ya kulevya laa sivyo sijui ndio wangemwondoa ktk madaraka au!. Na from that day, ilikuwa dharau tupu kwa rais kama vile Church is above the government.. I'm sorry bob hii ni imani yenu na mna kila haki ya kuchukizwa na maneno ya JK lakini msisahau kwamba JK ni rais wa watu wote hata kama hapendeki....Na kumbuka pia hatumpendi sote kama utawala wake lakini sii ktk swala hili la viongozi wauza unga kwa sababu wapo kweli...
mkuu naona sasa unajichanganya...! haya ni maneno yako mwenyewe! "Na kama JK angemtaja mtu pale basi ingekuwa noma zaidi kwa sababu huyo mtu angedai ushahidi na ingeonekana vibaya zaidi kwa nini serikali yake isimkamate kwanza ikamfungulia mashtaka badala yake anakuja mbele ya hadhara ya watu ktk sherehe ya Kikristu kumtaja mhalifu!".
Tunarudi kulekule...kikkwete hakutakiwa kutoa kauli kama ile kwenye kusanyiko la maaskofu wakatoliki peke yao! inaonekana kama vile alikuwa anawalenga wenyewe tu . Kama angekuwa sehemu neutral au kwenye hafla inayowahusisha viongozi wa dini zote(waislam, wakristo, hindu whatever) na angetoa kauli ile ....ingeleta mantiki nzuri kabisa!
Kilichotuudhi wengine zaidi ..ni kwamba inaonekana hiyo statement ilikuwa kama vile imepangwa kabisa . Soma hii excerpt kutoka mwanahalisi [Kauli hii ya maaskofu kuuza unga ilifuatiwa na vipindi vya televisheni kwenye TBC vilivyoandaliwa kuhalalisha hoja hiyo. Katika moja ya taarifa hizo, walionyeshwa vijana walioathirika na madawa ya kulevya wakieleza kuwa madawa hayo huingizwa nchini na viongozi wa dini.]
Mimi binafsi niliona kipindi kesho yake channel ten ..alikuwapo Nzowa naye akiwa anajaribu kujustify kauli ya Kikwete!
Mlolongo wa vitu vyote hivyo vinaonyesha kuwa kuna kitu fulani kilikuwa kimekusudiwa nyuma ya kauli ya Kikwete.
 
Back
Top Bottom